DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Si Kwamgu tu Kote Malaika Ni Mjumbe!...Kwako malaika ni nani?
Kuna Tatizo hapo?
Maana tafsiri ya Malaika ni Mjumbe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si Kwamgu tu Kote Malaika Ni Mjumbe!...Kwako malaika ni nani?
Okay ulipimaje hizi frequencyKnowledge is power..kumbe MAJINI, WACHAWI, NA BLACK MAGIC ZOTE, zinafanyika at low vibrational frequency ndio maana ili mtu alogeke lazima washushe frequency yake awe kwenye range zao.
Kwa mfano mtu akiwa ana hofu au hasira ni rahis kumloga coz ana resonate at 7Hz very low frequency.
PEPO MCHAFU anamuingia mtu akiwa at low frequency. Siri iliyopo hapa ni kucheza frequency game isishuke, msibani watu wanalogwa sana coz wana huzuni na frequency zao zinakuwa down, bila shaka umewahi kusikia msiba mmoja umesababisha msiba mwingine then wanasingizia presha..
Embu tupe somo kidogo jinsi ya kufanya hizo hatua (ku-chant)Kama ni mkristo kuna namna ya ku-chant mantra zinazoihusu DAMU YA YESU na baadhi ya ARCHANGELS ni njia rahisi za kukuweka frequency za juu ukifanya kwa usahihi....
Si kweliWiseman.
Malaika si wajumbe, ila miongoni mwa majukumu yao ni kuwa mjumbe.Si Kwamgu tu Kote Malaika Ni Mjumbe!...
Kuna Tatizo hapo?
Maana tafsiri ya Malaika ni Mjumbe
Mkuu Kasoma Tena..Malaika si wajumbe, ila miongoni mwa majukumu yao ni kuwa mjumbe.
Ukitaka kulijua hili kwa kina fahamu majukumu yao!
Lugha kongwe hapa duniani ni mbili!Neno Malaika limetokana na Neno la Kiyunani (Greek) ἄγγελος (angelos).
Au kwa Kingereza angel linalomaanisha Mjumbe au Mpeleka Taarifa..
au Pia neno מַלְאָךְ (mal'akh) la Kiebrani linalomaanisha Mjumbe au Mpeleka Taafifa kwahyi malakh, angelos..yote sawa..
Kwa kiarabu Malaika haina maana ya mjumbe! Mjumbe ni rasuul, na ujumbe unaitwa risala.Na kwa Kiarabu مَلَك (malak, au Wingi wake ملائكة malā'ikah)
Ambayp ndo unayotamka wewe Malaikah ni neno la Kiarabu la Malaika lenye maana Sawa na hayo hapo Juu kuwa NI Mjumbe au Mpeleka Taarifa..
Unafahamu kuwa kila binadamu ana malaika maalumu ambaye utumishi wake ni kukulinda wewe? Na kila huyo malaika mlinzi ana jina lake? Mlinzi wako jina lake tofauti na jina la mlinzi wangu na kwa kila mtu yupo hivyo!Angelology na Demonology sio Elimu ambayo wanaijua Wengi zaidi ya wale waliosoma Theology au wachungaji wengi..
Kuna Vitu vingi viko Concealed kwa Muumini wa Kawaida..
Sina Shaka na Wewe kabisa na umeongea Vizuri sana Na Nimependa Ila Kuna kitu Kimoja Unaniangusha sheikh wangu..Lugha kongwe hapa duniani ni mbili!
Kiarabu na lugha ya wayahudi Hebrew.
Hizi lugha kiasili ndizo lugha zinahusika na masula ya kidini na ya kiimani, na ndizo lugha zilizotambulisha kuwa mbali na sisi binadamu ila kuna viumbe vyengine vilivyoumbwa na Mungu vinavyoitwa Malaika.
Malaika si wajumbe, ila moja ya utumishi wao ni kuwa wajumbe. Malaika ni viumbe wa Mungu, kazi yao ni utumishi, na miongoni mwa huo utumishi ni kuwa mjumbe.
Kwa mfano Malaika Jibril utumishi wake ni mjumbe. Anapokea taarifa kutoka kwa Mungu na kupeleka kwa mitume ya Mungu. Huyu Malaika miongoni mwa kazi yake ni kupeleka ujumbe au ufunuo au wahyi! Hivyo yeye ni mjumbe.
Hamalat Al Arsh; hawa ni malaika ambao utumishi wao ni wanaobeba the throne of God.
Malakul Maut au kwa jina maarufu Israel huyu si mjumbe, huyu kazi yake au utumishi wake ni kuchukua roho! Haji kukuletea taarifa bali anakuja kukutoa uhai.
Malaika anayeitwa Ishmael utumishi wake ni ulinzi wa mbingu ya kwanza. Utumishi wake si kupeleka taarifa, utumishi wake ni ulinzi wa Mbingu ya kwanza. Kutwa nzima kazi yake ni kuungalia kwa chini ulimwengu wetu huu wenye sayari na magimba.
Kwa msingi huo malaika ni nani? Malaika ni watumishi wa Mungu wenye majukumu yao maalumu ambayo Mungu mwenyewe kawapangia.
Na ndiyo maana ukija kwenye dini ya kiislamu, idadi ya mbawa za malaika zimetofautiana kulingana na majukumu.
Kwa kiarabu Malaika haina maana ya mjumbe! Mjumbe ni rasuul, na ujumbe unaitwa risala.
Kwenye Qur'an inaweta tamka "na tukamtuma mjumbe wetu" haimaanishi kuwa maana ya Malaika ni mjumbe bali kwa kazi aliyopatiwa ya kupeleka taarifa au ujumbe hivyo akaitwa Mjumbe.
Malaika Jibril anaitwa mjumbe kwa sababu kazi yake ni kupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa Mungu na kuyapeleka kwa Malaika wenzake au binadamu.
Ila Malaika Israfil si mjumbe, kwa sababu hup si utumishi aliyopewa. Utumishi aliyopewa na Mungu ni kupuliza baragumu.
Unafahamu kuwa kila binadamu ana malaika maalumu ambaye utumishi wake ni kukulinda wewe? Na kila huyo malaika mlinzi ana jina lake? Mlinzi wako jina lake tofauti na jina la mlinzi wangu na kwa kila mtu yupo hivyo!
DR Mambo Jambo unafahamu Malaika wako wa ulinzi anaitwa nani? Sisi tunayo elimu ya kukuambia jina la Malika wako mlinzi ni nani! Na kama amekaa pembeni kulingana na matendo yako tunajua namna gani ya kumuita na akupatie ulinzi.
Unawafahamu Hamatan? Lamatan n.k?
Hawa ni majini kutoka kwenye koo za kisultani. Wana nguvu kubwa na wana majeshi na wanaogopeka kwenye ulimwengu wa kimajini.
Kuna koo za kijini ambazo zimedhamiria kumuasi Mungu na kuleta athari kwa binadamu, ambao hawa majini nao wana nguvu kubwa wewe binadamu wa kawaida huwezi kupambana nao!
Sometimes kama umezingwa na majini wachafu unaweza ukawaita hao wakaja kukusaidia bila makubaliano ya namna yoyote wakaja na jeshi lake kukupigania.
Hawahitaji malipo yoyote! Ila kuna namna unawaita. Hawa ndiyo wanaitwa Makhudamu.
Bado unamashaka na mimi?
Hujui vitu kaa kimyaMlijifunza nini?
Ni wapi ulishawahi kumuona mchawi anapaa kwny ungo?
Wazungu nao zamani walikuwa wanaamini ushirikina kama wewe, lakini walikuja kuelimika na hadi leo huwezi kukuta mganga wa kienyeji Ulaya.
Niambie best, ni wapi umekutana na popobawa, au jini Maimuna?
Wewe unajua vitu?Hujui vitu kaa kimya
Unataka attention?Wewe unajua vitu?
Tueleze.
Au unachojua ni kutunyamazisha tu tukae kimya?
Attention?Unataka attention?
Hawa si malaika wa ulinzi wa mwili usipaywe na madhara. Hawa ni malaika wa ku record matendo yako yote ya kimaisha mpaka utakapokufa na ndiyo maana wanaitwa Kiraaman Kaatibiin, yaani "waandishi wenye heshima".Umezungumzia Kuhusu Malaika walinzi ..
Ukisoma Kwenye Surah Al-Infitar 82:10-12 ..
kuna malaika M/Mungu anawaita (كِرَامًۭا كَٰتِبِينَ) Kiraman katibiina
Taarifa zako hazipelekwi kwa Mungu, bali kuna mahali zinahifadhiwa mbinguni, ni kama ofisini tu file lako linavyopelekwa masijala na ndicho hawa Malaika wanachofanya. Siku ya Qiyama file lako linanyofolewa na kusomewa mwenendo wako.Sasa Unajua Kazi yake Huyu ni Mjumbe ambaye anachukua Taarifa kutoka kwako na Kuzipeleka Kwa M/Mungu na Hiyo ndiyo kazi yake kwanini ameitwa Ujumbe..
{ ٱلَّذِينَ يَحۡمِلُونَ ٱلۡعَرۡشَ وَمَنۡ حَوۡلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْۖ رَبَّنَا وَسِعۡتَ كُلَّ شَيۡءٖ رَّحۡمَةٗ وَعِلۡمٗا فَٱغۡفِرۡ لِلَّذِينَ تَابُواْ وَٱتَّبَعُواْ سَبِيلَكَ وَقِهِمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ }Malaika wanaobeba arshi ya Mungu yaani Hamalat Al arsh Umesema Sio wajumbe?..
Hauko Serious Sheikh wangu Soma Surah Ghafir 40:7
UKisoma mpaka Aya ya 7 utaona Dua ya Malaika hawa kama sijasahau huwa ni mapaka aya ya 10 au 11..
Dr, ikiwa kama mahala popote au umepata vyanzo vyovyote katika uislamu vinavyosema malaika wanaobeba arshi(hamalatal arshi) kuwa wanashuka duniani kuja kuchukua ujumbe kutoka kwa sisi binadamu na kuuepeleka kwa Mungu, naku challenge leta hapa hayo maandiko!Malaika Hawa wanachukua Ujumbe kutoka kwa Sisi wanadamu Tulio wema na Kumfikishia Mungu kwa Kutuombea Dua na toba kwake na kumkumbusha mazuri tunayofanya sisi waja wake..
Soma hapo jina lake utaona limeandikwaje. Hiki ni kitabu kinaitwa Dalaailul Khayraat.Turudi kwa Malakutul Mawti..
Anaitwa Azrael na Sio Israel..
Dr wewe unatumia fikra zaidi kuliko elimu kwenye haya masuala. Ni makosa ukifanya hivyo!Maana Nimeshtuka Kidogo ulivyosema Israfil sio Mjumbe..
unafikiri Kazi ya Kupuliza Baragumu aliyopewa Siku ya Kiama ni Ya nini? Kujifurahisha?
Lengo ni kupeleka Ujumbe kwa Viumbe vyote kuwa Al haqqah, Yawmul Qiyama, Yawmul Hisab, Yawmul tanad, kwetu sisi watenda mema Ni Yawm al-Fawz au Yawm al-Din..
Mkuu unatumia hisia sana badala ya kutumia vyanzo vya elimu.Turudi kwa Malakutul Mawti..
Anaitwa Azrael na Sio Israel..
Unahisi Hiyo kazi ya Kutoa roho Ilifika Siku akaamua Tu kwamba Kuanzia Sasa ntaanza kutoa roho?
hakuna anayemtuma Kufanya Hivyo?
Kiwango Cha Uelewa Wako Na Maarifa Yako Yakiwa Chini Ndio Utataka Mijadala Kwenye Mambo Madogo Kama Haya.Attention?
Kwa muktadha upi?
Jamaa nimemuuliza maswali ananiambia nikae kimya.
Watu kama hao, au labda na wewe ndio mnaharibu mtandao wa Jamiiforums. JF ni sehemu ya mijadala, hoja kwa hoja. Hujui kitu unauliza, na wewe unaejua unaeleza unachojua.
Siyo sehemu ya kuambizana kukaa kimya.
Kumbe ni wewe mwenyewe ulieniambia nikae kimya.
I can bet you are very stupid.
Shame on me?! You cant be serious.Kiwango Cha Uelewa Wako Na Maarifa Yako Yakiwa Chini Ndio Utataka Mijadala Kwenye Mambo Madogo Kama Haya.
Na Mbaya Zaidi Kadri Unavyotengeneza Maswali Ili Uonekane Una Hoja Ndio Zaidi Unavyoonesha We Ni Mweupe Kiasi Gani.
Shame on you!!!
Ushauri😀ig Deep Kwenye Dini/Imani Yako Maana Ukiielewa Dini Hata Vitu Vya Kijinga Unavyouliza Hutouliza Tena.
Maswali dawa yake kuyajibu au kukubali huna jibu.Shame on me?! You cant be serious.
It must be shame on the person, who is mweupe and then haulizi.
And most importantly, shame on the person like you anaedhani anajua sana halafu hataki kuelimisha wenzie ambao ni 'weupe'
Mbona kuna watu wanajua sana humu kama akina DR Mambo Jambo na Kiranga tukiuliza kitu wanatuelekeza?
Inawezekana na wewe hujui tu unashindwa kujibu maswali unakimbilia kuyaita ya kijinga.
Kuna Kitu Kimoja ambacho nimekigundua Kwenye Uandishi wako wote na Sio Kibaya Kinaitaji Kuelekezwa kidogo tu..Hawa si malaika wa ulinzi wa mwili usipaywe na madhara. Hawa ni malaika wa ku record matendo yako yote ya kimaisha mpaka utakapokufa na ndiyo maana wanaitwa Kiraaman Kaatibiin, yaani "waandishi wenye heshima".
Mlinzi hawezi kuwa mwandishi. Mlinzi ni mlinzi na mwandishi ni mwandishi. Kwenye Qur'an hiyo aya imemuita mlinzi kwa maana mlinzi anayedhibiti matendo yako yote kwani anayanakili na kuyahifadhi.
Na hii siyo rai! Bali ndivyo ilivyo! Qur'an ina nyenzo zake za kutafsiri Qur'an ambazo ni 3.
1)Qur'an kwa Qur'an
2)Qur'an kwa sunna (hadithi) na
3)Qur'an bi Swahaba
Mbali na hapo ukitafsiri utakuwa umetumia rai, na rai Mtume amekataza na makazi yake ni mabaya.
Wewe hiyo aya hapo haujaitafsiri bali umetumia tarjum. Tarjum ni kuihamisha Qur'an kutoka kwenye lugha yake ya asili yaani kiarabu kwenda kwenye lugha ya kiajemi, yaani lugha isiyo ya kiarabu. Mfano lugha ya kiswahili, kichina, kimongolia n.k
Ila ufafanuzi wa hiyo aya haswaa ina maanisha nini? Kinachomaanishwa ndicho utakipata kwenye nyenzo 3 tajwa hapo juu za kutafsiri Qur'an.
Na kilichomaanishwa ndicho nilichokufafanulia. Kiraaman Kaatibiin ni malaika walinzi wa kunakili na kuhifadhi kumbukumbu za matendo yako. Na ndiyo maana wakaitwa waandishi wenye heshima. Si malaika wa walinzi wako wa mwili usikumbwe na madhara!
Taarifa zako hazipelekwi kwa Mungu, bali kuna mahali zinahifadhiwa mbinguni, ni kama ofisini tu file lako linavyopelekwa masijala na ndicho hawa Malaika wanachofanya. Siku ya Qiyama file lako linanyofolewa na kusomewa mwenendo wako.
Na kwa siku wanakujia wawili kwani wana shift.
Sasa hawa si wajumbe mkuu! Yaani unalazimisha jambo ambalo halipo kwenye uasili wake.
Malaika Mikaeel, huyu anasimamia mwenendo wa dunia kama mvua, upepo, n.k na anafanya hivyo kwa amri ya Mungu. Sasa ukisema Malaika ni mjumbe huyu anapeleka ujumbe gani kwa Mungu hali ya kuwa hayo mabadiliko ya hali ya hewa na kuiendesha dunia anayafanya kwa kupata maelekezo kutoka kwa Mungu?
Malaika Maliki ni msimamizi wa motoni (jehannam). Huyu naye anapeleka ujumbe gani ndugu yangu? Kwamba moto umefifia? Hapana! Huyu anafanya kile anachoambiwa na Mungu naye anatekeleza. Hilo ndiyo jukumu lake.
Kama wafanyakazi waliyo chini ya serikali wanaitwa watumishi wa umma kwa kadri ya majukumu yao waliyopangiwa na ndivyo kwa Malaika, ni watumishi wa Mungu, wao wanafanya kazi kwa majukumu waliyopangiwa, na miongoni mwa majukumu kuna wajumbe ni kama ofisi zetu zilivyo na messenger!
{ ٱلَّذِينَ يَحۡمِلُونَ ٱلۡعَرۡشَ وَمَنۡ حَوۡلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْۖ رَبَّنَا وَسِعۡتَ كُلَّ شَيۡءٖ رَّحۡمَةٗ وَعِلۡمٗا فَٱغۡفِرۡ لِلَّذِينَ تَابُواْ وَٱتَّبَعُواْ سَبِيلَكَ وَقِهِمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ }
[Surah Ghāfir: 7]
Tarjumu yake ni hii:
Wale wanao beba A'rshi, na wanao izunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.
{ رَبَّنَا وَأَدۡخِلۡهُمۡ جَنَّٰتِ عَدۡنٍ ٱلَّتِي وَعَدتَّهُمۡ وَمَن صَلَحَ مِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَأَزۡوَٰجِهِمۡ وَذُرِّيَّٰتِهِمۡۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ }
[Surah Ghāfir: 8]
Mola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizo waahidi. Na uwape haya pia wale walio fanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
{ وَقِهِمُ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ وَمَن تَقِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ يَوۡمَئِذٖ فَقَدۡ رَحِمۡتَهُۥۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ }
[Surah Ghāfir: 9]
Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa.
Maandiko haya matakatifu ni haya hapo juu! Katika hayo maandiko wapi unaona kuna onyesha hao malaika wanafanya ujumbe wowote? Mimi naona wanafanya maombi.
Dr, ikiwa kama mahala popote au umepata vyanzo vyovyote katika uislamu vinavyosema malaika wanaobeba arshi(hamalatal arshi) kuwa wanashuka duniani kuja kuchukua ujumbe kutoka kwa sisi binadamu na kuuepeleka kwa Mungu, naku challenge leta hapa hayo maandiko!
Ili niweke mazingira sawa katika hili kwa manufaa ya wasomaji wengine: Hata siku moja malaika hamalatal arshi hawajawahi kushuka duniani. Jukumu lao wao ni kubeba arshi. Na wapo 4 tu.
Nipatie ushahidi wapi wanashuka duniani na wapi ni wajumbe. Mkuu wa malaika Jibril A.S mwenyewe kuna siku alimuomba Mungu aende akawaone. Wewe unasema wanashuka duniani.
Soma hapo jina lake utaona limeandikwaje. Hiki ni kitabu kinaitwa Dalaailul Khayraat.
Picha yake ipo chini! Hajaandikwa kama ulivyoandika bali ameandikwa kama nilivyoandika.
Dr wewe unatumia fikra zaidi kuliko elimu kwenye haya masuala. Ni makosa ukifanya hivyo!
Malaika wakubwa 2 wanahusika na maisha kwa binadamu na malaika 2 wakubwa wanahusika na kifo kwa binadamu.
Malaika Israfil na Israel wanahusika na kifo. Malaika israfil anahusika na kuchukua roho za watu massively au collectively.
Mtume Muhammad s.a.w anasema kwenye safari yake ya Miiraji:
"Alimuona Malaika Israfil mguu wake mmoja ameupeleka mbele na mwengine nyuma, na ameshika baragumu na huku pumzi zake amezivutia kwa ndani akiashiria anataka kuziachia kwa kulipuliza huku akiwa ameiangalia arshi tukufu ya Mungu na chozi likimtoka, akisubiria amri ya Mungu alipulize.."
Akilipuliza hili hakuna ujumbe, isipokuwa ni kifo kinakukutia hapo hapo! Anachopuliza kinaleta destruction ya ulimwengu mzima na mauti hapo hapo kwa muda huo huo! Yaani kinaharibu order ya ulimwengu mzima.
Tena vinakufa vya mbinguni na vya ardhini. Isipokuwa wale Mungu mwenyewe atataka wabaki. Na watabaki kwa muda ila nao watakufa.
Hayo maeno uliyaandika hayapo! Hayo maneno ni ya kupeana ufahamu kwenye darsa kuwa Qiyama kinahusika na nini? Katika uelewa wa kuielewa dini na Qiyama ndiyo mmojwapo anaweza akatoa ufafanuzi wewe ambaye umeutoa.
Hivyo Malaika Israfil siyo mjumbe! Yeye anahusika na kutoa roho massively au collectively, ndiyo kazi aliyopewa na Mungu. Awe mjumbe ili iweje?
Ujumbe aliufanya maishani mwake mara 1 tu tena kipindi cha Mtume Muhammad s.a.w...Alipokea ujumbe kutoka kwa mhusika (Mungu) na kuupeleka kwa mhusika (Mtume)kisha akrudi akaenda kwenye jukumu lake alilopatiwa la kushika baragumu.
Mkuu unatumia hisia sana badala ya kutumia vyanzo vya elimu.
Kwa mafundisho ya kiislamu idadi yako ya pumzi, quantity yako ya chakula, kiasi chako cha maji kimeshawekwa na Mungu na kuna malaika maalumu wanaohusika na hayo majukumu.
Ikiwa kama kiasi chako cha maji ulichopangiwa kwa matumizi ya uhai wako kimekwisha, anakuja malaika maalumu aliyepatiwa hilo jukumu na Mungu ambaye utamuona wewe tu na kukuambia "Ewe mwana wa adamu, nimezunguka mashariki na magharibi ya dunia lakini sijaona hata tone lako la maji lilibakia kwa matumizi yako!
Anakuja wa chakula naye anatamka hayo hayo! Anakuja wa pumzi naye anatamka hayo hayo! Wa pumzi akimaliza kutamka tu anakuja Malakul maut! Malaika wa kifo yaani Israel. Yeye anakuja kwa kazi moja tu la kukutoa roho! Hana stori yule!
Sasa hapo ujumbe ameufanya wapi? Bali yeye amefanya alichoamrishwa! Yupo bosi wake! Hivyo yeye ni mtumishi wa bosi wake. Ujumbe ni kupokea taarifa kutoka kwa mhusika na kuipeleka kwa mhusika kwa lengo la kupatiwa taarifa.
Wewe hayo maneno mengine unayatolea wapi Dr? Usitumie fikra zako rai zako kwenye dini! Mtume anasema:
"Yeyote atakayesema maneno ya Mungu kwa kutumia rai yake, mapema motoni makazi yake ajiandalie".
Kwa sababu utakuwa unafanya mzaha! Yaani maneno ya Mungu umeyachukulia mzaha mzaha! Maneno ya Mtume umeyachukulia mzaha mzaha! Ili usiyachukulie mzaha mzaha rudi kwa wanawachuoni. Kwa sababu wao ndiyo warithi wa Mitume.
Qiyama kitafanyika hapa hapa duniani! Jehannam itasogezwa karibu na hapa duniani, Mtume anasema:
"Jehannam itasogezwa karibu na dunia na Malaika kwa amri ya Mungu. Jehannam itakuwa na kamba 70,000. Na kila kamba moja itavutwa na malaika 70,000."
Kwa msingi huo, Malaika si wajumbe, Malaika ni watumishi wa Mungu, wanatekeleza majukumu yao waliyopangiwa na Mungu yakiwemo ujumbe.