KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

Vipi katika kupatia na kukosea katika misingi ya Falsafa ? Namaanisha Falsafs na Mantiki nayo unaipimaje kama imepatia au kukosea, sababu inaonekana msingi wao mkuu Elimu hizi ni AKILI.
 
Ulichosema ni sahihi kabisa, katika vitu vinavyotakiwa kuwahishwa ni kuzika. Wapo watu walikufa saa kumi na mbili jioni akazikwa saa mbili usiku. Alimuhimu hakuna haja ya kuchelewesha maiti zaidi ya kujipa gharama na kupoteza muda.

Tuko pamoja.
 
Kuna kipindi lilikuwa na mgogoro sijui ni mipaka au ninini..likapigwa X..kama bado lipo tunaweza kujipanga upya[emoji848][emoji848]
Kuna Bro mmoja kitaa alikuwa analipenda sana gazeti la JITAMBUE nikawa na muona mtu wa ajabu sana. Mada zake nilikuwa sizielewi kabisa.
 
Uzi maalumu kwa watu maalamu,hasa sisi wa kipindi kile ambapo kusoma makala haikuwa shida.
 
Vipi katika kupatia na kukosea katika misingi ya Falsafa ? Namaanisha Falsafs na Mantiki nayo unaipimaje kama imepatia au kukosea, sababu inaonekana msingi wao mkuu Elimu hizi ni AKILI.
Falsafa ni wazo, halafu mantiki ndio inazaa dhana....sasa dhana inaweza kuwa dhanifu ama halisi
Shule na elimu zetu vina ukomo, na ukomo wake unaishia kwenye mantiki ya dhana halisi , hivyo huwa vigumu kumtoa mtu kutoka dhana halisi kumpeleka dhanifu..na hapa ndio tatizo la kimantiki linapoanzia
Wenzetu wamewekeza kwenye falsafa kama msingi wa mfumo mzima wa dhana dhanifu ama dhana maizi na kutoka hapo ndio hutohoa michakato yote na kuihuisha na dhana halisi
Na kwenye hilo la kuhuisha wameipa falsafa makundi mbalimbali..kwa maana ya kwamba.. Msingi wake ni mmoja lakini wenye matawi mengi
 
Kuna Bro mmoja kitaa alikuwa analipenda sana gazeti la JITAMBUE nikawa na muona mtu wa ajabu sana. Mada zake nilikuwa sizielewi kabisa.
Hii ndio elimu ya utambuzi...kuongea ama kuandika vitu beyond normal thinking ya binadamu wengine
 
Kweli dunia ni jumba. Natamani wengi tungelijua na kulithamini hili, labda maisha yetu na watu wetu yangekuwa yamepiga hatua.
 
Hii ndio elimu ya utambuzi...kuongea ama kuandika vitu beyond normal thinking ya binadamu wengine
Shida katika Falsafa na Mantiki ni kuufikia ukweli kama ulivyo. Kama elimu haikusaidii kuufikia Ukweli ujue ina shida.

Kufikiri kuliko tukuka kunataka msaada wa njia madhubuti zaidi ya akili(Falsafa na Mantiki) pekee.
 
Late 90's to early 2000
moja ya mtu mahiri munga tehnanan mungu kutokea kwa sisi tuliobahatika kupata nakala zake na kuhudhuri kongamano zake hakika tunamkumbuka kila siku hadi sasa hakuna aliyeweza kuandika nakala za munga!
rest in peace munga.....
 
nashukuru sana kaka watu kama nyinyi mnatambua uwepo wa gwiji huyu wa elimu ya utambuzi....
moja ya mtu mahiri munga tehnanan mungu kutokea kwa sisi tuliobahatika kupata nakala zake na kuhudhuri kongamano zake hakika tunamkumbuka kila siku hadi sasa hakuna aliyeweza kuandika nakala za munga!
rest in peace munga.....
 
Binafsi kazi zake zimenisaidia sana kujitambua japo sikumfahamu mapema , sikuwahi kosa gazeti la Jitambue au mshauri nikipata muda nitaangalia nilikoficha baadhi, wengine niliwapa wakasome kwa kutojua thamani ya kilicho ndani waliyateketeza na nilipoyahitaji viswahili vikawa vingi. leo hii kila nikishauri lazima nizungumzie umuhumu wa KUJITAMBUA.
 
Dah! Munga Tehnan alikuwa mwalimu/ mentor wangu. Mshana Jr inawezekana tulikuwa darasa moja na tunafahamiana kupitia mtu huyu maana kuna wakati unatoa mada ambazo nahisi kama ulikuwa akilini mwangu.

Huwezi kuamini lile gazeti la Jitambue alikuwa anaandika peke yake (kwa majina tofauti na angle tofauti) kuanzia page 1 hadi page ya mwisho...
 
Kipindi hiko nilikuwa na msichana nikiwa chuo yeye alikuwa secondary kila tukionana alikuwa ananikuta na gazeti la jitambue hakuwa akinielewa aliona nina mambo ya kizee na hata magazeti ninayoyapenda ni ya kizee alikuwa halielewi hata akiamua kulisoma the same applied to me nilikuwa simwelewi na magazeti yake ya KIU, RiSASI, UWAZI just to mention a few.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…