Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kabla ya kuingiliana na Waarabu, hao Wamanyema walikuwa wanazungumza lugha gani?Nguruvi mimi nazungumzia historia ya karibuni ya kuingia Wamanyema Tanganyika wakija huku wakiwa kwanza Waislamu na lugha yao Kiswahili. Hiki Kiswahili wamekipata katika kuingiliana na Waarabu. Wamanyema wakakichukua Kiswahili kama lugha yao na huo Ulungwana maana yake ni Uungwana yaani yeye kastaarabika ni Muislam.
OK kwahiyo kuna lugha ya Kimanyema
Kabla sijatoka umenijibu. Mohamed ni kweli hujui tofauti ya vitu hivyo?Hili la Arabic na Qur'an sijui tofauti yake.
Dah habar kubwa sheikh. Ina maana hakuna mahusiano yoyote kati ya Quran na Arabic?Tafsiri ya Qur'an nimesoma na ikisomwa nami nasikiliza nafahamu maana yake lakini siwezi kuzungumza lugha. Swali hilo lako aliniuliza mwalimu wangu mmoja Arab Maratime Transport Academy Alexandria, Egypt baada ya sala ya Ijumaa, akaniuliza kama nimeelewa khutba. Nikamjibu ndiyo. Akashangaa vipi nitaelewa khutba ilhali sijui Kiarabu?
Hakuna kosa wewe kutojua kimanyema. Swali la msingi ni kuwa kabla ya Wamanyema hawajaingiliana na Waarabu na kupata lugha ya kilungwana, walikuwa wanazungumza lugha gani.Mimi ni kizazi cha tatu Mmanyema kuzaliwa Tanganyika hata bibi yangu mkuu nimemuwahi hakuwa anazungumza Kimanyema. Yeye alikuja kutoka Kongo
Hard copy[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]Uko serious? kama kiingereza hamkimudu tumieni kiswahili. Pia hii ungepeleka Jukwaa la biashara au historia.
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
Ah Mohamed, kama utamaduni wako ni ule wa Nabii Ibrahimu hakuna shakaNgruvi3,
Mimi utamaduni wangu ni mila ya Nabii Ibrahim.
Inaanzalna Qur'an Arabiyya...Qur'an imeshushwa katika lugha ya Kiarabu.
Nguruvi3,Ah Mohamed, kama utamaduni wako ni ule wa Nabii Ibrahimu hakuna shaka
Tatizo linajitokeza kwa ukweli kuwa LUGHA hubeba utamaduni wa jamii husika.
Ni ukweli usiopingika popote pale duniani
Sasa Arabic umesema huwezi kuzungumza, na hiyo ndiyo imebeba utamaduni. Huoni tatizo hapo?
Kwa mantiki hiyo ukielewa Quran kwa kuisoma na kuieleza moja kwa moja unaongea Kiarabu.Inaanzalna Qur'an Arabiyya...Qur'an imeshushwa katika lugha ya Kiarabu
Nguruvi3,Kwa mantiki hiyo ukielewa Quran kwa kuisoma na kuieleza moja kwa moja unaongea Kiarabu.
Kiarabu ni lugha imetumiwa kama 'vehicle' ya contents ndani ya Quran.
Huwezi kuzielewa contents kama huelewi zimebebwa kwa 'vehicle' gani
Unachojaribu kukwepa ni kusema 'unaongea kiarabu' kama lugha kukwepa fedheha ya Kimanyema kama lugha mama
Pili, unaposema Kiswahili ni lugha ya Quran kuna walakini.
Waliopokea Uislam ni watu wa Pwani kwasababu za usafiri zilizoleta wageni kwa bahari
Kiswahili kilikuwepo bali ujio wa dini uliimarisha na kutumika kama lugha ya mawasiliano iliyosambaza dini. Soma vitabu vya watunzi wa kale utaelewa kwanini kiswahili kilikuwepo
Hoja ya kwamba Kiswahili kimebeba Uislam ni kweli na ina mantiki kwasababu nilizoeleza
Hata hivyo Kiswahili si Uislam bali kuna mahusiano ya Kiswahili na Uislam kutokana na mazingira ya wakati. Ni mahusiano hayo kama yalivyo ya Ukristo na Kiingereza
Tukirudi katika Umanyema, ningekuomba usidharau lugha hiyo.
Umanyema ndio mother tongue yako hizi zingine ni za kufikia.
Na wala kuwa mmanyema hakuondoi mantiki ya utamaduni wa Ibrahimu.
Unaweza kuwa na tamaduni nyingi, muhimu ni namna gani una practice tamaduni hizo.
Kiingereza unachosema kimebeba utamaduni, hakijaondoa utamaduni wako wa Ibrahimu
Muhimu utambue kuwa dini yoyote ni imani iliyojengwa kiroho.
Hili ni tatizo kwa wananchi wetu wengi. Wanashindwa kuelewa mipaka ya dini na tamaduni