Kumbukizi ya Nyerere: Familia ya Mwalimu Nyerere yawataka wasanii kuacha kutumia jina la Baba wa Taifa kama ubin wao

Kumbukizi ya Nyerere: Familia ya Mwalimu Nyerere yawataka wasanii kuacha kutumia jina la Baba wa Taifa kama ubin wao

Kuna watu wanaitwa akina Pili Magufuli, ...trump, ....biden nk. Na wala sio watoto wao wala hawana vinasaba.
Kuitwa jina la kiongozi fulani ni heshima kwa hao viongozi.
 

Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.

Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.

Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.

Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.

Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.

Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.

Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.

USSR
Kweli ni kosa kisheria kutumia jina la mtu pasipo na izini
 
Kabisa atunze heshima ya mwalimu, kwa nini usitumie

jina la ukoo wako, yani haoni fahari ya ukoo wake? Kwa nini?
 
Kila ukoo ujitahidi kutoka kimaisha ili ujivunie ubini wao

Ubini wa Huyo Steve wa Mengele ni maskini wa kutupwa ndio maana kaamua akimbie huo ubini atumie ubini wa watu ubini wa Nyerere

Ukoo wa Mengele mkae chini mjitathimini kumaliza tatizo la ulofa kwenye ukoo wa Mengele ili watoto na wajukuu na vitukuu wajisikie fanatic kutumia jins la ubini ls Mengele badala ya kulikimbia na kwenda kuokota majina ya ubini ya watu sababu anaona jina la ubini la baba yake halina maana yoyote zaidi ya ulofa

Kaeni kikao mjadiliane hilo
Ni aibu kufikia wenye jina wanakuambia uache kulitumia.
 
Madaraka labda hajui kuwa Tanzania hakuna jina linalozuiwa mtu kujiita.

Mimi naweza kuamua kujiita Jitu Jiwe kama (Given names) si lazima Jiwe liwe ni surname.

Sasa Steve Nyerere kaamua kujiita Steve Nyerere kwa nini hutaki ajiite anavyotaka yeye?

Hakuna mahali Steve Nyerere kajiita mtoto wa Nyerere
 
Nyerere alikosea sana kuto wasomesha watoto.

Mtu kuchagua jina si ni jambo la hiyari yake ?

Kwani Nyerere wa kwanza ni huyo baba yao?

Kwani kila Nyerere ni Kambarage ?

Hakuna hatia miliki ya Jina, watu wanaojiita Yesu sembuse Nyerere.

Maendeleo hayana Chama.
Ukiona amekosea kulilinda jina la babake kutumika kiholela na kuwa hana haki hiyo basi nawe badili jina la babako kisha itangazie jamii kuwa wewe hutotumia jina la babako mzazi uuone mtoto wa wanaukoo!
 
Eti watu wangine wanakuja hapa ila wakishaondoka hawapokei simu Tena na wanapotea..... Kwenye haya maisha usijipe umuhumu kwenye maisha ya watu Wala usitake kupendwa... Hapa huyu Madaraka alitaka tu kutoa hisia zake kwamba hawathaminiki na hawapewi kipaumbele familia yao especially yeye, ningekua yeye ikifika Nyerere day nazima simu na sipatikani ili wasinizoee tena.

Kutumia jina Nyerere ni jina kama majina mengine Kila mtu ana haki ya kuitwa au kujiita... Mohammed, Mwakyambiki, Yesu, Mkapa, Obote, Kassim yote hayo ni majina unajichagulia unalotaka,, Hata huyo Nyerere baba ake kuna watu waliitwa Nyerere kabla yake...
Ujumbe wako umefika kesho simu haipatikani kuanzia Asubuhi mpaka jioni mpaka waje na land rover za Arusha 😁
 
Hivi unajua hata hiyo Elsa Marie ni jina la mtu huko liliko toka
Inawezekana.
Lakini huyu steve mangere sijui steve nani alianza kutumia jina la nyerere wakati anafanya usanii wa kuigiza sauti ya nyerere. Hata sasa akiongea anajifanya anaongea kama mwalimu nyerere.
Pia kawarithisha watoto wake nao pia wanatumia ubini wa nyerere kwenye mitandao ya kijamii.
 
Inawezekana.
Lakini huyu steve mangere sijui steve nani alianza kutumia jina la nyerere wakati anafanya usanii wa kuigiza sauti ya nyerere. Hata sasa akiongea anajifanya anaongea kama mwalimu nyerere.
Pia kawarithisha watoto wake nao pia wanatumia ubini wa nyerere kwenye mitandao ya kijamii.
Hujawahi kuona watu wenye ukoo tofauti lakn wana majina yanafanana kama Massawe Mushi etc
 
Back
Top Bottom