Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Hatuuzi nje na pia tunanunua sana toka nje
Nchi zinazoongoza kuuza nje na sababu zao....

1)Afrika Kusini....
2)Nigeria
3)Misri
4)Algeria
5)Morocco

Hivi kweli tunaweza kujifananisha nao?!!!!

Mathalani....Nigeria ina raia milioni 220....Misri ina raia milioni 110.....

Kigezo cha idadi kubwa ya Raia na sababu nyinginezo zinachangia kutuzidi parefu.....

1)Viwanda vingi
2)Elimu kwa raia wao

Afrika ya kusini ijapokuwa tumewazidi idadi ya raia lakini inajulikana UWEKEZAJI MKUBWA WA MAKABURU NA MAKAMPUNI YA NJE.......

Algeria na Morocco pamoja na sababu nyingine tusisahau wana DIASPORA wengi mno kutuzidi......

Tanzania inaendelea kukua kiuchumi kila uchao.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Usiwe na haraka....maswali yako utapata majibu wakati mh.Dr.Mwigulu atakaposoma bajeti mwezi wa 7 in shaa Allah...

#SiempreJMT[emoji120]
 
JPM atabaki katika kumbukumbu njema....

Ila USISAHAU.....

Ameacha miradi ya:

1)SGR

2)Bwawa la kufua umeme(MWALIMU NYERERE HYDRO ELECTRIC POWER PLANT) .

Miradi yote hiyo inahitaji Fedha na utawala wa awamu ya 5 haukulipa FEDHA yote kwa sababu ya kutokamilika kwa miradi......

Mh.Rais SSH anaendelea kulipa Fedha ili miradi hiyo ikamilishwe itakiwavyo.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Lakini sababu nyingine ni kuwepo Kwa mamiradi makubwa hapa Tanzania ambayo yanalipiwa Kwa dollar so nayo inaongeza Kasi ya dola kuisha ukiacha import bill kuzidi kuongezeka vs exports as well as dollar kuwa ghali kwenye soko pia.
[emoji2956]
 
Magufuli alikuwa ahead of time, he was a Genius in a pool of fools wakaona kupambana nae its the only way ya kuendelea ku survive. Wenye akili tu ndio huwa tunamuelewa Magufuli.
 
Tanzania hata mkifika million 300 kama style ya Uongozi na katiba itakuwa hii hii ya kuzalisha mafisadi na kuchekea wezi. Hakuna kitu kitabadilika
 
Kupitia tozo za miamala tungechangia vizuri tu miradi yote ikakamilika kwa wakati. Ingekuwa inaumiza ila kwa maendeleo ya kasi watu wangelalamika ila at last wangeelewa.
 
Kuna government expenditures ambazo lazima zitumie dollars hilo alikwekepeki.

Kwa hivyo uwezi kulaumu necessary government expenditures za nje kama kununua madawa, kulipa madeni, na necessary tangible assets zingine za serikali ambazo hazizalishwi nchini ili kutekeleza miradi yake. Wengine ni wafanyabiashara pia wakubwa na wadogo ambao wanaagiza inventories kutoka nje au machinery kwa shughuli zao.

Issue ni pale wafanyakazi wa serikali wanaposafiri ovyo kuongeza demand ya dollar, mafisadi na wauza nganda wanapo geuza hela zao kuwa dollars (ndio wawekezaji wa baadhi ya bureau de changes) na ndio maana zilipovamiwa nd kufanyiwa forensic auditing zingine hazikuwa na maelezo ya sources za reserves au investment zao. Uwezi kumuongopea auditor makini akikagua; Magufuli hakuwa mjinga hizo zilikuwa hela za majizi.

Sasa hao mafisadi ndio tatizo kwenye uchumi. Hayo matumizi ya serikalini na wafanyabiashara ayazuiliki ndio maana bank kuu inaweka dollar reserve kwa sababu hizo ku-stabilise uchumi.

Lakini kama kuna hela ambazo upatikani wake sio halali mtu kapiga 800 million ambayo ilitakiwa kuingia kwenye matumizi ya mzunguko wa uchumi wa ndani, halafu yeye kaitia mfukoni, awezi kuiweka bank, halafu anataka kutunza hizo hela kama dollars. It’s obvious demand ya dollars itakuwa kubwa, hii ndio dhana ya artificial economy.

Ufisadi una madhara mengi sana kwenye uchumi hasa kwenye kuchochea inflation za sector ambazo hizo hela zinaenda. Mara nyingi huwa kwenye kununua foreign reserves na ardhi au nyumba in prime areas.

Mother hana shida vile, ila kundi gani analoamua kusikiliza ndio linaonyesha uongozi wake.

Na mimi narudia tena, tatizo letu ni Jakaya Mrisho Kikwete
 
Nchi imefunguliwa wezi na wauza madawa.
 
Halafu nyie machawa huwa mnapenda kujificha sana kwenye kichaka cha swala la dunia
Nakukumbusha tu mkuu….Chuki hupofusha, chuki hufanya watu wakawa wachawi, na chuki inaua ….
Endelea kuamini Tanzania haiathiriwi na yanayoendelea huko duniani! Maana sisi tupo huku kwenye sayari ya Neptune.
 
Nchi imefunguliwa wezi na wauza madawa.
Inasikitisha sana majuzi nimemsikia Bashe; anamjengea bwawa Bakhresa kwa mabillioni ya serikali kwa madai ya kuongeza uzalishaji wa sukari.

Halafu Mtibwa sugar, Kilombero Sugar na Kagera sugars wapo kimya na hii disadvantage ya kibiashara anayopata mwenzao in unit costs.

Nakuhakikishia Bashe kwenye hiyo deal nusu ya costs za huo mradi Bakhresa anamlipa.

Sasa usimlaume Bakhresa hivyo kwa sababu anatimu ambayo inauwezo wa kutafuta investment advantages kwenye fair market; ila kama kuna opportunities za kujipa advantages kwanini aziache.

Na hata huyo Bashe simlaumu hivyo kwa huo ufisadi anaoufanya ni zama zake za kupiga why not him kama kila mtu anafanya.

This is why I hate Jakaya Mrisho Kikwete yeye ndio source ya haya yote kujifanya anajua njia sahihi ya kuongoza Hii nchi; yaani huyo mzee nimetokea kumchukia sana kwa jinsi anavyo haribu uraisi wa Samia na Hii nchi yeye na genge lake.

Yaani tutumie hela za walipa kodi kumjengea Bakhresa bwawa, na hao wengine nani aliwajengea huko ni kumpa mfanyabiashara mmoja advantage kwa wenzake in unit costs. Halafu kuna mijitu itamsfia huyo Bashe, hana uzalendo wala huruma ata chembe ameonyesha.
 
Sa katika biashara, nyie msio na business yoyote ndio mnaamka sasa.
Hali hii imekuwapo karibia miezi sita.
 

Kwani tumeacha lini kuwadhamini majirani ili waweze japo kupumua?
 
BOT siku zote huwa na akiba ya $4billion kama Kuna uhaba sasa hivi aulizwe Gavana mpya
 
Nashauri Hatua na fursa za kuongeza reserve ya fedha za kigeni ni pamoja na:
1.Tumeambiwa tuanze kununua dhahabu kama nchi na kuweka akiba hatusikii,hiyo ndiyo shida. Nchi nyingi kwa sasa zinaweka akiba ya dhahabu na madini adimu, prof Muhongo nakubaliana naye.
2.pili safari za nje kwa wafanyakazi kutumia dola zipunguzwe,
3. katika nchi za sadc na EAC tuanze kufanya biashara kwa" local currency" zetu, kupunguza kwenye utegemezi wa dola km BRICS
4.Sekta ya utalii haijapewa nafuu ya kikodi inayostahili,kuondolewa tozo na kupewa mikopo yenye masharti nafuu ili kuchangia kuingiza fedha za kigeni,
5.Baadhi ya miradi km kununua ndege kwa fedha taslimu lingeangaliwa tena.
6. Serikali ipunguze maduka ya fedha za kigeni yasiyo na credibility na yaruhusiwe kwenye maeneo maalum km ilivyokuwa awamu ya tano.
7.Riba kwenye mikopo ya mabenki ipungue zaidi hadi digit 1 ili mikopo ichochee uchumi wa ndani na "exports" na kupata fedha za kigeni lakini hapo hapo turudi kwenye "import substitution strategy"kwa muda mrefu tuimarishe sekta ya kilimo na mifugo,viwanda vidogo.
8.Miradi mingi mikubwa izingatie sana "local content" ili fedha ya mikopo kwenye miradi ibakie hapa nchini.
9.Tuuze nguvu kazi na utaalam nje mf.nchi za kiarabu huwa zina uhitaji sana nk walimu wa kiswahili wanahitajika sana duniani.
10.Tuimarishe mfumo wa kuingiza fedha za "diaspora" na ikibidi tulegeze masharti ya uraia nchi mbili ili kuwavutia.
11. Tufungue masharti ya kibenki ya kuingiza fedha za kigeni nchini na kubana utoaji wake nje hususani kwa"online/digital payments".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…