Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Umeambiwa report za World Bank na CAG. Tulipewa fedha $21M kwaajili ya mifumo na DP World ndio wametajwa watekelezaji! Jamani hapa hatufanyi siasa! This is very serious National matters. Binafsi sijasoma hizo report lakini kwa credibility ya Maria hawezi kusema jambo linalogusa taasisi nyeti bila ushahidi.

Inaogopesha sana!
Anajiropokea tu, bandari ilishatoa maelezo nini kimefanyika tayari kwenye uwekezaji.
 
Huyo hapo Mrisho Mrisho akielezea kilichofanyika tayari bandarini mwezi Juni tu.

Sasa huyo Maria asijifanye anatoa siri kwa kitu kilichowazi na kimeelezewa na bandari yenyewe.

Hujaelewa, why? Yeye concern yake ni kuwa DP World anakuja kuwekeza nini? anatumia pesa yoyote kuwekeza? Nenda tweer kamsome vizuri.......
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Huo ndo ukweli na tatizo ni lipi waseme bayana siyo kuwa too general na kupotosha umma. Kama mtu hana capacity ya kuchambua hili bora kukaa kimya.

Tulishashindwa miaka kibao mpaka KAGAME alitucheka tukamjibu kwa kuwatimua Raia wa nchi yake.
 
Sijui kwa nini watu hawaoni umhimu na ufanis wa DPW na hawasemi tatizo ni nini wako too general.

Yani kuna mtu huku kitaa nilimuuliza tupe faida na hasara ya DP world kuwekeza bandarini hakunijibu
 
Let us agree to disagree, usinilazimishe niamini unacho amini, hoja yangu ni kwa DP world itaongeza ufanisi na mapato serikalini yataongezeka.......sisi wabongo tumeshindwa kuendesha bandari kwa mda mrefu
Nimekwambia uelewa wako umekomea hapo... sasa DP world anakuja kuwekeza nini? Unajua maana ya kuwekeza?
 
Kwani mkataba wa Dp world na Tpa tayari? Mbona mnaendekeza Cheap Politics hivi?

Dp world vifaa vyao sio vya kitoto eti waje watumie Existing infrastructure, Hizo Crane na miundombinu mingine capability yake wanayo wao tu ama ni kampuni chache zenye uwezo huo.

Kusema kwamba Dp world wanatutegemea sisi eti mkopo wetu wa World Bank uwawezeshe wao ni chai ya mchana.

..Dp hatengenezi au haundi hizo Cranes.

..kuna mahali Dp ananunua Cranes, na sisi tunaweza kwenda huko kununua.

..kilichotokea ni UJINGA wa serikali ya Ccm kutokuipa bandari ya Dsm Cranes za kutosha.

..DP wanaweza kuwa MANAGEMENT COMPANY ambapo serikali itakuwa inawalipa fee.

..Mkataba unaowafanya Dp wamiliki, na Watanzania watazamaji, haufai.
 
Hii ni kutoka report ya Worl Bank .................................BY MARIA SARUNGI

Muhimu kuhusu DPW na mradi wa Benki ya Dunia

Pesa za mkopo wa @WorldBankAfrica zimetumika (na kukamilika)
👉🏽 kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani
👉🏽kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11
👉🏽kuboresha na kuunganisha na reli
👉🏽 Kupanua na kuimarisha Gati 8-11
👉🏽Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa

Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA
Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7
🙄
Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini??

Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao 😄 kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu!

YAANI KIUFUPI WANAKUJA KUTEKELEZA MRADI WA PESA ZA MKOPO WA WORLD BANK

Nyieeeeeeeeee!
Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
Ila #TutaelewanaTu
Wazanzibari wanataka kutupiga kitu kizito
 
Yani kuna mtu huku kitaa nilimuuliza tupe faida na hasara ya DP world kuwekeza bandarini hakunijibu
Inategemea ni mtu gani umemuuliza...... Wewe huoni tatizo kenye construction ya mkataba?
 
Kwani mkataba wa Dp world na Tpa tayari? Mbona mnaendekeza Cheap Politics hivi?

Dp world vifaa vyao sio vya kitoto eti waje watumie Existing infrastructure, Hizo Crane na miundombinu mingine capability yake wanayo wao tu ama ni kampuni chache zenye uwezo huo.

Kusema kwamba Dp world wanatutegemea sisi eti mkopo wetu wa World Bank uwawezeshe wao ni chai ya mchana.
Hujaelewa argument ya Maria. soma between lines
 
Hujaelewa, why? Yeye concern yake ni kuwa DP World anakuja kuwekeza nini? anatumia pesa yoyote kuwekeza? Nenda tweer kamsome vizuri.......
7EC2299B-280D-4D6C-ADC2-25D443302F59.jpeg

Kwa kuanzia tu bandarini kuna multi storage car park?

Kingine wanampago wa kuamisha Ro-Ro kutoka hapo ilipo.

Wana mpango wa kuboresha terminal ya abiria na majahazi.

Wana mpango wa kuongeza uwekezaji kurasini kuweka kupokea mizigo mingi inayokwenda nje ya nchi.

Wana mpango wa kuweka ICT system inayoweza track mzigo unapoingia melini kokote duniani mpaka unatoka ata wewe mteja unaweza jua mzigo wako ulipo.

Mambo yote yameelezwa hapo phase 1 wao watafanya nini.
 
Hayo yote ya nini jambo muhimu ni ufanisi ili serikali iongeze mapato kupitia bandari........na hilo Dp world ndo imekuja kutekeleza basi, hata kama mkataba ni wa miaka 100 as long serikali ina pata faida na inahudumia wananchi wake vizuri na kufanya maendelo hamna shida tuache fitina za kijinga.
Hayo mapato serikali wanaongeza kwa njia gani?
 
Jamanieee, hapa cha msingi kila mtu atafute kamba ndefu ili ale vizuri, tulishaambiwa tukapuuza, tuongezeni urefu wa kambaaaaaa, wenzetu kamba zao ndefu wanakula mpaka nyasi za upande wetu.
 
Nimekwambia uelewa wako umekomea hapo... sasa DP world anakuja kuwekeza nini? Unajua maana ya kuwekeza?
Sawa hiyo mitambo itakao letwa na technology itakua ya kwako? Kwa akili zako mkuu unaona hapo bandari imekamilika kiuwekezaji au you are just a novice man.......katika mkataba wao kuna oparationa investment and mantainance wewe kwa akili zako huoni kama kuna direct investment usiwe radical kwa kila jambo, ni level pia ya ujinga hiyo
 
Back
Top Bottom