Hili swala imekaaje nakumbuka majuzi kuna mtu nimeamka nimekaa nikamfikiria sana nikawa nataka kutumia meseji ghafla text yake ikaingia nikajiuliza alikuwa anawaza kama mimi kumbe hiki ni niniWaliokimbia shule mambo ya physics yakijirudia lazima watoke nduki.
Anyway Wacha namimi niongeze vijipoint.
Iko hivi, mtu kaumbwa akiwa na nishati(Roho) ambayo iliingia ndani ya mwili ulipokuwa tumboni mwa mama yako na kuunda kiumbe mpya (Nafsi) ambaye ndie wewe mtu kamili.
Sasa wewe mtu kamili kwa kuwa umeumbwa kwa nishati iliyopo ndani yako, hivyo kama mjuavyo nishati inatabia ya kuatract na ku-disatract positive&negative charge inategemea na wewe kwa wakati huo upo ktk masafa ya energy za aina ipi.
Kila mtu ana energy ambayo huwezi kuiona kwa macho ya kawaida, lkn ipo,
Mfano ukiwa ktk energy ya positive charge kwenye matembezi yako na ukakutana na mtu mwenye positive charge the same to yours, hapa nadhani hata pyhsics haiapply Ile law of magnetism inayo state as alike charge repel, different/unlike charge attract, kwa upande huu ni tofauti, yaani utavuta nishati unayofanana nayo hapa ukikutana na mtu mwenye Charge inayofanana na yako lazima mtaendana kwa mood zenu, reaction zenu na response zenu ktk maongezi, body signs.
Ndiomana hata wale motivation speaker huwafundisha zile kanuni za law of attraction ama nguvu ya USUMAKU za kuvuta vitu unavyovipendelea kwa kuwekeza nguvu zako na akili zako ktk mawimbi sawa na vile vitu uvitakavyo.
Iko hivyo Kila kiumbe kina energy ya USUMAKU na pia umeme kiujumla, na Kila kiumbe kinaweza kudaka mawimbi sawa na kiumbe kingine, ndiomana Kuna muda hutokea, unammiss mtu Fulani ukitaka kumtafuta kwa simu ghafla anakutafuta na kukupa habari kama yako kuwa alikukumbuka, hiyo inaonesha wote mlikuwa ktk state ya mawimbi sawa, yaani akili zenu zilikuwa ktk frequency Moja kwenye mawimbi.
Na ifahamike kuwa kwa Kila kitu ufanyacho ujue kinabeba mawimbi yako na kinahusisha energy yako, iwe tendo jema&baya, ama iwe maongezi mema au mabaya ujuwe yanakuwa ktk mawimbi energy yako ivyo ni rahisi kwa viumbe wengine kukufikia kupitia mawimbi ya energy yako uliyonayo kwa wakati huo iwe matendo/maneno/mood yako na matamanio yako.
Kiumbe yeyote asiye na mwili(Roho) anauwezo wa kuisoma energy yako ndiyo itaamua kama anauwezo wa kukumudu ama vipi.
Ndiomaana huwa tunapinga sana hizi stories za kusadikika hasa kutoka kwa walokole na wafia dini wanaosema Kila jambo baya limetendwa kwa ushirikina/uchawi/shetan, hii si kweli, msababishi mkuu wa maovu dunian ni binadamu mwenyewe kwa kufungua Izo Channel za kusafirisha bad energies ktk maisha ya uhalisia.
Mchawi hawezi kukudhuru bila kupata sababu kwako, hawezi kukuloga bila kupata upenyo/mlango wa matendo yako.
Pepo hawezi kukuvamia bila sababu, na hii iwaendee wale walokole wanaodai watu huanguka makanisani sababu ya mapepo, acheni utani jmn hivyo viumbe havifanyi kazi kwa namna mnayoidhania, na pengine watu wenye mapepo ni wale tunaowaamini watusaidie kiroho, hao ndio ambao hupagawa na mapepo, kwa sababu maalumu ya kupotosha jamii.
Hao wanaodondoka makanisani na wengine kuleta stories za ajabu ajabu hao wote ni wagonjwa wa akili yaani waliologwa akili ama kiufupi waliopagawa na nguvu za Pepo ambao wameletwa na hao viongozi wenu wa kidini kwa kujua ama kutokujua.
Pepo hawezi kukuingia bila sababu za msingi, mchawi hawezi kukuloga bila sababu ya msingi, inaweza kuwa sababu ya kipumbavu kiuhalisia lkn kwake ni sababu ya msingi.
Yaani mshirikina/Pepo ili akuvamie lazima muwe ktk hali Moja ya charge, yaani kama hukuwa na doa lolote la kuatract energy ya Pepo ama kufungua channel ya energy ktk mwili wako huwezi kulogwa hata mchawi wa aina gani hawezi kukufanya lolote, isipokuwa kunafanyika jambo la kukufanya uendane na frequency zao ama ufanye jambo lolote la kufungua mlango wa energy ktk utu wako ndipo unapovamiwa, either kupitia watu wengine ambao wanaweza kukuletea ugomvi, hasira, ama matamanio yako hasa tamaa mbaya.
Niishie hapa, kiufupi hii elimu ni kubwa sana lkn ndio hivyo watu wengi hawana sababu viongozi wao wa kidini wamebase kwenye mafundisho mepesi yasiyohitaji akili, yaani mmebaki kufundishwa Kila siku mambo Yale Yale na stories zile zile kumbe Kuna mambo mengi ya msingi ambayo watu ilitakiwa wayajue.
Na mara nyingi nikikutana na mtu roho huwa inasem kwa ndani Huyu hamtawezana