KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake


Za siku mingi mkuu.

Munga alikuwa na kipaji kikubwa. Taifa limepoteza mtu muhimu. Pengo lake tunalihisi hata sasa.
 
Na haikua "jinsi nilivyofedheheka" ilikua "Siku niliyofedheheka"
kumbuka vizuri

Yaani huwezi amini niko likizo fupi nikayakumbuka haya magazeti hadithi zake(mama alipenda kunisomea)nikasema em niandike kisa kimoja kutoka humu,.hapa niko kuyachambua na kuyapanga tena kwenye shelf....gazeti lingine ni Mshauri Wako
Mother Confessor tusaidie kupata shot gazeti la jitambua safu hii, tujikumbushe jina lake.
 

Yeah kaka nadhani ni kweli tunafahamiana...familia ya FAJI huwa haijifichi
 
Munga Tehenan hakika alikuwa lulu iliyotutoka. Nafarijika sana Mshana Jr umeamua kuleta wazo la kumbukizi la gwiji huyu wa KUJITAMBUA.

Nilimjua Munga kupitia gazeti la JITAMBUE na gazeti la WAKATI NI HUU. Nilipoanza kusoma gazeti la JIITAMBUE sikuacha kulinunua na kulisoma hadi lilipopotea mitaani baadaye tukapata taarifa amefariki. Nililia na kuwa na huzuni kwa takribani wiki mbili.

Kupitia mawazo yake ndani ya JITAMBUE alinifanya nisipate sononi katika kipindi kigumu nilichokuwa napitia enzi za kusoma magazeti yake. Huwa najiuliza ni ipi namna bora ya kumuenzi kipenzi chetu MUNGA?. Ahsante Mshana kwa kutukumbusha mwana FALSAFA mahili Munga.
 
Mkuu
Mkuu Mshana Asante Sana kwa Bandiko Hili... Umenikumbusha Mbali Sana natamani mno kupata Maandiko ya Huyu nguli... Kadiri inavyowezekana tusaidie... Na kila post ya Andiko lake nitacopy nitunze
 
Nakumbuka pia kabla ya kuanzisha gazeti lake la Jitambue alikuwa mhariri wa gazeti la Majira. Nilimfahamu, alinifahamu, yaani tulifahamiana sana. Nimewahi kukaa na Munga sehemu kadhaa. Alikuwa ni mtambuzi wa tabia za Binadamu. Aliwahi kuniambia ukitaka kujua tabia ya mchora katuni angalia michoro yake kwa sababu, anachokichora kinatoka akilini mwake. Ofisi za Gazeti la Jitambue zilikuwa zipo Kimara. Mshana una kumbukumbu sana.
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545] kuna mwenzetu hapa amesema bado ana nakala karibia zote za gazeti la Jitambue, naangalia namna ya kufanya project tuhamishie kwenye soft copy...japo hapo kuna changamoto nyingi ikiwemo ya haki miliki
 
Mkuu

Mkuu Mshana Asante Sana kwa Bandiko Hili... Umenikumbusha Mbali Sana natamani mno kupata Maandiko ya Huyu nguli... Kadiri inavyowezekana tusaidie... Na kila post ya Andiko lake nitacopy nitunze
Pouwa nitafanya hivyo bila shaka
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Nilianza kumsoma Munga akiwa anaandikia gazeti dada la majira yaani dar leo lililokuwa likitoka mchana baadae akawa anaandikia gazeti la cheche ambalo lilikuwa na habari nyingi za rais Kabila marehemu wakati huo anapambana na Mobutu.
Alipoanzisha gazeti la jitambue marafiki zangu walikuwa wakishangaa kwanini nasoma hilo gazeti lakini nilipowapa wakawa wapenzi wakubwa wa hilo gazeti.
 
Story ya yule mtoto aliyepata ajali na kupoteza wazazi wake, zote nilisoma kwenye gazeti la jitambue enzi hizo za Y2K...!

Hiyo story mpaka leo inanisisimua damu, tuliwahi ijadili hapa na ile ya yule kibaka wa Temeke
Yes....
Nazikumbuka zote.
Yule mtoto wa Siame...inasisimua sana
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…