Kumbukumbu katika picha ya shambulizi baya la kigaidi septemba mwaka 2001 kwenye majengo ya world trade center huko marekani

Kumbukumbu katika picha ya shambulizi baya la kigaidi septemba mwaka 2001 kwenye majengo ya world trade center huko marekani

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Tunaingia mwezi wa 9 ambapo kumbukumbu za shambulizi la kigaidi huko marekani zitafanyika huko manhattan kwenye zero ground. Nikaona sio mbaya kuleta picha na kumbukumbu mbalimbali za tukio hilo tujikumbushe kidogo.
FB_IMG_1756645175278.jpg

Sehemu ya upande wa kaskazini mwa jengo la WTC muda mfupi baada ya ndege aina ya Boeing 767-200 ilipobamizwa na magaidi kati ya floor ya 93 na ya 99. Ukitazama vizuri picha hii watu wanapambana kujiokoa ... wengi wao walikufa kwa kuruka au kufukiwa na vifusi vya jengo hilo baada ya kuporomoka..
 
Afisa wa polisi Mike brennan pamoja na mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Beverly wakiwa wamechafuka kwa vumbi pamoja na moshi muda mfupi tu baada ya jengo mojawapo la WTC kuporomoka.
FB_IMG_1756646378752.jpg
 
Aliyebebwa hapa ni mtumishi wa mungu Rev. Maychal . F. Judge ambaye alikuwa ni chaplain kutoka idara ya zimamoto ya mji wa Newyork . Hapa alikuwa ameangukiwa na vipande vya jengo mojawapo lililoporomoka la WTC. Alifika hapa kuwafanyia maombi ya mwisho maafisa wa zimamoto waliokuwa kwenye eneo hili kabla ya kuingia kufanya uokozi.. lakini kama isivyo bahati akaangukiwa na baadhi ya mabaki ya jengo hili la wtc September 11 2001.
FB_IMG_1756646853713.jpg
 
Majira ya saa tatu na dakika tatu asubuhi ya September 11 ,2001 ndege aina ya boeing 767 iliyokuwa na safari na.175 ikiwa inaelekea kwenda kujibamiza kwenye jengo la kusini la WTC kwa spidi ya 800km/Hr kati ya floor ya 77 na 85 . inakadiriwa ndege hii ilikuwa imebeba mafuta gallon 9,100 ambayo ni sawa la lita 34,000 aina ya Jet A-1
FB_IMG_1756647669874.jpg
 
Moshi mzito ukitambaa sehemu ya juu ya jengo la Wtc baada ya ndege yenye safari namba 11 ilipobamizwa na magaidi
FB_IMG_1756648117995.jpg
 
Picha hii ilipigwa kwenye daraja la lililopo bay Ridge brooklyn hapo Newyork muda mfupi baada ya Jengo la north tower kuwaka moto mud mfupi baada ya ndege ya flight 11 kujibamiza.
FB_IMG_1756648304653.jpg
 
Picha hii inaaminika ikimuonesha mrembo edna cintron akipunga mkono kama ishara ya kuomba msaada baada ya jengo hilo kulipuliwa September 11 2001.
FB_IMG_1756648740684.jpg
 
Back
Top Bottom