Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kasella Bantu ndio huyo?
 
Porojo jazz band zimeanza cha uzuri huyo Sykes alikuwa mkristo aliingia Uislam sababu ya Mwanamke tu na si vingine..
 
 
Kasella Bantu ndio huyo?View attachment 553050
Duduwasha,
Kasella Bantu ni huyu hapa chini kama nilivyomwandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Kasella Bantu, yeye alisoma Afrika Kusini kwa hivyo alishuhudia utawala wa mabavu wa weupe na ubaguzi wa rangi. Kasella Bantu alikuwa akiwasema sana Waingereza. Alipokuwa Afrika ya Kusini alizozana na Mzungu mmoja, Hugh Tracey. Tracey aliandika ripoti ya siri kwa utawala wa kikoloni dhidi ya Bantu. Alipokuwa akifanya kazi Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) Shirika la Utangazaji Tanganyika, Bantu kwa mara nyingine tena alizozana na ofisa mmoja Mzungu. Kisa cha ugomvi ni kuwa yule Mzungu aliwaita Waafrika ‘’wapumbavu.’’ TBC ilikuwa chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii. Kesi ya Bantu ilipoletwa mbele ya Kamishna wa Maendeleo ya Jamii, Kamishna alirejelea ripoti ya awali kuhusu tabia ya Bantu iliyoandikwa na Tracey nchini Afrika ya Kusini. Kamishina yule alifikia uamuzi kuwa Bantu alikuwa mkorofi na akamfuta kazi.''
 
kwann us na sio saudia iran kuwait yemen syria nk
Mtanganyika...
Nakuwekea hapo chini nchi ambazo nimefika na nimejifunza mengi katika nchi hizo:

Zambia, Ethiopia, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey, Abu Dhabi, Uingereza, Afrika ya Kusini, Ujerumani, Nigeria na United States of America.
 
I thought hiyo dictionary imechapishwa miaka ya sitini kumbe 2011 means wanaweza kuwa wamelishwa na ukanjanja wako zaidi ya fact...
 
I thought hiyo dictionary imechapishwa miaka ya sitini kumbe 2011 means wanaweza kuwa wamelishwa na ukanjanja wako zaidi ya fact...
Duduwasha,
Dictionary of African Biography (DAB) ulikuwa mradi wa Oxford University Press,
New York na Harvard University chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong.

Uliwajumuisha wanahistoria zaidi ya 500 ulimwenguni.

Lakini kabla ya mimi kuwa katika mradi huu nilikuwa katika mradi mwingine wa
Qxford University Press, Nairobi na walichapa kitabu changu kimoja, ''The Torch
on Kilimanjaro.''

 
Hongera sana ndugu
 
Mkuu Mohamed Said
Humu vijana wengi na mbao za kuwasomeshea wengine endelea kuwatumia kwa hekma na busara mara dufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi mzee Mohamed Said msamehe mtoto mdogo sana huyu..!

Sent by Ubavu
 
Allah amewakataza Waislam kuwatukania watu miungu yao
wasije wakamtukana mungu wa kweli.
Ungelitambua hilo usingetembea dunia nzima ukiwatukana... Hivi Kleist Sykes asingebadili dini yake ya ukristu kisa mwanamke akawa muislamu leo ungemlilia kila kona ya ulimwengu? Mbona Cecil Matola humsemi wala kumuenzi zaidi ya kumfifisha ilihali yeye ndie mwasisi wa vyama Tanganyika?
 
Yericko hujui kitu katika historia hii wewe unajisemea tu.

Sykes Mbuwane kaingia Tanganyika akiwa Muislam na alikuwa na nduguye kipofu wamekuja pamoja anaitwa Ali Katini.

Ramadhani Mashado Plantan kaingia Tangnayika 1905 akiwa na umri wa miaka 5 akiwa Muislam.

Hakika nahadhiri kwingi duniani na nashirikishwa katika miradi ya historia ya Afrika kwa kupewa mialiko.

Ningekuwa natukana hakuna chuo wala taasisi kingenipa heshima wala wasingechapa vitabu vyangu.

Bado nakusisitizia usome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
historia unaipotosha kwa ufia dini wako!
ww mwanazuon wa madrasa dini itakuua kihoro,wacha porojo za vijiweni kwenye kahawa wacha "usomi mwanasesere"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…