View attachment 3587205
Tukio la huko Karibu na Ulaya,
Siyo wewe unayo ona ina muhimu, wao wanayo ona hutakuwa na swali lolote, jisomee, usiongee na mtu alafu muombe mungu akufunulie, utajutia miaka uliyopoteza huko "misri".
1. Kuabudu Sanamu na Kuchonga Sanamu .
Maandiko haya yanakataza kutengeneza au kusujudia sanamu:
- Kutoka 20:4-5 - "Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni... usivisujudie wala kuvitumikia..."
- Kumbukumbu la Torati 5:8-9 - Katazo sawa na hilo la kuchonga na kusujudia sanamu.
- Walawi 26:1 - "Msijifanyie sanamu, wala sanamu ya kuchonga, wala msiwavishe nguzo, wala msiweke jiwe la picha...".
- Zaburi 115:4-8 - Inazungumzia sanamu za fedha na dhahabu zinazotengenezwa na mikono ya wanadamu, zenye macho lakini hazioni.
- Isaya 44:9-20 - Nabii Isaya anadhihaki upumbavu wa kutengeneza sanamu na kuziabudu.
- 1 Yohana 5:21 - "Watoto wadogo, jilindeni na sanamu".
- Wakolosai 3:5 - "Basi, yaueni viungo vyenu vilivyo katika nchi... na tamaa mbaya... ambayo ni ibada ya sanamu".
2. Kutambika na Uganga (Ibada za Kipepo/Kimila)
Maandiko yanayokataza kutafuta msaada wa mizimu au matambiko:
- 1 Wakorintho 10:20-21 - "Mambo hayo wanayotoa dhabihu, wanaitolea pepo, wala si Mungu... Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo...".
- Kumbukumbu la Torati 18:10-12 - "Asionekane kwenu mtu... atoaye mwanawe... au atuaye bahati, wala mchawi... Kwa kuwa kila atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA".
- 1 Wakorintho 10:14 - "Kwa hiyo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu".
3. Kunywa Pombe na Ulevi
Biblia inaruhusu kinywaji kwa kiasi lakini inaonya vikali ulevi:
- Mithali 20:1 - "Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima".
- Waefeso 5:18 - "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho".
- Isaya 5:11 - "Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane...".
- Mithali 23:20-21 - "Usiwe miongoni mwa wanyakuzi wa mvinyo; miongoni mwao wanaokula nyama kwa ulafi".
- 1 Wakorintho 6:10 - "...wala walevi... hawaurithi ufalme wa Mungu
Haya maandiko hutakaa usomewe, wala kujadiliana, na ukitaka ulaaniwe jaribu kuulizia.
Kama una PhD ya theology au Professor, njoo na maandiko yanayopinga hayo maandiko niliyoyanukuu hapo juu. Stoery sijui hujui tafsiri hapana, njoo na maandiko tu.