KUMBUKIZI | Rais Samia: Siasa ni mchezo wa fikira na mawazo na kulumbana kwa hoja

KUMBUKIZI | Rais Samia: Siasa ni mchezo wa fikira na mawazo na kulumbana kwa hoja

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Rais Samia 08 Machi 2023 akiongea na BAWACHA alinukuliwa kusema "Wote tumejawa na furaha. Na hiyo ni kwa sababu ya matunda ya mazungumzo na maridhiano. Ndugu zangu siasa ni mchezo. Mchezo wa fikira na mawazo, kulumbana kwa hoja, kuangalia kakosea wapi tumzodoe na mimi naona kaongea nini namjibu. Hamna dhamira ya kushika dola 25, manajua mama yupo dhamira hiyo haipo.

Wote tuna lengo hilo lakini sasa tukafanye kwa ustaarabu, kama wanadamu, kama watu, tuheshimiane na nchi yetu iheshimike duniani. Nataka kuwaambia, kipindi hiki kifupi, nchi yetu inaheshimika sana duniani. Kwa iyo, tusirudishe chini, tusirudishe nyuma. Tuendeni na mwendo huu, tuweke heshima ya nchi yetu, pala inapostahili.

Tanzania ni taifa kubwa, tusilitole sifa yake. Nimefurahishwa na nyimbo zenu.Nilikuwa nazisikiliza. Ukiacha kile kipande, sijui cha tarehe tano, mwezi gani, sijui tuliandamana. Tukafanywaje sijui, ee, tunadai.

Lakini maneno mengi yote ni ya haki, ambayo ndo tunaitetea hata sisi CCM. Mnasema CHADEMA, tunataka amani. Na sisi tunakikishia, tunataka amani. Twendeni, tudumishe amani yetu ya nchi. Kuna beti zinasema, vitisho, kupigana, sijui kufanya aje, na nna hakika zile beti zita badilika karibu. Kwa sababu si, mmesema, mmesema wenyewe na mwenyekiti ya mesema. Kwamba sasa tunaona, mambo yamenyooka.

Nadhani zile beti nazo, zitakwenda kubadilika. Lakini nimevutiwa pia na lile la mwamba, tuvushe salama. Sasa nataka mkaibadilishe mseme mama, tuvushe salama."
 
Back
Top Bottom