Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Watu wenye magari yao ndio hawajua haya sticker za bima, sasa sisi tunaendesha baiskeli ndio tunajua hizi sheria vizuri kabisa .....
 
trafic kakupiga chief. kama ameangalia kwenye system ikaonekana imeshakatiwa kakupiga. mimi nina ofisi ya uwakala ya bima. nenda peleka malalamiko yako ngazi ya juu. huyo trafik atalipishwa.
 
Sheria haijabadilika, Askari akiamua kukuandikia atakuandikia na utalipa.
Msilotoshe watu, Sheria bado ipo palepale.

Kinachopaswa kufanywa ni kubadili hiyo sheria
Nimesema askari na mtoa mada hawapo updated , sijasema kwamba sheria hiyo haipo. Kuna vitu vinakufa automatically kwa sababu ya technology, ni swala la kutumia tu common sense.

Ni kama vile vocha za kukwangua, haijakatazwa na ipo, lakini kwa wanaojielewa, hakuna sababu ya kununua vocha ilhali kuna uwezekano wa kununua muda wa maongezi na vifurushi kupitia m pesa and the likes

Kada ya Askari kwa wengi ni option ya failures, na ndio sababu tunasumbuana barabarani kwa vitu ambavyo hata havina maana.

Hapo zamani kabla ya mambo ya technology, njia pekee ya kujua uhai wa bima ilikuwa ni kupitia hiyo sticker, na ndio iliwekwa hiyo sheria, siku hizi hata wewe mwenyewe unaweza kulifanya hilo kupitia simu ya mkononi.
 
Utaratibu haufuti Sheria, Bali Sheria ndio hufuta utaratibu.
Sheria ndio zinaongoza nchi
Mkuu
Sheria za Tanzania nyingi tulitoa kutoka kwa wakoloni hasa Uingereza , kwa wenzetu ni wepesi sana kufanya marekebisho , sisi huku kwetu tunachelewa sana kufanya hivyo kwa sababu kuna ya baadhi ya sheria hata kuzitafisiri tu ilikuwa shida .Tanroads kwa mfano anatumia length standards za Uk. Bila kujua Uk waliweka sheria hizo kwa kuwa hawana eneo kubwa la maegesho, .

Sheria zilizopitwa na wakati inahitajika busara kutumia common sense .
 
trafic kakupiga chief. kama ameangalia kwenye sistm ikaonekana imeshakatiwa kakupiga. mimi nina ofisi ya uwakala ya bima. nenda peleka malalamiko yako ngaz ya juu. huyo trafik atalipishwa.
Trafiki kwa hali ya sasa ilitakiwa recruitment yao at least wachukuliwe watu wenye elimu kiwango cha kuridhisha Wanasumbua sana .

Mtu anakukomalia na kuandikia , ati una speed 53 kwenye 50nkm/h zone!!!, Huyu mtu somo la errors and calibration aliwahi hata kulisikia kweli?, Kwamba chombo( gari) au , hiyo tochi yake vinaweza kuwa vinakosea kwa asilimia kadhaa, na kimantiki inakubalika ?

Sheria inasema limit ni 50km/h , sawa lakini ukipelekwa mahakamani unashinda mapema tu, inaeleweka , Askari wa barabarani kwa sababu hajui anakukomalia na anakuandikia fine.
 
Kuna sheria zinabadilika automaticaly zamani kweli ilikuwa lazima akague sticker , na watu walikuwa wana foji sana hizi sticker , siku hizi stiker haina maana na haisadii chochote zaidi ya kuweka uchafu pale kwenye kioo,
Vitu vipo online
Sheria haibadiliki automatic mkuu. Sheria inafanyiwa mabadiliko
So hapa walitumia sheria halali kabisa kunipiga fine.
 
Siku hizi stika za kubandika kwenye kioo za Bima hazitolewi manake waliona mastika Mengi ni feki.
Wewe na huyo traffic wote mtakuwa vilaza
Insurance siku hizi inaangaliwa kidigitali
Sheria haujui
 
Nimesema askari na mtoa mada hawapo updated , sijasema kwamba sheria hiyo haipo. Kuna vitu vinakufa automatically kwa sababu ya technology, ni swala la kutumia tu common sense.

Ni kama vile vocha za kukwangua, haijakatazwa na ipo, lakini kwa wanaojielewa, hakuna sababu ya kununua vocha ilhali kuna uwezekano wa kununua muda wa maongezi na vifurushi kupitia m pesa and the likes

Kada ya Askari kwa wengi ni option ya failures, na ndio sababu tunasumbuana barabarani kwa vitu ambavyo hata havina maana.

Hapo zamani kabla ya mambo ya technology, njia pekee ya kujua uhai wa bima ilikuwa ni kupitia hiyo sticker, na ndio iliwekwa hiyo sheria, siku hizi hata wewe mwenyewe unaweza kulifanya hilo kupitia simu ya mkononi.
Mkuu askari aliverify uhai wa BIMA kupitia machine na kukuta kweli BIMA ni halali, Sheria aliyotumia yeye kunipiga fine ni kuwa sijabandika stika kioo cha mbele upande wa kushoto.

Hii ni sheria imeorodhoshwa kwenye machine zao.
 
siku hizu hata ukienda kukata bima physically hupewi sticker ila unapewa COVER NOTE.. printout ya A4 kama kakitini hivi sasa unabandikaje kwenye kioo!!? we jamaa inaonekana kilaza somewhere.
 
Mkuu, kivipi. Siku hizi ukienda kukata Bima haupewi kile cha kubandika ila unapewa tu katarasi kubwa ya A4 inayoonesha umelipia Bima. Sasa utabandikaje?
Bandika A4 hivyo hivyo , kwa mujibu wa sheria🤣🤸‍♂️🐒
 
Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kinachotembea!🐒🐒🐒
20210421143347.jpg
 
Wana JF

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo. !

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakua hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.
 
Wana JF
Hii changes iliyofanyika ya kutoka katika Sticker za kubandika kwenye kioo mpaka sticker za kielectroniki ni kitu iliyofanya na Serikali chini ya Mamlaka Ya Bima Tanzania (TIRA).
Kwakweli tunapata changamoto kubwa kwa sisi wata Huduma sababu inaonesha moja kwa moja (Trafic na TIRA) awajapeana mwongozo wa kutosha juu ya Hii sheria ya kutokubandika sticker, na ndio maana wanaoendelea kuhumia ni wateja wote wa Magari,
Changamoto ya kwanza ni kuwepo kwa Mitandao Miwili ya kuhakiki Uhai wa Bima, hii inawachanganya watumiaji wa vyombo, sababu sas nyingine yeye anakuwa ajui gari yake ipo kwenye mfumo mpya au wa zamani, na polisi wa barabarani pia awajui kuangalia mifumo yote miwili, anaweza kukagua mfumo wa kwanza na akakuta gari haina Bima Hai na kumbe gari imekatiwa bima yake katika mfumo mpya.

NB: naishauri Serikali Chini ya Mamlaka ya Bima na Chini ya Polisi Tanzania wakae vzr kuweka sawa juu ya haya mabadiliko yaliyotokea , na juu ya izi system mbili zinazotumika kukagua bima ili mwisho wasiki watumiaji wa chombo kama kalipia Bima yake aisweze kupata usumbufu wa aina yoyote barabarani. Walink system zote mbili , mwenye chombo asiweze kujua yupo katika system mpya au ya zamani sababu ni kumchanganganya mnunuzi wa bima

Zaidi, kwa sasa Hakuna tena sticker za kubandika za bima kama mwanzo, hii imeanza kutumika tokea tarehe 1/4/2021 na Mamlaka walitoa Tangazo mpaka kwenye magazeti (Attached) na tuna Uhakika pia Polisi ilipewa mwongozo juu ya kuwepo na mfumo wa kielectroniki na sio tena kutumia Sticker za kubandika kwenye vioo.
(Sasa wa kulaumiwa ni TIRA AU POLISI)

TIRA ilitoa sababu kuu za kutoa mfumo wa sticker na kuleta mfumo wa kielectroniki kama attachment inavyoeleza

77B3A0C8-7BDB-4CEE-8568-8861C4A262A1.jpeg

F1D62809-DA83-42DB-8047-3710C567CF7F.jpeg
 
Aisee hiyo kali watu wote wanapita bila kubandika wewe ndio kasema sheria na bima umekata ni kweli sheria inasema hivyo ila kwa utaratibu wa sasa ulitakiwa kuhoji mpaka huko mbele na mkae na huyo askari na boss wake ikiwezekana mpaka hiyo kampuni ya Bima waliokukatia mnapoteza hela kirahisi mno...
 
Mkuu Maxence Melo na Mods,tunaomba mtutafutie watu wa TIRA na Jeshi la Polisi - Usalama Barabarani ili waje kutolea ufafanuzi swala hili pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani na sheria zake (kwa jeshi la polisi).
Madereva wengi Tanzania hatujui sheria wala alama za usalama barabarani kwani wengi wetu hatujaenda shule za udereva,hivyo ni vyema elimu hii ikatolewa humu jukwaani na penye mijumuiko ya watu ikiwezekana.
 
Wana JF

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo. !

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakua hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.

“Hii walikuwa wanafanya hivyo tangu mwanzo kaka,

Akikuta kwa system haipo hujaweka stiker fine, akikuta sticker umeweka ila kwa mfumo haipo ni kosa pia, so bado huyu askari ana hang over,

Kama huamimi mtafute huyu bwana tupate ile risiti yake ya fine halafu kitakachofuata kwa huyu askari kitafurahisha na kuwa fundisho kwa wengine”

Jibu nimepewa na mdau[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu Maxence Melo na Mods,tunaomba mtutafutie watu wa TIRA na Jeshi la Polisi - Usalama Barabarani ili waje kutolea ufafanuzi swala hili pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani na sheria zake (kwa jeshi la polisi).
Madereva wengi Tanzania hatujui sheria wala alama za usalama barabarani kwani wengi wetu hatujaenda shule za udereva,hivyo ni vyema elimu hii ikatolewa humu jukwaani na penye mijumuiko ya watu ikiwezekana.

Sasa si tuende shule kwanza ama?[emoji1787]
 
Back
Top Bottom