The BornAgain
JF-Expert Member
- Jun 23, 2024
- 428
- 582
Kweli..majina nickname sio ishu..ila ya ukoo..fikiria jina lenu la ukoo kuna mtu anaanza kulitumia wakat hana hata undugu nanyiUmeelewa alichokisema?hebu soma tena utaelewa,hajazungumzia majina ya bandia amezungumzia jina halisi la ukoo
Ndiyo mjue tunaongozwa na matapeli tupuJina na viongozi kukata mawasiliano.
Hii ya pili kwenye mzani ni nzito kuliko hiyo ya kwanza.
Kwanini usitumie jina la ukoo wako?Kwani hilo jina wana hati miliki.kuna watu wanaitwa hadi Yesu au Mohamed nini Nyerere.
Pia wanachanganya baba wa Taifa na baba yao.
Baba wa Taifa ni Mali ya Taifa sio Mali ya Familia.
Exactly 💯...Mtu kama unafanya mambo mazuri katika jamii sidhani wahusika wataona aibu ukijihusisha na ubini wao.
Sasa bwana Steve naona hujakubalika na wahusika wa jina la Nyerere.
Jichunguze kuna kitu unakifanya wazi wazi au sirini hakina sifa nzuri kwa jamii.
Nilitegemea hoja hii kutoka familia ya mwalimu nyerere siku nyingi ila kwa ustaarabu wao wamevumilia muda mrefu. Wasanii kujiita jina la nyerere eti kwa kuigiza sauti yake tu sio sahihi kabisa. Stephen Mengele amesikia asite mara moja kujiita Stephen Nyerere. waandishi wa habari mumesikia. Baadhi ya wasanii wana maadili mabaya wengine wameshiriki dili za ovyo kama huyu Mengele kutetea kuuza bandari za taifa kwa dubai. Unakuta anashambuliwa jina linatajwa stephen nyerere. Mtu wa ovyo anaitwa Nyerere kwa vile tu anajua kuigiza sauti yake. Hakika haipendezi.Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.
Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.
Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.
Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.
Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.
Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.
Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.
USSR
Kwani wao ni wamiliki wa lugha iliyotumika kutengeneza hilo jina? UKIULIZWA LEO NYERERE lina maana gani na ukapata jibu labda ukute linamaana ya msimu wa mvua. Sasa msimu wa mvua kuitwa kwa kizanaki halafu ndio utune na kusema hilo jina ni miliki yenu? HUO NI UBINAFSIKweli..majina nickname sio ishu..ila ya ukoo..fikiria jina lenu la ukoo kuna mtu anaanza kulitumia wakat hana hata undugu nanyi
🤣🤣🤣Pia wanachanganya baba wa Taifa na baba yao.
Baba wa Taifa ni Mali ya Taifa sio Mali ya Familia.
Ujinga tu , nchi zilizoendelea hayo majina ya watu yanatumika sana na akuna tatizo tz sijui uwa Kuna nn
Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.
Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.
Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.
Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.
Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.
Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.
Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.
USSR
Kila ukoo ujitahidi kutoka kimaisha ili ujivunie ubini waoMtu kama unafanya mambo mazuri katika jamii sidhani wahusika wataona aibu ukijihusisha na ubini wao
hakulelewa kuzima simu na kutokuwasikiliza viongozi wa nchi nduguEti watu wangine wanakuja hapa ila wakishaondoka hawapokei simu Tena na wanapotea..... Kwenye haya maisha usijipe umuhumu kwenye maisha ya watu Wala usitake kupendwa... Hapa huyu Madaraka alitaka tu kutoa hisia zake kwamba hawathaminiki na hawapewi kipaumbele familia yao especially yeye, ningekua yeye ikifika Nyerere day nazima simu na sipatikani ili wasinizoee tena.
Kutumia jina Nyerere ni jina kama majina mengine Kila mtu ana haki ya kuitwa au kujiita... Mohammed, Mwakyambiki, Yesu, Mkapa, Obote, Kassim yote hayo ni majina unajichagulia unalotaka,, Hata huyo Nyerere baba ake kuna watu waliitwa Nyerere kabla yake...