Kumbe kuoa ni kugumu hivi? Aisee mniombee niko hoi bin taabani

Tatizo Nini mkuu chakula au Kodi ?

Mimi nakushauri Kama tatizo ni PESA ya chakula useme au Kama tatizo ni mambo mengine useme ili tuone tunakusaidiaje Ila jifunze uvumilivu usimfukuze huyo Mwanamke endelea kujenga naye future huko Mbele Kuna mwanga.
 
Tatizo lilianzia ulipotamani michango ya sherehe ya harusi badala ya kufikiria ikiwa umepevuka au la kumdu masuala ya ndoa.
Usijali,kumbuka videos za ukumbini na namna ulivyokuwa unawachukia waliogoma kukuchangia.
 
Kataa ndoa kijana alikulupuka sana
 
😂
 
Mkuu komaa tu. Kwa umri wako mimi ni mdogo wako ila nimekomaa mpaka sasa naenda mwezi wangu wa nne. Hakuna mwanzo rahisi, na miezi 6 ya mwanzo ndio migumu balaa ila kila miezi inapoenda utaanza kuona unafuu kwenye ndoa yako. Mungu akusimamie
 
Unajiona hutoshi tatizo bado huamini kama umeoa, Yani mentality ya usingle inakusumbua na kujiona Bado mdogo Kwa hayo majukumu yako mapya, wakati tayari wewe ni mtu mzima uliyekomaa kidevu kabisa...Wala usiwe na presha kubali tu nafsini mwako kuwa kule ushatoka Sasa hivi upo ukurasa mwingine wa maisha, jitayarishe kuwa baba na kichwa cha familia Mzee...kuwa makini kama umechoka mapema hivi wahuni watakusaidia kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…