Kumbukumbu ya moja ya tarehe mbaya kutokea (Worse Date Ever)

Maotea ni nini?
 
😅😅😅😅 hii kali
 
Mimi niliwahi kumpenda binti mmoja haswa kipindi iko nimeingia chuo nimetoka boys school, yani kila nikimuona yule binti mwili unfreezy akitokea mbele yangu naskia kama mwili na akili vinafanya kazi tofauti nafaint nakua sijielewi.

Nilipitia mengi hadi nikaja kupata no zake na kumwomba tukutane restaurant ilokua unaogopwa na watoto wengi wachuo sababu ya ghalama nikasema huko ndo pakuchukulia credit zangu.

Basi mtoto wa mkulima nikachukua ela nikaweka ela elfu80 kwenye wallet nilikua najua itabaki tuu maana nilipanga kuywa juicy tu akifika nimdanganye mi nimeshakula tiyari.

SIKU MBAYA YENYEWE

Mapema jioni jioni nikawa nishafika eneo la tukio nimetulia napanga maneno yatakayo mchekesha na kumfurahisha, Picha linanza, mtoto kanitumia text niko naingia upo upande gani? Si moyo ukashituka mapigo yakanza kwenda mbio!!! na tumbo likanza kunguruma sa sijui ni juicy au nini, nikasimama nimwangaze njia yakuingilia, lahaula!! alikua kapendeza sana, aliponiona akanza kutembea kuja nilipokua wallahi nilianza kujuta kwanini nimemuita ni kama nafsi ilinikana mwili maana yule binti hakua lever zangu nilikua kama najaribu tuu ila ngoma ikaitika.

Nakumbuka kituko chakwanza ni kwenye salam, nilitaka et kumpa mkono kama vile officin ye ndo akaupokea kisha akanihug ile ya kuweka distance katkat mi apo nisha faint zamaani najaribu kurestore maneno ya ucheshi nilopanga kumwambia yalipotea yooote!!! Nakumbuka nilimpa salamu marambilimbili,

Tukio lilofanya nijutie ile siku kabisa ni tulianza kuongea nikawa nimechapia neno badala ya MASAA yanaenda nikasema MASHAA yanaenda apo alikua anakula samaki na addition ya chips mi nakula ugali makange ye ndo aliyeniordia maana nilitak kusema nimeshiba sasa yale makange yalikua na pilipili nyingi na mimi nilijikaza tuu asinione myonge sa nilivochapia vile si akangua kicheko na mimi ile kucheka likatoka puto kwenye pua lile la kamasi likapasuka na aliona ndo akanicheka hadi meza za jirani wakatuangalia na engerchief sikua nayo nikafuta na mkono uk nimeinama chini akanambia nenda washroom sa kwenda kwenyewe uko washroom sijui iko upande gan nikienda ivi watu wananambia nenda kwa uku yani nikajiona kituko na nikajidharau pia nikajisemea moyoni nimeletwa kusoma uku huu ni ujinga naofanya.

Inshot nilirud kutoka kujisafisha kidogo ila nilikua nimepoa sana msichana alikua kachangamka zaidi nilimwambia ombi langu sikunyingine akanikubalia ila sikumla maana wajanja walimchukua hadi leo ni single mother nachat nae tuu DM insta ila ananiambaga ananipenda sema nipo kwenye maisha memgine sintomsahau na sitohisahau iyo siku.
 
Umetisha Sana mkali wangu😅😅😅
 
Kwa nini usimuoe hivyo hivyo 🤣
 
Hiyo kuja na Eicher imenichekesha [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ha haaaaaa umenichekesha Sana!sipendi hiyo Mambo mengine vipi lakini?
 
Dah!!! Nimecheka kifala hapo kwenye puto la kamasi umenikumbusha utotoni hukooo😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Yaani ukiona mwanadada anasema umbambamba huyo Ni mchambaji hatari,ndio wale chura wa kwenye singeli
 
🤣🤣🤣🤣🤣Kha date zako kiboko!
 
Izo biz kama kawaida Yako mkuu [emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
 
Ukala pindi au sio [emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ulkua kwenye paper hiii balaaa
 
Uyu baba mzuri ataki usumbufu sumbfu wa kijinga [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
kifua kidogo Sana huna uvumilivu
 
mh ulimpeleka demu guest zanzibar???
heb tuambie ulimjingizaje kama sio mkeo au mm ndio nimesoma vibaya au ni zanzibar ya pale kigoma ujiji
 
Umezingua kinoma mwanaume unakosaje kitambaa ila hilo wenge limenifanya nicheke sana .
 
Hahahaa.. mkuu umenichekesha sana[emoji23][emoji23]
 
Ulikuwa mpenda starehe wewe ukakutana na wanaojua hesabu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…