Kumbukumbu ya miaka 16 tangu kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Kumbukumbu ya miaka 16 tangu kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

KISESERA

Member
Joined
Sep 21, 2015
Posts
86
Reaction score
38
Ikiwa leo ni siku tunakumbuka kifo cha Baba wa Taifa hili hatuna budi kumuenzi kwa kuyafuata yale aliyokuwa akiyapigania

1. Kupambana na Rushwa na Ufisadi (Uhusani kwenye uchaguzi tuwakatae MAFISADI)

2. Tupige vita UDINI (Hususani kwenye UCHAGUZI, Kiongozi mwenye nasba na Udini tumkatae)

3. Tuepuke UKABILA (HUSUSANI KWENYE UCHAGUZI), Kiongozi mwenye nasaba na ukabula tumuogope kama ukoma

4. Tusiwape nafasi genge la MATAJIRI (MAFISADI) Kutawala nchi yetu

nyerere.jpg


Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 -na alipoteza maisha London, Uingereza, 14 Oktoba 1999)

Alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa taifa". Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule.

Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha.

Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."

Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wake na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.

Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.

nyerere6.jpg


Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kumbukumbu ya Hayati Baba Wa Taifa.

Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

nyerere9.jpg


Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945. Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).

Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika. Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.

nyerere3.jpg


Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza. Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi. Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi. Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.

nyerere1.jpg


Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St. Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.

nyerere5.jpg


Mwalimu alizikwa nyumbani kwake Mwitongo katika Kijiji cha Butiama karibu na makaburi ya wazazi wake na mahali alipozaliwa na familia ya Mwalimu ilisema aliagiza azikiwe hapo.


REST IN PEACE BABA WA TAIFA
 
Mwalimu alitumia muda mwingi kukemea RUSHWA na UFISADI. Leo vyama vyenye muungano kivuli UKAWA vilivyoanzishwa kwa busara za Mwl ndio makuwadi wa RUSHWA NA UFISADI.

JE, MNAMUENZI MWL SIKU HII YA LEO KWA KUMSALITI?
 
kwa kusomesha watoto wa taifa hili elimu bure na bora ili waweze kufika mahali mlipofikishwa na nyerere mkawanyonga watanzania kwa umaskini
 
Kingunge amefichua siri kuwa Mwalimu alikuwa anajiandaa kuondoka CCM kuja Chadema bahati mbaya mauti yalimkuta

Tutamuenzi kwa kuichinjia baharini CCM na majizi yake
 
Mkuu iko hivi;

Ukawa watakuwa kwenye kampeni kama kawaida yao na wata-play zile clip za Mwal. Walizoedit kitoka kwenye hotuba zake...
Mfano;

"" watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata..wasipoyapata ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm""


"" ccm sio Baba yangu"


"Mpinzani wa kweli atatoka ndani ya ccm""


"" chama kitakacho puuza maamudhi ya wananchi kitalia kilio na kikakosa mtu wa kukipangusa machozi ""



Zile clip za RUSHWA na UDINI hazitaguswa.....
 
Tunamuenzi kwa kutoa ELIMU BURE NA BORA kama alivyofanya... na kuwang'oa Maccm kama akivyotabiri MABADILIKO.
 
Jf,

Mwalimu Nyerere alitutoka siku kama ya leo, RIP.

Leo tunamkumbuka kwa mambo meeeengi sana ma hasa wakati tukielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais wabunge na madiwani.

Machache makubwa ni kama yafuatayo;

1) Alikemea sana rushwa na ufisadi.

2) Alikemea matajiri kuendesha nchi.

3) Alisema waziwazi ikulu sio pango la walanguzi na wafanyabiashara. Wafanyabiashara wanataka kwenda ikulu kufanya nini.?

4) Alimkataa waziwazi LOWASA na kumkemea kuwa hana maadili ana harufu ya rushwa, na hivyo ajitenge kabisa na uongozi wa juu wa nchi.

5) Alijitoa maisha yake yote kwa ajili ya wananchi. Hata familia yake haikufaidika na chochote.

6) Alisema mgombea urais ambae ni mkabila , mdini au mbaguzi wa aina yoyote hafai kupewa uongozi

LEO HII TUTAFAKARI KWA HAYA MACHACHE NA KAMA KUNA MENGINE ONGEZENI

Cc. Lizabon, mzee mwanakijiji
 
Ikiwa leo ni siku tunakumbuka kifo cha Baba wa Taifa hili hatuna budi kumuenzi kwa kuyafuata yale aliyokuwa akiyapigania

1. kupambana na Rushwa na Ufisadi (Uhusani kwenye uchaguzi tuwakatae MAFISADI)

2.Tupige vita UDINI (Hususani kwenye UCHAGUZI, Kiongozi mwenye nasba na Udini tumkatae)

3. Tuepuke UKABILA (hUSUSANI KWENYE UCHAGUZI, Kiongozi mwenye nasaba na ukabula tumuogope kama ukoma

4.Tusiwape nafasi genge la wala MATAJIRI (MAFISADI) Kutawala nchi yetu

REST IN PEACE BABA WA TAIFA

Huko chamani kwenu mtambo wa kutengeneza mafisad.hamia chauma au jahaz asilia
 
Hotuba ya Mwalimu Nyerere, Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma - Mwaka 1995

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage katika Hotuba Zake, mojawapo aliwahi kusema kuwa Vyama vinatakiwa kutoa Mgombea ambaye anakidhi Matarajio ya Wananchi na Siyo matarajio ya wewe mpiga kura, na ambaye anakidhi mahitaji ya Watanzania.

kwa kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyaona ndani ya Ccm watayatafuta nje ya chama cha Mapinduzi, kwani watanzania kuna mambo mengi ambayo watanzania wanataka ikiwemo kuondokana na tatizo kubwa la Rushwa, kwani Mwalimu alisema kuwa alikuwa msitari wa mbele kupiga vita dhidi ya Rushwa akiwa mwanzilishi ili Viongozi wengine pia wafuate maana hali ya Rushwa imeendelea kuitesa Tanzania.

aidha Mwalimu alisisitiza kwamba Mgombea ambaye atakayeonekana kukidhi mahitaji hayo basi anatakiwa kutetewa na watu wote Tanzania na si kumwacha hivi hivi na kuwaachia nchini ielekee pabaya kutokana na kwamba Tanzania Bado ni nchi ya Kimasikini na si nchi ya Kitajiri.

Aidha alisisitiza kwamba Kiongozi ambaye atakayeulizwa maswali atambue kwamba majibu yake yawe ni kuwa nchi hii ni ya wakulima na watu masikini na siyo nchi ya Matajiri.

kuhusu Suala la Dini Mwalimu alituachia hosia kwamba, tunapompima mtu kumchagua kama hatastahili asiusishwe na imani ya dini maana kila mmoja dini hiyo ni imani yake hivyo sisi Tanzania hatujengi makanisa wala misikiti maana hayo ujenggwa na viongozi wa Imani.

isipokuwa Tanzania wanatakiwa kutambua mambo ya tanzania kwa kupitia huyo kiongozi ambaye akiulizwa maswali awe na majibu na awe anaitambua na kuifahamu vyema nchi yetu kwa kuwa watanzania bado wanaishi maisha ya kimasikini, kupitia Chama cha Mapinduzi pia ni lazima watambue kwamba Watanzania kwa ujumla siyo watu matajiri ambao wamekinai maisha kwa kuwa wametosheka na utajiri wao.

Kiongozi ambaye atasimamia haki za watu masikini watu wengi wanazungumzia Udini,"Sisi hatujali dini ya mtu maana dini anajua mwenyewe mtu, haiji katika akili kuwa tunapomchagua mtu aituhusu sisi kuanza kumjadili kuhusiana na dini, mambo hayo yalikuwa zamani, maana kama kuna mtu anataka kufuatilia masuala ya dini ya Mtu, basi mtu huyo ni bora aende kwenye misikiti ama makanisa kwa maimamu watafute wao kama wanataka kufahamu wana waislamu wangapi, na hata kama wakristo wanataka kujua idadi ya waumini wao waende kwa maaskofu wao, sisi tunataka mtuchagulie mgombea ambaye atatusaidia kuondoa mawazo ya kipumbavu katika nchi yetu, na mmomonyoko huu kwa Taifa letu, na ikitokea wewe mwananchi umeulizwa kuhusiana na huyu mgombea kama anastahili unatakiwa kusema kwa dhati kutoka moyoni kwamba ni sahihi huyo ndiye chaguo la Watanzania" alisema Mwalimu

Aidha Mwalimu pia alisema kuwa ikitokea hivyo Basi Tanzania itakuwa aiwezi kuingia katika matatizo yoyote yanayohusiana na Masuala ya Uchaguzi, na aliweza kukemea masuala ya Ukabila, Tanzania wakati wa kupigania uhuru aikuwa na masuala ya ukabila wakati huo Uganda na Kenya ndizo zilizokuwa zikizungumzia ukabila.

Faifa ya Ukabila kwa Taifa letu kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere ni Matambiko, na kwamba hakuna haja ya kuanza kuzungumzia Ukabila na kusema kuwa Wazungu wenyewe wanayo makabila lakiniivi sasa wanaungana mifano akasema ni mataifa makubwa yakiwemo Uingereza, Urusi na Marekani kwamba pamoja na kutawala nchi mbali mbali za Afrika lakini bado wanaungana.

Mwalimu alisisitiza kwamba kabila katika tanzania ya leo hatuna haja ya kuingia katika kuulizana masuala hayo, badala yake watanzania wakae na kujadili suala la kumpata kiongozi ambaye anastahili kupigiwa kura na watanzania wote bila kujali chama isipokuwa watazame huyo kiongozi kama anazo sifa za kuweza kuisaidia Tanzania bila kujadi Chama, Dini, wala Kabila.

Aidha Mwalimu alisema kuwa wenzetu wa jirani wataanza kutushangaa pamoja na kwamba Tanzania imekuwa ni nchi ambayo imekuwa mfano wa kuigwa lakini jambo hili sasa linataka kuwa ni aibu lakini alisema dhamana ya kumpata kiongozi bora lipo mikononi mwa Watanzania wenyewe na si vinginevyo, maana lengo ni kupata Kiongozi Safi ambaye atasimamia Demokrasia yetu Tanzania.

Wasalaam
Abel sere wa moshi town
 
Tumuogope lowasa kama ukoma! Wala usione haya kuyasema haya.ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni
 
Rejea maelezo ya kina pia aliyoyatoa Mzee Kasori aliyekuwa katibu wa Nyerere juu ya Lowasa. Utajuta kuzaliwa
 
Tumuenzi mzee wetu na tusimtumie vibaya hasa CCM hususan kipindi hiki kifupi kilichobaki maana tukifanya hivyo tunaendelea kupigilia msumari wa laana juu ya kichwa cha CCM na macho ya wanaccm yatatoka moshi kwa kutumia vibaya jina la Mwl.Nyerere.
 
Hii ni kauli iliyowahi kutolewa na Baba wa taifa miongo kadhaa iliyopita lakini mantiki yake bado inaishi.

Ni ukweli usiopingika bado nchi hii ni ya Wakulima ambao ni masikini na wafanyakazi wa kipato cha kati.

Tukiwa kwenye uchaguzi huu muhimu kuna kila ishara kuwa kuna kundi linataka kuifanya nchi hii irasimishwe na kuwa nchi ya mafisadi na matajiri wasio na kifani ilhali asilimia zaidi ya 75% ya watanzania wasijue la kufanya.

Je bado unaamini katika kauli hii ya Nyerere?
 
Najiuliza mwenyewe na wanaoamini kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi wetu. Pamoja na mapungufu yake mengi alimaanisha anachokisema. Je angekuea hai EL angejaza fomu kugombea u rais na kupita? Najiuliza pia Mh. Rais wangu Jk angelikuwa rais wa JMT leo?
 
WAKATI Benki ya NBC ikiuzwa kwa wawekezaji wa Afrika Kusini mwaka 2000, kwa thamani ya shilingi bilioni 16, yenyewe ilikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 151 taslimu katika akaunti zake mbalimbali duniani,

Kiasi hicho cha fedha ni mbali na thamani ya majengo na mali nyingine za NBC ilizokuwa ikimiliki wakati huo, na kwa maana hiyo, serikali iliuza benki hiyo kwa kiasi cha asilimia kumi ya kiasi ilichokuwa nacho kama akiba.

Mmoja wa wapinzani wakuu wa ubinafsishaji wa benki hiyo alikuwa ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alilia machozi wakati alipopewa taarifa za kutaka kuuzwa kwa benki hiyo.

Sasa, nimefanikiwa kupata ripoti ya mwisho ya hali ya kifedha ya benki hiyo wakati ikiuzwa, inayoonyesha kiasi cha fedha ilizokuwa nazo katika mabenki mbalimbali duniani.

Chini ya taratibu za kibenki, NBC ilikuwa na fedha zake katika akaunti za mabenki mengine ya nchi za nje; maarufu kwa jina la Nostro Accounts, kama ambavyo mabenki ya kigeni yalivyokuwa pia yana akaunti zake NBC.

Nimefanikiwa kuona ripoti, ambayo pamoja na mambo mengine, inaonyesha kwamba NBC ilikuwa na fedha katika nchi za Australia, Austria, Uingereza, Marekani, Canada, Ujerumani, Ufaransa, Uswisi, Uholanzi, Ubelgiji, Japan, Sweden na Norway.

Nchi nyingine ambazo NBC ilikuwa na fedha ni Denmark, India, Italia, Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Pakistani, Zambia na Zimbabwe.

Benki hiyo ilibadilishwa jina kutoka kuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kuwa NBC (1997) baada ya ubinafsishaji wake mwaka 1997, kabla ya kuitwa NBC Ltd baada ya kuuzwa mwaka 2000.

Baadhi ya mabenki ambayo NBC ilikuwa na akaunti ni Commonwealth Bank ya Australia, Barclays, Lloyds, ANZ Bank, Midland Bank, Deutsche Bank, National Westminster Bank, Citibank, HSBC, Canadian Imperial, Den Norske, Banque National du Paris, Banca Commerciale Italiano na nyinginezo.

Ubinafsishwaji na hatimaye uuzwaji wa benki hiyo ni miongoni mwa masuala tata yaliyogubika utawala wa serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

Serikali ilibinafsisha NBC kwa maelezo kwamba haikuwa na fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya kibenki, madai ambayo waliokuwa wakiongoza benki hiyo walisema hayakuwa ya kweli tupu.

Gazeti hili limefanikiwa kuzungumza na baadhi ya wakuu wa NBC, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Hazina waliokuwa kazini wakati huo na wengi wao walithibitisha kuwapo kwa kiwango hicho cha fedha na kwamba serikali haikutakiwa kabisa kuiuza benki hiyo.

“Ni kweli kwamba NBC haikuwa na fedha za kutosha kwenye akaunti zake za hapa nchini. Lakini jiulize kwanini ilifikia hapo? Ilifika hapo kwa sababu serikali ilikuwa imekopa kiasi kikubwa cha fedha pasipo kulipa.

“Hivyo serikali ndiyo iliyosababisha hali hiyo kwa kukopa bila kulipa. NBC ndiyo ilikuwa kimbilio la serikali kila ilipokuwa na tatizo la kifedha. Lakini dawa haikuwa kuiuza ile NBC. Serikali ingeuza tu majengo manne ya benki kwa mabenki haya ya kigeni yaliyokuwa yakitaka kuja nchini.

“Nakumbuka tulisema hivi, tuuze lile jengo la Bank House ambalo sasa ndilo linatumiwa na NMB jijini Dar es Salaam. Tungeweza kuuza na moja kubwa katika mikoa ile mikubwa ambayo mabenki haya mapya yalikuwa yanataka kuwa na majengo.

“Siku hizi mabenki yamekosa majengo mijini hadi yanakwenda kutafuta maeneo vichochoroni na wanapata shida na majambazi. Tulitaka tuuze maeneo ya mijini kwao. Kwa kuuza majengo manne tu, NBC ingeweza kuwa katika hali nzuri na ikajiendesha. Cha ajabu wakubwa wakaamua kuiuza,” alisema mmoja wa watu walioshiriki kwa karibu katika mchakato mzima wa uuzwaji wa benki hiyo.

Tuliambiwa kwamba ili kuhalalisha ubinafsishaji na uuzaji huo wa NBC, serikali kwanza iliomba ushauri wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu ambayo ilisema benki hiyo inaweza kujiendesha pasipo kuuzwa lakini baadaye ikaenda kuomba ushauri kwa mojawapo ya kampuni za kigeni, PriceWaterHouseCoopers ambayo ilipendekeza kuuzwa kwa NBC kwa maelezo kwamba haina fedha.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa NBC wakati wa mchakato wa kutaka kuiuza, Donald Kamori, anadaiwa kupingana na mpango wa kutaka kuiuza na inaelezwa ndiyo chanzo cha kung’olewa katika wadhifa wake huo.

Katika mazungumzo yake , aliyepata kuwa Katibu Myeka wa Mwalimu Nyerere, Samwel Kassori, alipata kusimulia namna Kamori alivyoeleza umuhimu wa kutouza NBC, mawazo ambayo Mwalimu alikubaliana nayo.

Nilielezwa kwamba vigogo waliotaka NBC iuzwe kwa gharama yoyote walimwona Kamori kama mtu aliyewachongea kwa Mwalimu na ndiyo maana aliondolewa NBC haraka.

Nimemtafuta Kamori ili aeleze kuhusu uhusika wake katika ubinafsishaji na uuzaji wa NBC lakini alikataa kuzungumza chochote kwa maelezo kwamba hapendi kuzungumzia mambo hayo.

“Naomba utafute watu wengine wakwambie. Mimi sina cha kusema. Wapo watu waliokuja kuchukua nafasi yangu watafute na uwaulize. Naheshimu sana gazeti lenu lakini naomba nisiongee,” alisema Kamori.

Hata alipoelezwa kwamba mtu aliyechukua nafasi yake, Dk. Francis Mlozi, aliyetokea BoT, amefariki dunia na hakuna njia ambayo linaweza kumpata, Kamori alisisitiza kwamba lazima wapo wanasheria au wahasibu waliokuwapo wakati huo ambao wangeweza kusaidia lakini si yeye.

Juhudi zangu hili kutafuta taarifa zaidi zililifikisha kwa aliyekuwa Mwanasheria wa NBC, Mathew Kakamba, ambaye naye hakutaka kuzungumza chochote kuhusu benki hiyo.

“Ndugu yangu mimi nimeondoka NBC zamani kidogo. Hapa katikati kuna mambo mengi yamepita na mengine nimesahau. Naomba utafute watu ambao wanaweza kuwa wanakumbuka vizuri,” alisema Kakamba.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, ambayo pia inasimamia shirika hilo, alisema wamezungumza na ofisi za Gavana wa BoT na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili suala la ubinafsishwaji na hatimaye uuzwaji wa NBC litazamwe upya.

“Sijajua hizo taarifa zako za Nostro Accounts kama ni za kweli au la lakini ninachojua ni kwamba zoezi zima la ubinafsishwaji na uuzwaji wa benki hiyo lina kiwingu kizito na ukweli ni lazima ujulikane. Gavana na CAG tayari wanaliangalia suala hilo,” alisema Zitto.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika tovuti ya NBC Ltd, kufikia mwezi Desemba mwaka 2010, benki hiyo ilikuwa na mali zenye thamani ya shilingi trilioni 1.4 na amana zenye thamani ya shilingi bilioni 153.

Benki hiyo iligawanywa mwaka 1997 ambapo taasisi tatu zilizaliwa. Taasisi hizo ni benki za NBC na NMB iliyopachikwa jina la Benki ya Makabwela na Shirika Hodhi la NBC ambalo kazi yake kubwa ilikuwa ni kusimamia zilizokuwa mali za benki hiyo kabla ya kugawanywa.
 
Tunamuenzi sana! Alisema kuwa Wananchi wasipoona mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Alisema kuwa chama chochote kikikataa kumchagua mtu anayependwa na watu wengi chama hicho kitaanguka. Alisema CCM sio mama yake hivyo angeweza kuiacha kama ingebidi kufanya hivyo! Alisema Bila CCM imara nchi itayumba! Na sasa nchi imeyumba kwa CCM si imara tena. UKAWA tunamuenzi mwalimu kwa mambo mengi!!
 
Kuna mambo mengi kumuhusu mwalimu nyerere na mi nakubali kua alikua MTU mzuri katika kuongoza watu hasa kupigania haki lakini kuna mambo mengi tu aliyafanya ambayo yanaleta matatizo Leo kisa mwalimu alisema nyerere si mungu so si kila alichokisema kilikua sahihi kuna vingine alivitamka mpaka leo vinaleta athari kwa nchi yetu lazima tuamini huyu slikua binadamu na katika ubinadamu huo kuna maneno sliyokua anaongea ambayo hayakua sahihi kuyatamka lakini aliyatamka kwa kua alitaka MTU au watu Fulani wapate kitu Fulani mwalimu nyerere ilifika mahali akawa hataki kabisa kumsikia mmoja ya waliokua wanagombea urais john Samuel malecela kiasi kwamba alikua tayari kurudisha kadi ya ccm kama jina lake lisingeondolewa mapema na alifanya hivyo kwa chuki ambayo sijui ilitokea wapi kama kuna ambae anajua sababu ya nyerere nyingine ya kumchukia kwa kiwango cha juu malecela mwaka 95 kisa tu alikua anagombea urais aniambie hapa. Athari za nyerere hasa katka chaguzi za Tanzania ni nyingi sana ukimtaka huyu utasikia nyerere alimkataa ukiwauliza aliklmkataa kwa sababu zipi hawana majibu ya kueleweka
 
Pamoja na mazuri mengi aliyoifanyia nchi hii ambayo hakuna atakayekataa but yapo pia mabaya yake mengi tu aliyoyafanya wakati wa utawala wake.
 
Kuna mambo mengi kumuhusu mwalimu nyerere na mi nakubali kua alikua MTU mzuri katika kuongoza watu hasa kupigania haki lakini kuna mambo mengi tu aliyafanya ambayo yanaleta matatizo Leo kisa mwalimu alisema nyerere si mungu so si kila alichokisema kilikua sahihi kuna vingine alivitamka mpaka leo vinaleta athari kwa nchi yetu lazima tuamini huyu slikua binadamu na katika ubinadamu huo kuna maneno sliyokua anaongea ambayo hayakua sahihi kuyatamka lakini aliyatamka kwa kua alitaka MTU au watu Fulani wapate kitu Fulani mwalimu nyerere ilifika mahali akawa hataki kabisa kumsikia mmoja ya waliokua wanagombea urais john Samuel malecela kiasi kwamba alikua tayari kurudisha kadi ya ccm kama jina lake lisingeondolewa mapema na alifanya hivyo kwa chuki ambayo sijui ilitokea wapi kama kuna ambae anajua sababu ya nyerere nyingine ya kumchukia kwa kiwango cha juu malecela mwaka 95 kisa tu alikua anagombea urais aniambie hapa. Athari za nyerere hasa katka chaguzi za Tanzania ni nyingi sana ukimtaka huyu utasikia nyerere alimkataa ukiwauliza aliklmkataa kwa sababu zipi hawana majibu ya kueleweka

unalalamika km mwanamke aliyenyimwa matumizi
njoo hapa orodhesha hayo mambo yanayoleta matatizo mpk sasa
 
Back
Top Bottom