Nimefikia hatua ambapo chochote ninachoshika natetemeka hata nikishika kikombe cha chai natetemeka tu kisa safari na smart gin
Pole, hapa kuna vitu vingi vya kiafya:
Unapata intetional tremor/kutetemeka kusiko kwa kudhamiria na huwezi kuzuia.
Ni dalili ya matumizi makubwa ya pombe na utegemezi. Hivyo, unahitaji kufanya UAMZI MHIMU DHIDI YA MSTAKABALI WA AFYA YAKO, unahitaji mpangilio mzuri wa kupunguza kiasi cha pombe na kupata tiba ya kutokukuletea madhira dhidi ya upunguzaji/kama yatakuwepo na mwisho kuamua kuacha.
1: Pombe huwa inaleta madhara kwenye sehemu ya ubongo inayosimamia fine motor activities skills/kazi za mikono na mengineyo.
2: Kama utasitisha ghafla kunywa pombe/bila mpangilio pia hili hutokea.
Hapa hili huonyesha kiasi kikubwa vha utegemezi wako kwenye pombe.
3: Pombe kuleta madhara kwenye ini ambapo hili pia hutokea.
4: Hii pia huweza kuwa dalili ya kushuka kwa sukari kama mhusika anakunywa pombe bila kula vyema.
Chagua fungu jema kusuka au kunyoa, hii ni baada ya kutafakari vyema wewe na nafsi yako pamoja na Muumba.