Kumbukizi ya miaka 59 toka Said Mwamwindi amuue RC Dkt. Kleruu siku kama ya leo mwaka 1971

Tungeipata pia hii simulizi ya Kisoky ingekuwa poa sana
 
Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania
 
Umeandika kwa hisia mtu anaweza akadhani kuwa wewe ni Maggid Mjengwa mwenyewe, au japo mtu wake wa karibu sana
 
Mwandishi kazi nzuri sana, inaonekana watu walikuwa wachapa kazi na walianza kuendelea miaka mingi sana ila siasa za kijamaa zikaturudisha nyuma sana, somo zuri kwa watu wasio na adabu, waonezi na ubabe wa kifala kama Makonda na Sabaya
 
Kwa sababu nachukia uvivu na wanaopromote uvivu, hasa kampuni za betting na hizo sera za kijamaa, yaani wengine wasafishe mapori we uje ulime tu, na mapori bado yamejaa, kwanini wasiende kusafisha?
Kampunj za kubeti unazionea tu wala hazipromote uvivu ila zinapromote free market economy coz huwez kubet kama Huna hela na ili upate hela ni lazima uitafute.

Wale wadau wa kubet lazima tukupinge kwa nguvu kwa hoja hiyo.
 
Asante kwa historia nzuri kama hii! Kwa mazingira yale kibinadamu Muuaji hakuwa na namna!
 
Kampunj za kubeti unazionea tu wala hazipromote uvivu ila zinapromote free market economy coz huwez kubet kama Huna hela na ili upate hela ni lazima uitafute.

Wale wadau wa kubet lazima tukupinge kwa nguvu kwa hoja hiyo.
Betting ni kazi? Kama ni kazi, inazalisha bidhaa / huduma ipi?

Maana kazi ni lazima izalishe kimoja wapo (bidhaa au huduma).
 
Unajichanganya tuu naona, na akili kama zako ndio maana hatuna umeme wala maji na Hospitals zetu ni za ovyo kabisa, Acha watu wafanye kazi wamiliki hayo makampuni ya umeme na mahospitali, serikali ikusanye Kodi na kusimamia haki na Sheria zilizopo ili biashara na uzalishaji viende vizuri
 
Ilibidi aje Mzee Nyerere mwenyewe, lakini akastukia mchezo akamtuma Rashid Kawawa. Wazee wa Kinyakyusa wakajipanga kumsubiri Nyerere wakashangaa kwenye Land Rover anashuka kawawa.

Wakakasirika mno wakaanza kusema "Kapimba" kumaanisha mtu mfupi amekuja kufanya nini hapa wakati sisi tunamtaka Nyerere mwenyewe. Kawawa kafanyiwa fujo, na baadaye hapo uwanjani zikaja NYUKI zikaanza kumfukuza, ambapo alikimbia kweli mzee wa watu hadi kwenye Land Rover lake huyo akaondoka.

Nyerere akaona haitoshi, hawa Wanyakyusa jehuri waliokataa UJAMAA ni kuwakomesha. Akamteua rafiki yake MARWA, kijana wa Kikurya Machachari awe RC Mbeya.

Marwa akaanza mbwembwe kama za Kreluu, kuwatishia Wanyakyusa kwamba yeye kaaga kwao na atawanyoosha. Wazee wa Kinyakyusa wakasema huyu kijana anatutukana sisi, tutaona.

Marwa katika jitihada zake za kulazimisha Ujamaa kwa Wanyakyusa alijikuta anatangulia peponi mapema. Siku moja RC yuko kwenye sherehe chakula kipepikwa, baada ya hapo tumbo likaanza kuvimba.

RC anakunywa maji wapi, tumbo linavimba tu na kiu haikati. Kijana wa watu wa kikurya akafia njiani, na ndiyo jitihada za kulazimisha UJAMAA kwa Wanyakyusa zikafia hapo.

Mzee Nyerere alifura mno kwa hasira na kutuma polisi kuwafanyia vurugu Wanyakyusa, ambapo watu walisulubishwa kwelikweli kwasababu wamemuua RC jehuri.​
 
 
Ye aendelee tu kuandaa kitabu, kila siku wasomaji wapya na wenye kutaka kujua kilichotokea kwa kleruu na mwamwindi wanaibuka,

Mfano me mwenyewe bado kuna vitu naamini hatujavijua au kujulishwa vizuri juu ya tukio hilo hivyo kama kutakuja kitabu kipya nitakinunua tu kwani kuna mengi sn ya kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…