Kumbukizi ya miaka 59 toka Said Mwamwindi amuue RC Dkt. Kleruu siku kama ya leo mwaka 1971

Mwambieni Kikwete hii kitu inaenda kutokea very soon huko Ndundu na Malamba, Mbeya

Ujamaa ni uchawi wa maendeleo kwa wananchi, haiwezekani leo hii mnakuja kutupora zaidi ya hekari 500 kiholela kwa ajili ya ujenzi wa chuo, ina maana Tanzania ardhi haina thamani?

Hii nchi naichukia kinoma!
 
Hapana. Ni tofauti kama mbingu na ardhi. Dr Kleruu alikuwa muumini wa ujamaa na aliuawa kwa kusimamia alichokiamini. Makonda na Sabaya hawa ni opportunists, wanafiki, wanasio na imani yoyote bali kujikweza na kujinufaisha wao.
Mie nazungumzia tabia, alichokifanya ni kama makonda kuvamia clouds, huwezi kwenda kumkejeli mtu namna ile, wote ni wale wale tu.
 
Hata Mimi nilisikia kama wewe mkuu lkn kwasababu sina uhakika wa asilimia hata 50 ndy maana sijauweka hapa
 
Huyo RC alikua mkuda sana namfata mtu kwake afu anamwita mbwa mi mwenyewe nakumwaga mavi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na nimchawi wa kufa mtu, pale mpaka akuendorse mwenyewe kama ilivyo kwa wale wa kongwa
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mie nazungumzia tabia, alichokifanya ni kama makonda kuvamia clouds, huwezi kwenda kumkejeli mtu namna ile, wote ni wale wale tu.
Ndiyo nikakuambia siyo ''wale wale''. Wote walifanya ubaya lakini kwa malengo tofauti.
 
Hili lipo na linatokana na Kleruu mkristu mlutheri mchaga wa Mwika Marangu aliwezaje kuipa kisogo siku ya Krisimasi huku familia yake ikiandaa mapochopocho ya sikukuu! Mkewe na watoto hawakujua baba ameenda wapi, hakuaga na hakutaka ulinzi japokuwa miaka hiyo hawakuwa na ulinzi wa maana.
Nirudi kwa mzee Kisoky aliyetoka kwenye udc, huyu na alifanya alichofanya Mwamwindi, alimpiga risasi na kumuua mkewe dogodogo ukiacha mke wa kwanza, hakuchukuliwa hatua yoyote.
Mhindi wa bima, huyu alimuua mkewe akamuweka ndani ya gari na kuiporomosha kwenye milima ya Likumburu*(sic), jina nimelihifadhi.
 
Aisee!!! Ushahidi wa kimazingira unafanya fununu hizi ziendelee kupata nguvu. Naona hata aliyekua RPC baada ya kutoa ushahidi kama shahidi wa Jamhuri alirudi tena mahakamani kua shahidi wa utetezi

Kikubwa alichokisema ni kwamba alishangaa kusikia RC akiwa ametoka kwenda kwenye majukumu ya "kiserikali" bila ya yeye kupewa taarifa na ikiwezekana atoe ulinzi stahiki

Hata kitendo cha Mh. RC kuendesha gari yeye mwenyewe bila ya dereva na kwenda kwenye shughuli za serikali ni jambo la kushangaza sana!
Hatuna hakika na hili lakini hakuna dharau mbaya kama mtu kukuchapia mkeo ukawa unajua na halafu huyo mtu akuletee dharau na ubabe!

Kama jambo hilo ni kweli lilikuwepo basi itakua ni siri ambayo wote wawili, yaani Mzee Said Mwamwindi na RC Dr Kleruu hawakutaka tuijue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…