NB: Video hii ni kumbukizi wakati wa Kampeni za Uchaguzi mwaka 2020
Huyu kiongozi ana mkashifu Mwenyezi Mungu, oky sikiliza mpaka mwisho.👇
"…sikiliza ana mpango gani na tawi lake halafu tutaendelea kuzungumza si ndio? Si tumekuja tuzungumze pamoja, siyo kutoa maagizo sasa hivi, nataka tujue kati ya matawi 6 makatibu tawi mpaka leo hii tarehe 3 bado siku 20 tunakitu. Mipango yenu ni nini ya kuifanya CCM ishinde. Kwasababu ushindi wa CCM hauna Mungu akipenda.
"Hili mnalijua? Ushindi wa CCM hamna mpaka Mungu apende Hapana, Mungu akijaalia, Hapana, ushindi wa CCM ni lazima na kushinda ni lazima hata iweje, kwahiyo Mungu akipenda.
"Mimi nataka kwanza niwasikie Makatibu Tawi si wana Kamati za Siasa, hata kama wamekuja watatu si wana mipango yao? Naomba nijue tawi moja moja kwanza, wana mipango gani."
Acha kulazimisha Mungu wako awe wa watu wote. Dunia hii zipo imani tofauti. Hivi unataarifa kwamba kuna wale Wanaabudu Ng'ombe, Mawe Miti na wasioabudu? Msemaji yuko sahihi kulingana na Imani yake acha kulazimisha uelewa wako uwe Universal. Over

Is that not a misconstruation of the statement? Hivi kwenye uhitaji wa kufanikisha jambo lolote muhimu inatakiwa kumwachia tu Mungu au kuwepo na jitihada binafsi kwanza huku ukimwomba Mungu akusaidie jitihada zako zizae matunda?