Diamond ni mwanzilishi wa Bongofleva?Katika hali ya kuonyesha kukata tamaa na kutamaushwa, msanii maarufu na mwanzilishi wa Bongofleva hapa nchini, ndugu Diamond Platinumz, amesikitishwa na kitendo cha BASATA kufungia nyimbo zake kwa kisingizio kuwa hazina maadili. "Kama hazina maadili mbona mashabiki wanazipenda?", ameuliza. Amedokeza kuwa ikiwa hali hii anayokumbana nayo itaendelea, itabidi tu ahame nchi ambapo atakuwa huru kufanya sanaa yake bila bughudha wala kuingiliwa na mtu yeyote.
View attachment 3693005
Diamond amesema hayo huku kukiwa na rundo la tuhuma zinazomuandama, zikiwemo za ushoga na u-freemason. Baadhi ya watu wanashuku kwamba utajiri wake hautokani na muziki pekee bali pia u-freemason. Aidha katika siku za hivi karibuni, Dudubaya amesikika akimhusisha na masuala ya ushoga na utakatishaji fedha, ijapokuwa siku zote amekuwa akikanusha kujihusisha na masuala hayo.
View attachment 3693263
MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono Bwana Diamond. Kama akiona Tanzania hawamuelewi, bora tu ahamie nchi nyingine, isiwe shida. Nabii hakubaliki kwao.
Ok, tusubiri. Jamaa zaidi ya kuwa tu maarufu hana mchango mkubwa.Basi tusubiri ahame ndipo tutajua umuhimu wake. Huwezi kufahamu umuhimu wa kisima hadi kitakapokauka
Me, halafu ameshazeeka.Mwenye jina ni ke au me?
Katika hali ya kuonyesha kukata tamaa na kutamaushwa, msanii maarufu na mwanzilishi wa Bongofleva hapa nchini, ndugu Diamond Platinumz, amesikitishwa na kitendo cha BASATA kufungia nyimbo zake kwa kisingizio kuwa hazina maadili. "Kama hazina maadili mbona mashabiki wanazipenda?", ameuliza. Amedokeza kuwa ikiwa hali hii anayokumbana nayo itaendelea, itabidi tu ahame nchi ambapo atakuwa huru kufanya sanaa yake bila bughudha wala kuingiliwa na mtu yeyote.
View attachment 3693005
Diamond amesema hayo huku kukiwa na rundo la tuhuma zinazomuandama, zikiwemo za ushoga na u-freemason. Baadhi ya watu wanashuku kwamba utajiri wake hautokani na muziki pekee bali pia u-freemason. Aidha katika siku za hivi karibuni, Dudubaya amesikika akimhusisha na masuala ya ushoga na utakatishaji fedha, ijapokuwa siku zote amekuwa akikanusha kujihusisha na masuala hayo.
View attachment 3693263
MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono Bwana Diamond. Kama akiona Tanzania hawamuelewi, bora tu ahamie nchi nyingine, isiwe shida. Nabii hakubaliki kwao.
Shida ya watanzania nadhani ndiyo hii. Mara nyingi watu hawaangalii kama mwanamuziki anaachia nyimbo nzuri bali wanaangalia kama msanii anatrendi na ni maarufu.Angekuwa hana mchango hizo noti zote anazohesabu hapo kwenye video anazipataje mkuu?
Una maana gani mkuu? Kwani BASATA hawajahusika kumfungia?
Hujaelewa hoja yangu mkuu. Nasema watanzania wanaona msanii ni mzuri kwa sababu ana pesa. Akiwa anatoa ngoma nzuri halafu hana pesa Wala siyo mzuri kwa mujibu wao.Kwani wana biashara gani zaidi ya muziki mkuu? Diamond kakataa hahusiki na ushoga na u-freemason.