MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,974
- 12,662
Watu wakipata vyeo wanasahau kuwa bado wana miili ya nyama na damu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JOHN CRABLE(maarufu Crable) alikuwa headmaster na makazi yake yalikuwa hapohapo shuleni pamoja na walimu wote.1. Usuli
Jumamosi mujarab ya leo, Desemba 25, 2021, siku ya Krismasi, imetimia nusu karne toka "Mnyalukolo" SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI (42) amtangulize Mbele ya Haki, Mh. Dk. WILBERT ANDREW KLERUU, aliyekuwa Regional Commissioner ("RC") wa Iringa, Jumamosi kuntu ya Krismasi, Desemba 25, 1971, baada ya kummiminia risasi kijijini Mkungugu, Isimani, maili takriban 23 toka Iringa mjini kuelekea Idodomia.
"Atikali " hii inatiririsha kinagaubaga kilichotaradadi na kupelekea "Mnyalukolo" huyo machachari, Bw. MWAMWINDI , kusema "Swela" na kisha kuchukua bunduki yake na kuhamisha risasi toka kwenye bunduki hiyo kwenda kwenye mwili wa "RC" huyo na kupelekea kifo chake kilichosababisha songombingo kubwa ambayo kwayo, "Wanyalukolo" hawatakuja kuisahau, aslan abadan !.
"Atikali" hii inaanza kwa kuelezea historia fupi ya marehemu Dk. KLERUU aliyekuwa Msomi Mbobevu na Mjamaa wa aina yake.
2. Dk. KLERUU: Msomi Mbobevu
Marehemu Dk. WILBERT ANDREW KLERUU alizaliwa huko Mwika, mkoani Kilimanjaro. Alipofika umri wa kuanza shule, alipelekwa shule. Shuleni alikuwa na akili sana darasani zilizochagizwa na juhudi kubwa za kubundi. Alipofanya mtihani wa shule ya msingi na shule ya kati aliwatimulia vumbi wanafunzi wenzake wote. Hiyo ikapelekea aheshimiwe na wanafunzi wenzake na apendwe sana na waalimu.
KLERUU alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya "Old Moshi" alikosoma na watu wengine waliokuja kuwa mashuhuri kama vile EDWIN MTEI, HERMAN SARWATT, ABDULRAHMAN MSANGI & DANIEL MFINANGA. MTEI amemuelezea KLERUU kwenye kitabu chake "From Goatherd to Governor" Uk. 24 kuwa alikuwa anapenda masomo na hakukosa kufika shule licha ya kuishi mbali-:
"I was fortunate that my home was only one kilometer from the school. Wilbert Kleruu (at that time his name was Ndechumia Ndefuno) used to walk more than 10 kilometres from his home in Mwika. Whether it rained or however cold it was, Wilbert used to be even more punctual than those, like myself, who resided nearby...".
Baada ya kufaulu mitihani yake kwa kiwango cha juu, KLERUU alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Wavulana Tabora "Tabora school", iliyokuwa maarufu kuliko shule zote nchini.
KLERUU alisoma darasa moja na MTEI, JOB LUSINDE, OSCAR KAMBONA, MARK BOMANI, GEOFREY MMARI, JOHN PENDAEL, ANORD TEMU, ALFRED MEENA, ROWLAND MWANJISI, G. SIMITI & O. MWAMBUNGU huku Mkuu wa shule akiwa ni mzungu akiitwa JOHN CRABBE. Darasa hili linakubalika na wengi kuwa ndilo darasa lilikuwa na vipanga wengi kuliko madarasa yote toka shule hiyo ianzishwe mwaka 1922. Kipanga wa Vipanga wa darasa hilo alikuwa ni EDWIN MTEI "Tanganyika One" wa 1952.
KLERUU alipomaliza masomo ya sekondari shuleni hapo akaenda Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda "The Harvard of Africa" na kisha Marekani. Nchini Marekani, KLERUU alipata Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Political Science kwenye Chuo Kikuu cha California, Los Angeles. Hivyo, Dk. KLERUU alikuwa mmoja wa wananchi wa mwanzo kupata PhD (PhD yake ilitokana na kupiga kitabu kisawasawa hadi usiku wa manani akiweka miguu kwenye karai la maji na sio ya hisani kama PhD za hisani (Mbeleko) zilizotamalaki Bongo miaka hii ambapo kila "Tom, Dick & Harry anaweza kupewa ili mradi tu aitwe "DK" !!!.
3. Dk. KLERUU Awa "Publicity Secretary" wa TANU
KLERUU alirejea nchini mwanzoni mwa miaka ya 1960s akiwa na gamba lake la Uzamivu kibindoni kisha akaanza kujulikana kama "Dk. KLERUU " na akateuliwa kuwa "Publicity Secretary" wa TANU.
4. Rais NYERERE Amteua Dk. KLERUU Kuwa "RC"
Baada ya kufanya kazi nzuri ndani ya TANU kwa takriban muongo mmoja, Rais wa kwanza wa nchi yetu, Mwalimu JK NYERERE, alimteua Dk. KLERUU kuwa RC wa Ntwara. Hii ilitokana na imani kubwa ya Rais NYERERE kwa Dk. KLERUU.
5. Dk. KLERUU: RC Machachari Sana
Dk. KLERUU alikuwa RC machachari sana na sifa zake zilienea nchi nzima.
Dk. KLERUU alifanya kazi kubwa kuhakikisha ulinzi unakuwa imara mkoani Ntwara kwani enzi hizo kulikuwa na mapambano makali ya kudai uhuru wa Nchumbiji ambapo nchi yetu ilitoa mchango mkubwa kwa wapigania uhuru wa nchi hiyo.
Katika utendaji wake, Dk. KLERUU alikuwa akiwapeleka wakulima nginjanginja. Aidha, Dk. KLERUU alikuwa hana simile na hakusita kuwafokea na kuwadhalilisha wafanyakazi, hata Wakurugenzi, mbele ya kadamnasi, pale alipohisi kuna uvivu na uzembe. Bw. PHILIP RAIKES alimueleza Dk. KLERUU kwa ufupi na weledi katika kitabu chake "Agrarian Crisis & Economic Liberalization in Tanzania 1979-:"
"Dr. Kleruu had achieved a certain local popularity largely because of his habit of abusing civil servants in public. His expropriation of the rich peasants also seems to have been quite popular, especially of course with those who received the land".
6. RC Dk. KLERUU Aweka Rekodi
Mwaka 1970 akiwa RC wa Ntwara, Dk. KLERUU aliweka rekodi ya kuanzisha vijiji vingi vya ujamaa Tanzania. Kati ya vijiji 2000 vilivyoanzishwa Tanzania, yeye peke yake alianzisha vijiji 750. Hili lilimpendeza mno Rais NYERERE.
7. Rais NYERERE Amhamishia RC DK. KLERUU Iringa
Rais NYERERE alimpongeza sana Dk. KLERUU kwa mafanikio hayo makubwa ya uanzishwaji vijiji vya ujamaa na katikati ya mwaka 1971, akamuhamishia mkoani Iringa, moja ya mikoa iliyounda "The Big 4" nchini, ili akasambaze mafanikio hayo ya Ntwara. RC Dk. KLERUU, alipohamia Iringa, alichukua nafasi ya Mh. RC JOHN MWAKANGALE.
Eneo la Isimani mkoani Iringa ndiko kulikokuwa kumeshamiri kilimo cha mahindi na kuuletea heshima mkoa wa Iringa kwani ndiyo iliyokuwa ikiongoza nchi nzima kwa kilimo cha mahindi. Hata kitabu cha Jiografia shule za msingi kilikuwa na sura ya "Kilimo cha Mahindi Isimani". Bw. AMANI MWAMWINDI ( mtoto wa kwanza wa MWAMWINDI ambaye pia alikuja kuwa Meya wa Iringa) alielezea kuhusu umuhimu wa Isimani enzi hizo, alipoongea na gazeti la Mwananchi mwaka 2016-:
"Mji wa Iringa umejengwa na Matajiri wa Isimani, akiwemo Mzee wangu, kwavile matajiri wakulima wa Isimani walijenga majumba yao ya kifahari Iringa mjini ikiwemo eneo la Mshindo, Mlandege na Kihesa. Kuna wakati nchi ya Zambia ilikumbwa na baa la njaa na Isimani ndio iliyotoa msaada wa mahindi".
8. Wananchi Ntwara Wademka Wakishangilia Uhamisho wa RC Dk. KLERUU!
Katika hali ya kustaajabisha, baadhi ya wakazi wa Ntwara walifurahia mno mara tu baada ya RTD kutangaza uhamisho wa RC huyo wa shoka. Wananchi hao, bila hiyana, walijimwaga mitaani na wengine kwenye mabaa na vilabu vya pombe ambako walikuwa wakidemka kwa furaha na bashasha kubwa bila kificho!.
Bw. DAVID BUTININI ,(baba yake DUNCAN BUTININI, mchezaji wa zamani wa Reli ya Morogoro), aliyekuwa askari polisi na kada kindakindaki wa TANU enzi hizo akiwa Ntwara kabla ya kuhamishiwa Iringa na ambaye pia alikuja kuwa shahidi kwenye kesi ya MWAMWINDI, alihabarisha kuhusu undava wa RC Dk. KLERUU-:
"Kule Mtwara, Dk. Kleruu alionekana mtemi sana. Lakini tuelewe kuwa wakati ule tulikuwa tunawasaidia ndugu zetu wa Frelimo kwani kulikuwa na vita hivyo kulihitaji mtu mbabe kama Dk. Kleruu. Kwa maoni yangu, Dk. Kleruu alipaswa kujifunza kwanza mila na desturi za Wahehe kwani Wahehe ni Wahehe tu. Mji wa Iringa ulikuwa na kikundi kidogo cha wakulima matajiri wa Isimani ambao ndio waliijenga Iringa".
9. RC Dk. KLERUU Atinga Iringa na Mkwara mzito!
RC Dk. KLERUU, kijana wa miaka 35 akiwa na damu inayochemka, hakuwa mtu wa mchezo-mchezo. Alipotinga tu Iringa aliwachimba mkwara mzito "Wanyalukolo" kuwa kamwe hatavumilia uzembe na uvivu. Pia, aliwaonya kuwa tabia ya baadhi yao ya kushinda kutwa nzima wakifakamia ulanzi, kangara na komoni itakuwa ni historia. Mzee maarufu Iringa mjini enzi hizo, Bw. OMAR MSELEM NZOWA, rafiki wa zamani wa MWAMWINDI, anaeleza jinsi Dk. KLERUU alivyochimba mkwara mzito siku ya kwanza tu alipokanyaga mkoani Iringa, ambapo Dk. KLERUU alinena-:
"Nyie naona hamnijui mimi. Kawaulizeni watu wa Mtwara ndio watawapeni habari zangu. Mimi sio mtu wa kuchezeachezea na sina utani hata kidogo. Uvivu na uzembe vitakuwa historia mkoani hapa".
RC Dk. KLERUU hakuwa mtu wa kukaa ofisini bali aliwafuata wananchi na kushirikiana nao bega kwa bega katika shughuli za ujenzi wa Taifa. Kushika jembe na kulima au kushika panga na kukata miti, kwake ilikuwa ni kama kumsukuma mlevi mzee aliyelewa mataputapu chakali!.
10. RC Dr. KLERUU Aanzisha Kampeni Kabambe ya Kilimo
Moja kati ya shughuli za mwanzo za RC Dk. KLERUU alipofika Iringa ilikuwa ni kuanzisha kampeni kabambe ya kutaifisha mashamba makubwa ili yawe ya vijijiji vya ujamaa kufikia mwishoni mwa Novemba 1971.
Huyu ndiye RC DR. KLERUU.
Baada ya kumjua RC Dk. KLERUU, ni vyema sasa kumjua Bw. SAID MWAMWINDI.
11. "Mnyalu" SAID MWAMWINDI ni Nani?"
Bw. SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI ni "Mnyalukolo" aliyezaliwa Iringa mjini mwaka 1929 ambapo baba yake alikuwa jumbe eneo la Mshindo.
Bw. MWAMWINDI akaja kuwa dreva na kisha akaoa. Mwaka 1954 yeye na familia yake walihamia Mkungugu, Isimani ambako aliweza kulima kidogokidogo, huku akitembea masafa marefu kutafuta maji hadi akamiliki hekari nyingi na kuselelea hukohuko kijijini Mkungugu. Kilimo kilimnufaisha sana hadi akawa tajiri mwenye mashamba makubwa, matrekta na majumba kadhaa Iringa mjini.
Huyu kwa kifupi ndiye Bw. SAID MWAMWINDI.
Je, nini kilijiri kati ya mafahari hawa wawili, Dk. KLERUU na Bw. MWAMWINDI, mwezi Desemba 1971?.
12. RC Dk. KLERUU Aitisha Mkutano na Wakulima Wakubwa
Desemba 23, 1971, RC Dk. KLERUU aliitisha mkutano na wakulima wakubwa wa Isimani kuwaelezea azma ya serikali kuyachukua mashamba yao na kuyageuza kuwa vijiji vya Ujamaa.
Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa "Welfare" mjini Iringa. Wakulima hao wa "Kinyalukolo" , Bw. MWAMWINDI akiwa mmoja wao, walicharuka vibaya sana. Hoja yao ilikuwa kwamba si sahihi kuwapoka mashamba yao wakati mapori bado yako mengi. Hivyo, mkutano huo ulivunjika bila kupata muafaka wowote.
Bw. AMANI MWAMWINDI anasimulia-:
" Baada tu ya mkutano huo kumalizika, baba alikuja kwangu Mlandege. Akaniekeza kuwa kwenye mkutano huo, yeye alimshauri Mh. Dk. Kleruu kuwa ni bora akawasaidia wale ambao hawajaanza kutembea kuliko kuhangaika na wenye uwezo wa kukimbia. Hoja yao wakulima ilikuwa ni kwamba wao walifyeka mapori miaka ya 50 na mapori bado yako mengi, kwanini wananchi wengine nao wasiende kufyeka mapori hayo? Wakulima wale matajiri, akiwemo baba, walipanga kutafuta mwanasheria kutoka hata Uingereza ili aje kuwatetea kwenye uovu ule waliotaka kufanyiwa".
13. RC Dk. KLERUU Atinga Shambani Kwa Bw. MWAMWINDI Siku ya Krismasi
Mh. RC Dk. KLERUU alikuwa ni kiongozi mchapakazi hodari aliyekuwa akiwaza kazi masaa ishirini na nne na haikuwa jambo la ajabu kumkuta usiku wa manani akifuatilia jambo hili au lile. Aidha, mapumziko ya wikiendi au sikukuu hayakumhusu hata kidogo.
Hivyo basi, alasiri ya Jumamosi, Desemba 25, 1971, siku ya Krismasi, RC Dk. KLERUU alichukua gari la RC, Peugeot 404, rangi ya bluu ambayo ubavuni ilikuwa imeandikwa "RC Iringa", akavaa kofia ya pama na kuelekea Isimani. Katika hali ya kustaajabisha, RC huyo alienda bila mlinzi wala ulinzi wowote!. Alienda kwanza kwa mkulima mkubwa aliyeitwaye RASHID JUMA huko Nyang'olo lakini akamkosa.
Saa 10 jioni, RC Dk. KLERUU akafika shambani kwa Bw. MWAMWINDI na akamkuta akilima. Bw. MWAMWINDI alikuwa juu ya trekta lake pamoja na mwanae (MOHAMED) na watu 2 aliokuwa amewaajiri (YADI CHAULA & CHARLES MWAMALATA) na mkwewe JOSEPH KISAVA.
14. RC Dk. KLERUU Atunishiana Msuli na Bw. MWAMWINDI!
RC Dk. KLERUU, aliyekuwa jeuri kwelikweli, bila kusabahi, alianza kuvurumisha maswali chechefu yaliyomkera sana Bw. MWAMWINDI. Kwa mujibu wa Bw. MWAMWINDI na mwanae, MOHAMMED, aliyekuja kuwa shahidi wa 6 upande wa utetezi, mazungumzo yafuatayo ndiyo yaliyojiri:
RC Dk. KLERUU-: "Unafanya nini hapo?" .
Bw. MWAMWINDI-: "Nalima shamba langu".
RC Dk. KLERUU -: "Kwanini bado unaendelea kulima , shenzi wewe".
Bw. MWAMWINDI-: "Mbona unanitukana kwani nimefanya kosa gani?"
RC Dk. KLERUU- : "Funga domo lako, ng'e ng'e ng'e, hii hii nini? Bloody fool, kwanini hutaki mashamba yako yawe ya ujamaa?".
RC Dk. KLERUU alikuwa akiuliza maswali hayo huku akimtomasatomasa tumboni Bw. MWAMWINDI, aliyekuwa juu ya trekta lake, kwa kutumia kifimbo chake alichopenda kutembea nacho.
Bw. MWAMWINDI akahamaki na akasema "Swela". Kikawaida "Mnyalu" akitamka neno hilo kaa mbali.
Ghafla bin vuu, Bw. MWAMWINDI akaelekea kwenye nyumba yake iliyokuwa jirani huku akifuatiwa kwa nyuma na RC Dk. KLERUU. Walipopita makaburini kabla ya kuifikia nyumba hiyo, RC Dk. KLERUU akamwambia- "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu!".
Bw. MWAMWINDI akajibu- "Hizi sio nyumba, ni makaburi ninapozikia ndugu zangu mfano marehemu baba, mwanangu na shangazi zangu".
RC Dk. KLERUU akamwambia-: "Ni mahali unapozikia mirija wenzio, mbwa wee!".
"Mnyalu" MWAMWINDI akazidi kufura hasira hivyo akaongeza kasi ya kuelelea nyumbani kwake!.
15. Bw. MWAMWINDI Ammiminia "Shaba" RC Dk. KLERUU!!!
Kufumba na kufumbua, Bw. MWAMWINDI aliingia ndani na akachukua bunduki kisha, kama afanyavyo muigizaji Mbelgiji JEAN-CLAUDE VAN DAMME, akammiminia risasi RC Dk. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo bila hata kuomba maji!.
16. Bw. MWAMWINDI Aripoti Polisi
Bw. MWAMWINDI akachukua pama ya RC Dk. KLERUU akaivaa, akatoa ufunguo wa gari mfukoni mwa suruali yake kisha akauingiza mwili wake kwenye kiti cha nyuma cha ile Peugeot 404 kwa kusaidiana na mwanae, MOHAMMED. Baada ya hapo akawasha gari lililokuwa na bendera ya Taifa akaelekea Iringa mjini.
17. Bw. MWAMWINDI Aukabidhi Mwili wa RC Dk. KLERUU Polisi!
Alipofika Iringa mjini, Bw. MWAMWINDI aliwashangaza watu kwani alikuwa akiendesha gari upande wa kulia hali iliyofanya watu wahisi RC Dk. KLERUU ana dharura kwani barabara aliyotumia ni "One way" na gari hushuka Kusini, hazipandi Kaskazini. Bw. MWAMWINDI alipofika Kituo Kikuu cha Polisi alienda "counter" na kumkuta PC MBETA KASONDA na akamkabidhi funguo na bunduki kisha akamueleza-:
"Nendeni kachukueni mbwa yenu kwenye gari, tayari nimeishaiua".
18. PC KASONDA Ashangaa Kubaini ni RC Dk. KLERUU!
PC KASONDA alipigwa butwaa kubwa na hakuamini macho yake alipobaini kuwa mwili uliokuwa kwenye gari ni wa RC Dr. KLERUU! RC Dk. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli jeusi huku mwili ukiwa umetapakaa damu. Mara moja PC KASONDA akamuweka Bw. MWAMWINDI chini ya ulinzi. Tarumbeta likapigwa na askari wakakusanyika na kujuzwa kifo hicho kisha gari likahifadhiwa nyuma ya kituo hicho cha polisi. Askari wanne walienda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali ya mkoa na mwili ukaenda kuhifadhiwa "mortuary" ya hospitali ya mkoa.
19. RTD Yatangaza Kifo cha RC Dk. KLERUU
Watu waliokuwa wakisheherekea Krismasi, maeneo mbalimbali nchini, walishtuka sana baada ya RTD kuutangazia umma kuhusu kifo cha RC Dk. KLERUU katika taarifa yake ya habari ya saa 2 usiku. Majonzi yalitamalaki nchi nzima hasa kutokana na jinsi kifo hicho kilivyotokea na kwavile kilitokea siku ya Krismasi.
20. "WANYALU" Washangilia Kifo!
Kulikuwa na baadhi ya "Wanyalu" mkoani Iringa waliokuwa wakimchukia sana RC Dk. KLERUU kutokana na aina yake ya utendaji kazi. Hivyo, usiku huo walipopata taarifa ya kifo chake tu, walianza kununua makreti ya bia kwenye mabaa mbalimbali na wengine wakiwa eneo la Mlandege walinunua ulanzi na kuanza kunywa kwa kushangilia waziwazi kifo hicho kwa maneno ya shombo huku wakimwaga ofa za bure hata kwa wapita njia!. Kwa hakika, ilikuwa ni hali ya kustaajabisha na kushangaza sana! Kwa wengi, hii ilikuwa ni mara ya kwanza kushuhudia mwanadamu akishangilia kifo cha mwanadamu mwenzake kwa bashasha kiasi hicho.
Hali hiyo ilikuja kutokea tena baada ya kifo cha Rais JUVENAL HABYARIMANA wa Rwanda April 6, 1994. Wanyarwanda 10 waliokuwa wakiishi Mwanza, walishangilia mno na kutoa ofa kedekede za bia kwenye baa walimokuwamo. Watu hao walikamatwa lakini DPP, marehemu KULWA SATO MASSABA, akawafutia kesi (Nolle Prosequi) kwa maelezo kuwa hilo si kosa la jinai.
"Wehu" huo ulijitokeza tena Machi 20, 2021 ambapo wananchi 8 wa Simanjiro nao walikamatwa na polisi kwa kushangilia na kukejeri kifo cha Marehemu Dk. JOHN MAGUFULI, Rais wa Awamu ya Tano, Tanzania lakini nao walikuja kuachiwa baadaye.
21. Kamatakamata Yarindima Iringa
Kufuatia kadhia hiyo ya kushangilia kifo cha RC Dr. KLERUU, kufumba na kufumbua, kamatakamata ya kufa mtu ilirindima usiku huo huo mjini Iringa na kuwakumba watu wengi wakiwemo watu maarufu enzi hizo mkoani humo kama vile SAID MOHAMMED, IBRAHIM KHALIL, PESAMBILI, MURSAL nk.
Waliokamatwa walipelekwa maeneo tofauti nchini mf. Mwanza, Shinyanga na Zanzibar huku ndugu zao wakiwa hawajui walikopelekwa. Sintofahamu hiyo ilipelekea kiza kinene na ndugu hao kukumbwa na simanzi na sonono kubwa !. Bw. MWAMWINDI alipelekwa gerezani la Isanga, Idodomia huku nyumba zake Isimani na Iringa mjini zikilindwa kwa masaa 24.
Bw. AMANI MWAMWINDI, anatujuza zaidi kuhusu kimuhemuhe hicho-:
"Ulikuja mtikisiko mkubwa sana. Wazee wengi maarufu Iringa na wakulima wenzie Mzee kule Isimani walisombwa na vyombo vya usalama".
Nyumba na baadhi ya mali za waliokamatwa zikachukuliwa na hazikurudishwa kitendo kilichopelekea Mzee PESAMBILI kuwa mtu wa huzuni na akawa, kwa miaka mingi baadaye, akiongea mwenyewe barabarani kama mtu aliyedata !.
22. "Wanyalu" Wachanga $ 2,500 Kumtafutia Bw. MWAMWINDI Wakili wa Nje
Baada ya kuona mwenzao MWAMWINDI amekamatwa, wakulima matajiri wa Isimani waliamua kumtafutia wakili. Juhudi za kumpata wakili wa hapa nchini ziligagonga mwamba kutokana na figisufigisu hivyo wakachanga $ 2,500 kwaajili ya kumtafuta wakili toka nje ya nchi ili aje kumtetea.
Wahenga walionena "Serikali ina mkono mrefu" na "Siku ya kufa nyani miti yote huteleza" hawakukosea. Wakati juhudi hizo zinapamba moto, walioshiriki kwenye mchango huo nao walidakwa na kuswekwa lupango!.
23. Mtoto Wa MWAMWINDI Amtembelea Baba Yake Lupango
Kamatakamata iliyotamalaki Iringa ilipelekea kutokea kwa uhasama mkubwa sana kati ya ndugu wa Bw. MWAMWINDI na ndugu wa watu waliokamatwa kwenye papatupapatu hiyo kwani walidai tatizo hilo lilisababishwa na Bw. MWAMWINDI! Hivyo, mwanae, AMANI (akiwa kijana wa miaka (21) tu), akaomba Kibali cha DC wa Iringa na akaweza kwenda kumuona baba yake gerezani na akamuhabarisha yote yaliyokuwa yanayojiri uraiani. Bw. MWAMWINDI alihuzunika sana.
24. Bw. MWAMWINDI Amwandikia Barua Rais NYERERE
Bw. MWAMWINDI akaamua mara moja kumwandikia barua Rais NYERERE na kumueleza kuwa ni yeye ndiye aliyemuua RC Dk. KLERUU hivyo ni vyema wengine waachiwe kwani hawahusiki kwa namna yoyote na kifo hicho.
25. Rais NYERERE Aaamuru Waliotiwa Ndani Wachiwe
Rais NYERERE, siku chache tu baada ya kupokea ombi la Bw. MWAMWINDI, aliamuru kuaachiwa kwa watu wote waliokamatwa kwenye msala huo. Amri hiyo ikatekelezwa mara moja. Hata hivyo, baada tu ya kuachiwa, baadhi yao waliamua kuhama kabisa eneo la Isimani na kuhamia vijiji vingine huku wengine wakihamia mikoa mingine kwani waliona imeishakuwa nuksi kwani togwa liliishaingia nzi!.
26. Kesi ya Bw. MWAMWINDI Yaanza Kurindima Mahakama Kuu
Upelelezi wa kesi hii ulifanywa kwa spidi isiyo ya kawaida na Bw. MWAMWINDI akafikishwa Mahakama Kuu mjini Iringa akikabiliwa na kesi ya "Murder" chini ya Kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu, Sura ya 16. Wananchi lukuki walikuwa wakijitokeza kufuatilia kesi hiyo ya aina yake kila siku. Kesi hiyo ilikuwa mbele ya Mh. Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE wa Nigeria (ambaye alikuwepo nchini toka 1970 hadi 1973).
27. Bw. MWAMWINDI Apelekwa Kortin kama Mfalme
Kutokana na unyeti wa kesi yake, Bw. MWAMWINDI alikuwa akipelekwa kortin na msafara mkubwa wa magari na ulinzi mkali huku wananchi lukuki wakijipanga barabarani kutaka kumuona "Mnyalu" huyo. Kwa hakika, Bw. MWAMWINDI alionekana kama mfalme na siku zote za kesi yake mji ulikuwa ukisimama!.
28. DPP SAMATTA Aendesha Kesi!
Kutokana na unyeti wa kesi hii, aliyekuwa "Director of Public Prosecutions" (DPP) wa wakati huo, BARNABA A. SAMATTA, ndiye aliyekuwa akiiiendesha kesi hii yeye mwenyewe na si wasaidizi wake.
29. RPC Iringa Atoa Ushahidi Upande wa Bw. MWAMWINDI
Moja ya matukio ya kuvutia kwenye kesi hii ilikuwa pale RPC wa Iringa, ABUBAKAR HASSAN, alipotoa ushahidi kwa upande wa mshtakiwa.
RPC huyo alieleza kuwa siku ya tukio hakutaarifiwa kuwa RC Dk. KLERUU alikuwa na safari ya Isimani ndio maana hakumpa "police escort" na hakuwa na taarifa yoyote kuwa marehemu RC Dk. KLERUU angeenda Isimani siku hiyo.
30. Kigogo wa Polisi Aieleza Korti WANYALU sio Watu wa Mchezo!!!
Bw. KHAN LODHI (Regional CID Officer) alitoa ushahidi kama shahidi wa 18 wa Serikali na pia kama shahidi wa 4 wa Utetezi. Katika ushahidi wake, aliieleza mahakama kuwa amefanya kazi kwa miaka mingi maeneo mengi nchini kama vile kwa Wachaga, Wamasai, Wabondei na Wadigo. Alieleza kuwa alibaini kuwa Wanyalu ni tofauti na makabila hayo yote kwani hawanaga simile na huwezi kubaki salama hasa ukiwatukania ndugu zao ambao ni marehemu!.
Maelezo haya pia yaliungwa mkono na RPC ABUBAKAR HASSAN aliyeeleza kuwa kwa uzoefu wake wa miaka 22 alibaini "Mnyalu" ni mtu wa kipekee na si wa kumchezea hovyohovyo kwani "Wanyalu" wako tofauti na makabila mengine!.
31. Bw. MWAMWINDI Ajitetea
Utetezi wa Bw. MWAMWINDI katika kesi hiyo ulikuwa wa aina mbili. Kwanza, alidai kuwa yeye huwa mara nyingine anakuwa na mawenge/waruwaru (insane). Mama yake, Bi ZULA d/o FERUZI, alitinga mahakamani kama shahidi na akatoa ushahidi kuthibitisha kuwa mwaka 1958 ndipo mwanae huyo alipoanza kupata hayo mawenge ambayo hujirudiarudia. Pili, Bw. MWAMWINDI alidai kuwa alikuwa "provoked" (alikasirishwa) na maneno ya shombo yaliyotamkwa kwa kejeri na RC Dr. KLERUU siku ya tukio.
32. DPP Adai Bw. MWAMWINDI Aliua Kwa Kukusudia
DPP alileta mashahidi ili kuthibitisha kuwa Bw. MWAMWINDI aliua kwa kukusudia. Mmoja wa mashahidi wake alikuwa Dk. PENDAEL ambaye alieleza kuwa ingawa ni kweli Bw. MWAMWINDI aliwahi kupata mawenge, lakini wakati akifanya mauaji hayo akili yake ilikuwa iko vizuri na hakuwa na chembe hata moja ya mawenge.
33. Washauri wa Mahakama Watofautiana
Katika kesi za "Murder" ni lazma kuwe na Washauri (Assessors) ambao husikiliza kesi na mwisho humpatia Jaji maoni yao. Jaji ni lazma ayasikilize maoni hayo lakini halazimiki kuyakubali. Katika kesi ya MWAMWINDI kulikuwa na "Assessors" 4. Wawili kati yao walisema MWAMWINDI hakuwa na hatia ya kosa aliloshtakiwa nalo na wawili walitoa maoni kuwa alikuwa na hatia.
34. Hukumu Yasubiriwa kwa Hamu!
Baada ya Pilato, Jaji GABRIEL ONYIUKE, kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili pamoja na maoni ya "Assessors", akapanga Jumatatu ya Octoba 2, 1972 kuwa siku ya hukumu. Kitahanani kikubwa kikaikumba nchi nzima hususani mji wa Iringa. Maofisini, vilabuni, vijiweni, mashuleni nk wananchi wakawa wakitabiri hukumu itakuwaje ambapo kila mmoja alibashiri jinsi alivyoona yeye ni sahihi!.
35. Jaji ONYIUKE "Amnyonga" Bw. MWAMWINDI!
Siku tulivu ya Jumatatu, Octoba 2, 1972, Mahakama Kuu mjini Iringa ilifurika hadi pomoni kuanzia saa 12 asubuhi na viunga vya Mahakama hiyo vilijaa "Wanyalukolo" waliotaka kushuhudia yaliyokuwa yakijiri. Mh. Jaji ONYIUKE alimtia hatiani Bw. MWAMWINDI kwa kosa la mauaji ya kukusudia na akaamuru anyongwe hadi afe. Mh.Jaji aliona kwamba kitendo cha Bw. MWAMWINDI kwenda hadi nyumbani kuchukua bunduki kiliakisi dhamira ovu, hivyo alifanya kitendo hicho kwa kukusudia.
36. Bw. MWAMWINDI Anyongwa "Fastafasta"
Kesi hii ilichukua takriban miezi 10 tu kwa upelelezi kukamilika, ushahidi kutolewa na hukumu kusomwa! (Desemba 1971 - Octoba 1972)!.
Rais NYERERE, mara tu baada ya hukumu hiyo, alitia saini mara moja Hati ya kunyongwa kwa Bw. MWAMWINDI. Bw. MWAMWINDI alinyongwa hata kabla ya kesi yake kusikilizwa na Mahakama ya Rufaa kama ilivyo kawaida na hivyo huo ndio ukawa ndio mwisho wa maisha yake hapa duniani!.
37. Rais NYERERE Alihofia RCs Wangevunjika Mioyo
Moja ya sababu kubwa zilizozopelekea Rais NYERERE kuchukua uamuzi huo wa kutia saini Hati hiyo haraka ni kuogopa RCs wangevunjika mioyo baada ya kuona mwenzao akiuawa kinyama.
38. Rais NYERERE Aliidhinisha Kunyongwa Watu Wangapi Wakati wa Utawala Wake?
Kwa mujibu wa Kifungu cha 3 cha "Presidential Affairs Act, Cap. 9" , mtu aliyehukumiwa na mahakama kunyongwa hawezi kunyongwa hadi Rais wa nchi aidhinishe kwa kusaini Hati Maalum baada ya kupokea ushauri wa Kamati Maalum. Kwa miaka mingi, watu wengi wamekuwa wakijiuliza kama Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, aliwahi kuidhinisha mtu yeyote anyongwe akiwa madarakani hadi alipong'atuka Novemba 5, 1985. Wapo waliodai kuwa Baba wa Taifa aliidhinisha watu 1,000 wanyongwe, wapo waliodai aliidhinisha watu 100, wapo waliodai aliidhinisha watu 2 na pia wapo waliodai kuwa hakuwahi kuidhinisha kunyongwa hata mtu mmoja.
Kitendawili hiki kilipatiwa jibu mujarab lilitolewa bungeni Januari 30, 2008 ambapo Mh. MATHIAS CHIKAWE, aliyekuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, alilijuza Bunge-:
"Mh. Spika, toka nchi yetu ipate uhuru, jumla ya watu 82 wamenyongwa kuanzia awamu ya kwanza. Kati ya watu hao, 10 walinyongwa wakati wa awamu ya kwanza na 72 wakati wa awamu ya pili. Hakuna mtu aliyenyongwa kwenye awamu ya tatu na ya nne".
Aidha, Mh. KHAMIS KAGASHEKI, alipokuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, alitoa jibu Bungeni, Octoba 31, 2008, ambalo halikutofautiana na la Mh. CHIKAWE:
"Mh. Naibu Spika, amri ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa mara ya mwisho ilitolewa mwaka 1994".
Ukimuacha SAID MWAMWINDI, mtu mwingine maarufu ambaye ni mmoja wa watu 10 ambao Mwalimu JK NYERERE aliidhinisha wanyongwe ni Mhindi mmoja ambaye alikuwa akiua wake zake kwa kupindua gari ili alipwe bima!.
Suala la ma-Rais wa hivi karibuni kutotekeleza adhabu ya kunyongwa pia limeelezewa na Bw. SIJALI KOJHO, mfungwa aliyeachiliwa na Rais SAMIA SULUHU HASSAN Desemba 9, 2021 ambaye alihukumiwa kunyongwa takriban miongo mitatu iliyopita. Akihojiwa na "Zamaradi Tv" alinena-;
"Wapo washtakiwa wengi walihukumiwa kunyongwa nikiwemo mimi ingawa mimi mwaka 1999 nilibadilishiwa adhabu kutoka kunyongwa na kuwa kifungo cha maisha. Sijawahi kuona mtu yeyote akinyongwa".
Rais wa Awamu ya Tatu, Mh. BENJAMIN WILLIAM MKAPA, aliyeongoza nchi toka mwaka 1995 hadi mwaka 2005, ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza Tanzania "kutonyonga" mtu yeyote. Baada ya Mh. MKAPA, marais wengine nao walimuiga kwani nao "hawakumnyonga" mtu yeyote hadi hivi leo.
39. Je, Unyongaji Watu Waliohukumiwa Kunyongwa Hufanyikaje?
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza jinsi adhabu hii ya kunyonga inavyotekelezwa.
Mwaka 1984, waliajiriwa watu 2 kufanya kazi za kunyonga nchi nzima. Mmoja wa "Nyonganyonga" hao (Jina limehifadhiwa), aliyestaafu mwaka 2006, alielezea kinagaubaga kinachojiri kwenye shughuli hiyo pevu, alipoongea na Mwananchi, Agosti 21, 2016-:
"Nimefanya kazi hii ya kunyonga kwa miaka 22. Hakuna bingwa wa kunyonga nchi hii kama mimi. Tulikuwa wawili na tuliajiriwa mwaka 1984. Siku ya kwanza kunyonga nilipata shida sana na sikuweza kulala. Niliweweseka sana na nikapiga kelele hadi mke wangu akaamka niliona wale niliowanyonga wananikimbiza na mashoka!. Baadae nikazoea. Kabla ya kunyonga, Viongozi wa dini huja kuwaongoza kwa sala ya toba. Usiku kabla ya kunyonga tulikuwa tunapewa bia, mimi nikipendelea Safari lager. Tulikuwa tukipewa kreti zima. Bia zilitupa ujasiri kwani tulikuwa tukigida hadi asubuhi. Kitanzi ni kamba inayoning'inizwa ambapo mhusika hufungwa kitambaa cheusi usoni. Mimi naingiza kitanzi shingoni na ubao unakuwa umeegeshwa na kazi yangu ni kufyatua kitufe mf wa gia ya gari. Kikifyatuka humfanya mtu huyo kuning'inia na hapo kitanzi humkaba. Nikihakikisha amekufa naondoka. Askari wanakuja na kuiondoa maiti na kwenda kuizika kwa msaada wa wafungwa wachache. Nduguze huwa hawahusishwi. Baada ya hapo nashtakiwa Mahakamani (tunakuwa peke yetu) kwa mauaji na najitetea. Ni utaratibu tu wa kisheria kwani sichukuliwi hatua yoyote bali naendelea na kazi!".
40. Familia ya RC Dk. KLERUU Yarejea Kilimanjaro
Marehemu RC Dk. KLERUU aliacha mke na watoto 4 (EVA, ANDREW, CARMEN & EDWIN). Baada ya kifo hicho, familia ya marehemu Dk. KLERUU ilirejea nyumbani Kilimanjaro.
41. Serikali Yawasomesha Watoto wa Dk. KLERUU Mamtoni
Rais NYERERE alihuzunishwa sana na mauaji ya RC Dk. KLERUU. Hivyo alisaidia wanawe kusoma Bulgaria na Urusi. Viongozi wengine nao walikuwa karibu sana na mjane na watoto hao mfano ABEID KARUME, ABDOU JUMBE, RASHID KAWAWA & GETRUDE MONGELLA.
"Mzee wa Atikali" alikuwa kombania moja ya "Danger Coy" huko Mafinga JKT na Bw. EDWIN aliyekuwa kijana nadhifu na msomi wa hali ya juu.
42. Rais NYERERE Ateua RC Mpya
Baada ya kuuawa kwa RC Dk. KLERUU, Rais NYERERE alimteua Mh. MOHAMED KISSOKY kuwa RC mpya wa Iringa.
43. MBARAKA MWINSHEHE Amtungia Wimbo Dk. KLERUU
MBARAKA MWISHEHE, mwimbaji Bora kabisa kuwahi kutokea nchini, alimtungia Dk. KLERUU wimbo mujarab uliovuma sana enzi hizo "Dk. KLERUU: SHUJAA & MWANAMAPINDUZI".
44. Maandamano Kulaani Mauaji ya Dk. KLERUU Yasambaratika
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu, Iringa walifanya maandamano ya kulaani mauaji ya Mjamaa, Dk. KLERUU. Hata hivyo, maandamano hayo yalisambaratika baada ya "Wanyalu" kutaka kuwafurumua kwa mawe na nyengo wanafunzi hao wa ualimu hivyo kila mmoja akachukua hamsini zake kwa kasi ya ajabu ambapo hata USAIN BOLT angesubiri!.
45. Maoni kuhusu Mauaji ya Dk. KLERUU
Kila mmoja alikuwa na maoni yake kuhusu tukio la mauaji ya Dk. KLERUU. Mh. JOSEPH LYATA (aliyekuwa Naibu Meya wa Iringa mjini hivi karibuni) ametanabaisha maoni yake-:
"Dk. Kleruu alitaka wakulima wafuate anayotaka yeye, hakutaka kujipa fursa ya kujifunza mila na desturi za Wahehe kwa sababu angelijua asingeenda shambani kwa mkulima peke yake. Kulikuwa na kila sababu kuwashirikisha wananchi. Ukiwa Kiongozi jifunze kusikiliza usijifanye mtwana na kujiona wewe ni zaidi ya unaowaongoza".
Binti wa kwanza wa Dk.KLERUU, Bi EVA(60) nae almetoa yake ya moyoni-:
"Baba alikuwa muumini wa siasa ya ujamaa aliyesimamia sera za ujamaa. Serikali ilikuwa inahimiza vijiji vya ujamaa ili wananchi washiriki pamoja kwenye kilimo cha kufa na kupona. Baba alikuwa akifuatilia kwa kina maagizo ya Rais Nyerere. Hiki ndicho kilichosababisha kuuawa akiamini alichosimamia kilikuwa sahihi. Serikali haikutaka ukiritimba wa ubepari wa mtu mmoja kumiliki eneo kubwa jambo ambalo watu wasiopenda maendeleo hawakulipenda".
46. RCs waikwepa Nyumba ya RC Dk. KLERUU
Kutokana na jinsi Dk. KLERUU alivyoaga dunia, nyumba yake ilisusiwa na RCs wengine waliomfuata kwa kuwa "wanaogopa kutokewa na SAID MWAMWINDI usiku akiwakimbiza kwa bunduki"! Nyumba hiyo, ambayo ilikuwa ni Ikulu ndogo iliyojengwa na Mjerumani mwaka 1906, sasa ni gofu lililozingirwa na majani marefu!.
47. Familia ya Dk. KLERUU na ya Bw. MWAMWINDI Zamaliza Tofauti Zao
Mwezi Machi 2014, Bi. EVA (60), mtoto wa kwanza wa Dk. KLERUU na Bw. AMANI MWAMWINDI (67), mtoto wa kwanza wa MWAMWINDI, walikutana kwaajili ya maridhiano. Wawili hao walipiga picha kwa bashasha katika ofisi ya Bw. AMANI ie Mstahiki Meya wa Iringa mjini yalikofikiwa maridhiano hayo.
Bi. EVA, huku akububujikwa machozi alinena-:
"Tukio la mauaji ya 1971 lilifanya familia iogope kuja Iringa. Hata hivyo, niliweka nadhiri ya kufika kuona mahali baba yangu alipouawa. Hatimaye leo nimefika na pia nimeonana na Amani, mtoto wa Mwamwindi, na tumefanya maridhiano".
Naye Meya AMANI, alitiririka-:
"Ninayo furaha kukutana na dada yangu Eva na kuondoa tofauti zetu. Ni jambo la kumshukuru Mungu".
48. Chuo cha Ualimu chapewa jina la Dk. KLERUU
Ili kukumbuka na kuenzi mchango wa marehemu RC Dk. KLERUU, chuo cha ualimu mkoani Iringa kilipewa jina lake "Dr. KLERUU Teachers Training College".
49. MNARA wa Dk. KLERUU Wajengwa "Mji" wa Bw. MWAMWINDI
Mnara wa kumbukumbu ya mauaji ya RC Dk. KLERUU ulijengwa kwenye "mji" wa Bw. MWAMWINDI sehemu ambayo RC huyo alimiminiwa risasi ikiwa ni ukumbusho wa tukio hilo la kihistoria.
50. TAMATI
Jumamosi mujarab ya leo, Desemba 25, 2021, imetimia miaka 50 toka "Mnyalukolo" SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI amuue kwa risasi RC Dk. WILBERT ANDREW KLERUU, siku ya Jumamosi Desemba 25, 1971. Hili ni tukio la kihistoria ambalo lina mafunzo kedekede. Ni vyema sote tukajifunza.
ATIKALI hii imeambatisha picha zifuatazo-
1. "Mnyalu" Bw. MWAMWINDI akiwa anatoka Mahakamani
2. Mnara Isimani;
3. Eva & Amani;
4. Nyumba ya RC Dk. KLERUU, Iringa; na
5. Amani Mwamwindi alipokuwa Meya wa Iringa
Wajukuu wa huyo RC?Huu ukoo,wajukuu wako block41 kinondoni
Wana asili ya utata sana,naona hiyo ni nature yao[emoji23][emoji23]
Ova
Si unaona hapo Kati ya vijiji 2000 vya ujamaa,750 ni mtwara tu peke yake,akapelekwa kwa kina mwamindiKivipi? Tupe mifano.
Ahsante sana kwa historia hii!1. Usuli

Jumamosi mujarab ya leo, Desemba 25, 2021, imetimia miaka 50 toka "Mnyalukolo" ss ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI amuue kwa risasi RC Dk. WILBERT ANDREW KLERUU, siku ya Jumamosi Desemba 25, 1971. Hili ni tukio la kihistoria ambalo lina mafunzo kedekede. Ni vyema sote tukajifunza.
ATIKALI hii imeambatisha picha zifuatazo-
1. "Mnyalu" Bw. MWAMWINDI akiwa anatoka Mahakamani
2. Mnara Isimani;
3. Eva & Amani;
4. Nyumba ya RC Dk. KLERUU, Iringa; na
5. Amani Mwamwindi alipokuwa Meya wa Iringa
Picha hazionekani mkuu1. Usuli

Hamza je?Shukrani. Mwamwindi na zakaria ni mashujaa wangu
Mzee Ibrahim Khalil(marehemu), alihamia Temeke Dar akiwa na matrekta yake! Serikali ya Nyerere haikujali kilimo japo ilipenda kujionesha inakipenda kilimo. Kleruu alisambaratisha kilimo cha mahindi Isimani Iringa akasingizia vita ya Uganda!1. Usuli

Ditopile yeye alimuua dereva daladala, nae tumuweke kwenye kundi la mashujaa?Mpaka hapo namuona Mwamwindi kama shujaa wangu wa muda wote. Hakupenda kudhalilishwa na kuonewa. Na imetuchukua miaka 50 kumpata shujaa mwingine Hamza. Mwenyezi Mungu awape pumziko jema walikuwa wanaume majabali kwelikweli.
Ditopile kiburi cha madaraka hapo hakuna ushuja wowote. Pia tukio Mwamwindi huwezi kulilinganisha na la Ditopile ni scenario mbili tofauti.Ditopile yeye alimuua dereva daladala, nae tumuweke kwenye kundi la mashujaa?