Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
1. Binti alikuwa mwanachuo, chuo flani Mkoani. Nimeenda kikazi ndo bado kijana miaka hiyo. Katika kupita pita town nikakutana naye kwenye duka moja la vinywaji. Nikamtamani nikaomba namba ya simu. Akanipa.
Baadaye tukawa tunachat na hatimaye nikamwambia kusudio langu na kumtaka aje tupate dinner jioni tuongee vizuri. Nlijua siku hiyo ngeosha bakora. Nikawa mfukoni nina tsh 40,000 ambayo nilijua ingetosha mlo na vinywaji.
Basi nikaenda eneo husika. Baadaye akaniambia nimwelekeze nimekaa wapi. Heeeehh..... Si kaja na wenzie wengine wawili. Kila mtu akaagiza chips kuku. Ambayo mpaka hao wao tu walikuwa wanatumia 27,000 na vinywaji beer Heineken kila mtu.
Nlianza hisi kizunguzungu.maana ni wazi ile 40,000 ilikuwa inaelekea kutotosha. Mimi nikaagiza chips mishkaki mitatu. Pale mshkaki mmoja tsh 2,000 nikaona hili sasa so.
Ikabidi nifanye kama naenda washroom.nikampigia dereva wa ofisini aniletee tsh 100,000 ntamrudishia kesho. Nikarudi ndani. Baada ya kama dk 20 dereva akapiga simu nikachukue pesa nikatoka nje nikachukua sasa nikiwa na kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya.
Yule dada alifanya uswahili ambao alikuja jutia baadaye. Maana katika wale marafiki zake mmoja alikuwa mkali kuliko yeye. Nikavumilia tu siku ile. Mpaka nlipokuja mla nikaanza kumweka sawa na mwenzie. Nikamla halafu nikakaa kwake. Yule dada alikuja gundua akaumia sana. Nlimwambia ni yeye aliniletea. I hope alijifunza kitu.
2. Hii ilitokea kwa dada mmoja. Nikamweka sawa akanikubalia na kuniambia lakini aliwahi kuzaa. Nikasema haina shida. Siku nimepanga naye appointment jumamosi lunch Mlimani City. Akaniambia atakuja anikute. Kweli nikafika muda muafaka.
Nimetulia akapiga simu niende mchukua. Nikamwelekeza nilipo akadai atapenda nikamchukue. Nikaenda kumbe anataka nimlipie Taxi. Zikanitoka 20,000 za Taxi maana ubaya wa mazingira yale huwezi hata bargain. Anashuka na watoto 4. Nikashtuka. Ila i held my breath. Akawaambia haya muamkieni uncle.
Wakaja nisalimia.... Nilikwazika sana.first appointment anawaleta na akina uncles tena? Tukaenda kaa samaki samaki...yeye amekazana kupiga picha kila tukio. Ndo tumekaa anitambulisha watoto wake. Nikamwambia sawa.vikaagizwa vyakula. Nika piga hesabu kichwani nikaona haya majanga.
Nikamwambia ngoja nikanunue vocha. Sikurudi na namba yake nili block. Niliona ni mambo ya kiswahili.
Dada au Kaka ni appointment gani worse uliwahi kutana nayo huwahi isahau?