Kumbe Wakoloni walishajenga mabwawa ya umeme kama hili la Nyerere kwa kitambo sana!

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !
 
Mkuu ni kawaida sisi tupo nyuma kidogo.

Kama umewahi kuangalia move inaitwa HEAT ya mwaka 1995 utaona mule kuna treni ya umeme inapiga kazi na inaonekana ilijegwa miaka kibao(1950 au 60).

Vipi hapa kwetu train ya umeme imekuja muda gani?
 
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !

Hakuna maendeleo ya viwanda bila nishati endelevu na ya uhakika. Kujenga hili bwawa, tumechelewa sana. Tulitakiwa kujenga miaka ya 80.

Hizi thermal power plant haziwezi kukwepeka, ila zina gharama kubwa sana za uendeshaji.

Namsifu sana marehemu Rais wetu JPM kwa uthubutu wake. Bila kuwa na maono na kuamua kutosikiliza makelele ya watu, ikiwemo hao wanaozindua mradi mara mbili mbili, hilo bwawa lisingejengwa
 
Yapo miaka mingi sana mengi tu.
Juzi nilipita mahali EU wanalo hayo mabwawa mjini tu hapo yanazalisha umeme karne na karne.
Bwawa la mtera lipo zamani tu,
Hili jipya ni la kujivunia,
kama isingekua yule jambazi februari kuiba mabilioni na kwenda nazo kwao bombo siku nyingi lingezinduliwa
 
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !
Usione aibu kupongeza jambo zuri . Acha porojo za wakoloni wewe pongeza tu hata kama uliusagia kunguni.

Hili Taifa tunawatu wengi sana wasio litakia mema. Tusijidanganye uzalendo ni kila kitu katika nchi. Huwa tunajidanganya kwenye Tv lakini ukienda hata nchi zilizoendelea lazima uwe na uzalendo kwa nchi ndipo uweze kupewa uongozi.

Ingekuwa rahisi kujenga hili bwawa kila nchi ingekuwa nalo.
 
Kariba Dam.
kariba-2.jpg
2418978588_f55ea8e88b_z.jpg
0000982457_resized_karibadam1022.jpg
 
Usione aibu kupongeza jambo zuri . Acha porojo za wakoloni wewe pongeza tu hata kama uliusagia kunguni.

Hili Taifa tunawatu wengi sana wasio litakia mema. Tusijidanganye uzalendo ni kila kitu katika nchi. Huwa tunajidanganya kwenye Tv lakini ukienda hata nchi zilizoendelea lazima uwe na uzalendo kwa nchi ndipo uweze kupewa uongozi.

Ingekuwa rahisi kujenga hili bwawa kila nchi ingekuwa nalo.
Wakoloni wangeondoka Tanganyika 2000 leo tungekuwa na vini vya umeme wa nyuklia.
 
a) Miradi ni mingi
1. Hale 1964
2. Nyumba ya Mungu 1965
3. Kidatu 1970
4. Mtera 1979
5. Kihansi 2000
6. Rusumo 2025
7. JNHPP 2026
8. Maragarasi unaendelea kutekelezwa.

b) Bado tuna miradi ya umeme wa jua
1. Kishapu I
2. Kishapu II unaendelea kutekelezwa.

c) Tuna umeme kutoka chanzo cha Songas kusini. Na vyanzo vingine vingi...
 
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !
Chelewa ufike, cha msingi tumefika na tunapongeza ila sasa imebaki kuona italeta mabadiliko gani yenye ahueni kwenye gharama za umeme
 
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !
Usishangae sisi hupenda shughuri za ngoma mwezi mzima.
 
communists walidanganya sana waafrika, kama tusingewasikiliza communists leo hii tungekuwa mbali sana. maputo ilikuwa inaitwa "rio of afrika" kwa jinsi ilivyokuwa inachuana na rio ya brazili zilifanana karibia kila kitu kabla ya communists kuchukuwa na kuharibu kila kitu, lobito angola was riviela kabla ya vita ya communists iliyoharibu angola kabisa.

kwanza karibia kila kitu tunachokifanya leo plan iliwekwa na wazungu, hata hili bwawa la Nyerere plan ya kulijenga ilikuwepo tangia enzi za wajerumani, cha ajabu communists walikuja wakabomoa trajectory iliyokuwepo tuliokuwa tunaenda nayo sasa miaka 60 imepita ndiyo tunataka kurudia kule kule ambako tulikukataa miaka 60 iliyopita wakati dunia imesha move on ...
 
a) Miradi ni mingi
1. Hale 1964
2. Nyumba ya Mungu 1965
3. Kidatu 1970
4. Mtera 1979
5. Kihansi 2000
6. Rusumo 2025
7. JNHPP 2026
8. Maragarasi unaendelea kutekelezwa.

b) Bado tuna miradi ya umeme wa jua
1. Kishapu I
2. Kishapu II unaendelea kutekelezwa.

c) Tuna umeme kutoka chanzo cha Songas kusini. Na vyanzo vingine vingi...
Na bei juu.
 
Back
Top Bottom