Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA

Badala ya kutafuta makala ya bandari ya Dar na kumsikiliza mkurugenzi wa port.

Yote hayo keshayaongelea issue ni cranes za kisasa ambazo hazitoshi.

Pili wawekezaji wameelezea wanachoenda kuongezea wao hapo bandarini.

Wewe unatoka kwenda kumsikiliza kichaa mmoja Twitter ndio source yako; badala ya kuwasikiliza wahusika tena video wameonyesha ya kilichofanyika bandarini.
Yaani aache kuwasikiliza wenye akili, akawasikilize wala rushwa za DP?
 
Hivi hao wanaoendesha bandari wanapatikana kwa utaratibu gani?!

Sikubaliani na wewe kuwa Watanzania tumeshindwa kuendesha bandari. Labda ujisemee wewe mwenyewe lakini si ku- generalize.
Kuna kamati za bunge ndo zina utafiti neenda ukasome hasadi uone how bandari ya Dar inavo kua under utilised na mapato serikalini ni kidogo sana wizi ufisadi ndo umejikita sana pale......manaake tumeshindwa kuendesha hiyo bandari, kwanza niambie tulishawahi kufanikisha kuendesha nini?
 
Hii ni kutoka report ya Worl Bank .................................BY MARIA SARUNGI

Muhimu kuhusu DPW na mradi wa Benki ya Dunia

Pesa za mkopo wa @WorldBankAfrica zimetumika (na kukamilika)
[emoji1428] kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani
[emoji1428]kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11
[emoji1428]kuboresha na kuunganisha na reli
[emoji1428] Kupanua na kuimarisha Gati 8-11
[emoji1428]Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa

Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA
Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7
[emoji849]
Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini??

Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao [emoji1] kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu!

YAANI KIUFUPI WANAKUJA KUTEKELEZA MRADI WA PESA ZA MKOPO WA WORLD BANK

Nyieeeeeeeeee!
Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
Ila #TutaelewanaTu
Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini??[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala ya kutafuta makala ya bandari ya Dar na kumsikiliza mkurugenzi wa port.

Yote hayo keshayaongelea issue ni cranes za kisasa ambazo hazitoshi.

Pili wawekezaji wameelezea wanachoenda kuongezea wao hapo bandarini.

Wewe unatoka kwenda kumsikiliza kichaa mmoja Twitter ndio source yako; badala ya kuwasikiliza wahusika tena video wameonyesha ya kilichofanyika bandarini.
Hizo Cranes wanazo DP World Pekee au wenyewe ndio watengenezaji ?
 
Kwani mkataba wa Dp world na Tpa tayari? Mbona mnaendekeza Cheap Politics hivi?

Dp world vifaa vyao sio vya kitoto eti waje watumie Existing infrastructure, Hizo Crane na miundombinu mingine capability yake wanayo wao tu ama ni kampuni chache zenye uwezo huo.

Kusema kwamba Dp world wanatutegemea sisi eti mkopo wetu wa World Bank uwawezeshe wao ni chai ya mchana.
Basi tuwape bandari ya Bagamoyo. Wajenge, waweke hivyo vifaa vya kisasa, kama tulichokiwekeza sisi hakina msaada katika uendeshaji wao.

Lakini nina uhakila watakachowekeza wao hapo bandari hakitafikia hata 40% ya uwekezaji wetu.
 
Fikra ndogo sana!!

Kama ndiyo hivyo, basi tuwaulize Waingereza na Wajerumani kama wanaweza kurudi na kutufanya koloni lao, halafu wakatupatia maendeleo. Kama wakisema wanaweza, basi tubakie koloni lao milele. Tuingie nao mkataba usio na mwisho, maana tunachotaka ni wananchi wetu tu wapate huduma bora. Unalipnaje hilo bwana Covax?
Mkuu wewe unaona tuna independence au flag independence kukopa ndo tunacho jua, 47% ya bajeti ni misaada, mpaka tutakapo kubali watu wenye mitaji waje wawekeze mega project kama bandari ili tuweze kua economic indipendence, uzalendo wakumiliki mali na hatuwezi kuzitumia kubadili maisha ya wananchi ni ujinga na umesha pita na wakati.
 
Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini??[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeona Mshana... Alina Mbarawa wanasema anakuja kuwekeza fedha......... wakati WB imeshalipia kazi zote na kukamilika
 
Mkuu wewe unaona tuna independence au flag independence kukopa ndo tunacho jua, 47% ya bajeti ni misaada, mpaka tutakapo kubali watu wenye mitaji waje wawekeze mega project kama bandari ili tuweze kua economic indipendence, uzalendo wakumiliki mali na hatuwezi kuzitumia kubadili maisha ya wananchi ni ujinga na umesha pita na wakati.
Argument ya maria siyo hiyo...soma tena and internalise it
 
..Dp hatengenezi au haundi hizo Cranes.

..kuna mahali Dp ananunua Cranes, na sisi tunaweza kwenda huko kununua.

..kilichotokea ni UJINGA wa serikali ya Ccm kutokuipa bandari ya Dsm Cranes za kutosha.

..DP wanaweza kuwa MANAGEMENT COMPANY ambapo serikali itakuwa inawalipa fee.

..Mkataba unaowafanya Dp wamiliki, na Watanzania watazamaji, haufai.
Ingekuwa ni Rahisi hivyo Dp wananunua tu Mahali crane kwanini Ujerumani, Uingereza, Canada, China hawawezi nunua ZAO? Kwanini wamempa Dp?

Hivi vitu ni complicated sana ila sisi tunajifanya tu wajuaji sana.

Kampuni Zote kubwa Duniani zinapo Outsource hivi vitu lazima ziwe na mikataba ya kupewa Exclusivity Atleast Kwa Muda fulani
 
..una mawazo mazuri sana.

..sasa labda ungetupa na mifano ya nchi ambazo Dp imefanya hayo uliyoeleza.

..ni nchi gani Dp waliwekeza, wakaendesha bandari, halafu wakarudisha thamani ya uwekezaji wao, na mwisho wakakabidhi bandari kwa nchi husika?

..Na sio lazima iwe Dp. Unaweza kutupa mfano wa nchi nyingine yoyote ambako hayo mema unayodai tutatafanyiwa na Dp yamefanyika?

..Kama suala la kuongeza UFANISI wa bandari yetu ushauri mzuri ni Dp kuwa management company na sio wamiliki na wajenzi wa miundombinu hapo bandarini.
Kila nchi ina taratibu zake na sababu zake za uwekezaji.

The common denominator ya uwekezaji ni concession agreement, unaweka hela yako unapewa muda wa kurudisha kama Build Operate Contract.

But then unaweza pewa port uendeshe ata bila ya kuwekeza for efficiency purposes ila utatakiwa kufanya modernisation.

Halafu kuna siasa hasa kwa nchi zilizoendelea ajira ya serikali ina kuja na rights nyingi za wafanyakazi ambazo ni kero kwa serikali. Ukiangalia asilimia kubwa ya migomo ya cost of living in the west ni public sector.

Kwa hivyo solution yao ni kutoa sehemu ambazo sio lazima serikali kuendesha na kuwapa private kukodisha with performance targets; hiyo inaongeza ufanisi na inawapunguzia serikali zao ku deal na watu ambao ingekuwa wanasimamia wenyewe kila siku wana demand mpya na migomo.

Kwa hivyo siasa na aina ya democracy ya nchi pia zina mchango mkubwa kwenye maamuzi.
 
tumeshasema tunapinga mkataba sio uwekezaji
exactly! tunapinga contract construction na siyo uwekezaji. Funny enough hawa hawaji kuwekeza pesa zao, kazi zote zilishafanywa na WB funding..... lkn tunaambiwa watawekeza trillions
 
Basi tuwape bandari ya Bagamoyo. Wajenge, waweke hivyo vifaa vya kisasa, kama tulichokiwekeza sisi hakina msaada katika uendeshaji wao.

Lakini nina uhakila watakachowekeza wao hapo bandari hakitafikia hata 40% ya uwekezaji wetu.
Bandari ya Bagamoyo China na Oman walitaka kuwekeza miaka 30 tu then wanaondoka Tukakataa kwamba wataua Bandari ya Dar?

Hata Bandari ya Bagamoyo Dp world wanajenga, maana Bandari wanayojenga Congo (Uwekezaji wa Trilioni 3) ni kama wanaanza wao from Scratch.

Wawekezaji wote Wanataka Faida as long as Kuna faida chochote wanafanya.
 
Hizo Cranes wanazo DP World Pekee au wenyewe ndio watengenezaji ?
Zinauzwa serikali aitaki kununua kwa sababu ni hela nyingi serikali inaona kama kuna mtu yupo tayari kununua na kurudisha hela yake wampe muda; basi iwe ivyo (sasa usije kusema muda wa milele) maana hilo halipo.
 
Hayo yote ya nini jambo muhimu ni ufanisi ili serikali iongeze mapato kupitia bandari........na hilo Dp world ndo imekuja kutekeleza basi, hata kama mkataba ni wa miaka 100 as long serikali ina pata faida na inahudumia wananchi wake vizuri na kufanya maendelo hamna shida tuache fitina za kijinga.
Ukiwa mzee na mawazo haya hata mtaani kwako huna faida
 
Yaani aache kuwasikiliza wenye akili, akawasikilize wala rushwa za DP?
Sikiliza facts sio hearsay, bandari wameonyesha kilichofanyika na hizo hela tayari; huyo Maria anataka kuongelea mambo hayo hayo kama siri vile.
 
Umeona Mshana... Alina Mbarawa wanasema anakuja kuwekeza fedha......... wakati WB imeshalipia kazi zote na kukamilika
Nakushangaa kutojua kwamba WB inakupa mkopo baada ya kutimiza conditions zake ikiwemo ku akikisha una mwekezaji atakae weza kuendesha na kurudisha huo mkopo, baada ya wenyeji kushindwa usafiri kwamba wb ikui kinachoendelea wakati hiyo conditionality moja ya mkopo........jutahid kujua world economic financial policies za WB neenda akaone kwenye website yao hiyo aina ya mikopo imetolewa kwa nchi ngapi... na terms and condition ni zipi
 
Hayo yote ya nini jambo muhimu ni ufanisi ili serikali iongeze mapato kupitia bandari........na hilo Dp world ndo imekuja kutekeleza basi, hata kama mkataba ni wa miaka 100 as long serikali ina pata faida na inahudumia wananchi wake vizuri na kufanya maendelo hamna shida tuache fitina za kijinga.
Wewe ndo yule ambaye umegundua kuwa mwanao ni pung'a lakini hukereki bali ni kuishia kuwaambia majirani zako kuwa, hajalishi hilo ili mradi basha wake analeta fedha za matumizi nyumbani.
 
Back
Top Bottom