Lethergo
JF-Expert Member
- Aug 7, 2023
- 6,534
- 11,421
Wakuu!
Naomba nielezee na hii walau kwa uchache.
Katika pitapita zangu za hapa na pale na kuangalia huku na kule kwenye kujitafuta, kujitafakari, kufikiri na kujichanganya na watu tofauti tofauti. Nimekuja kugundua/kubaini kwamba kuna ongezeko kubwa sana la wanawake wenye msongo mkali wa mawazo.
Hususani wenye umri kuanzia miaka 22 mpaka 40+ hao ni kwa kiwango kikubwa yaan ni kwa kiasi kikubwa wamekumbwa na msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huo umewapata kwa sababu tofauti tofauti, kwa mfano hawa wa miaka 22-30 ni wana msongo mkali wa mawazo mpaka unaweza ukasema wamekumbwa na mapepo wabaya/wachafu.
Kuanzia 30 kuelekea 40 hawa ni msongo umechachamaa vibaya sana haswa haswa km ikitokea kile walichokitarajia kimekua kinyume na uhalisia kwa hio wamechanganyikiwa kabisa, msongo umekua wa kupindukia.
Miaka 40 kuelekea juu mpaka 50/60 ndio Mungu nisaidie usimkute mwanamke wa aina hii ambae msongo wa mawazo umemuelemea mpaka anapoteza kumbukumbu.
Turudi nyuma kidogo wanawake wenye miaka 25 kuja juu mpaka 30+ hawa wengi wao wakiwa hawajapata kile walikitarajia maishani kwanza kikawaida kabisa huanza kua viburi, jeuri, hawaambiliki na hujenga dharau kubwa sana kwa wanaume. Ila kadri umri unavyosogea ndivyo akili inazidi kuchanganyikiwa na kiwango cha msongo wa mawazo kinavyozidi kuongezeka.
Utajuaje sasa kwamba huyu mwanamke ana msongo wa mawazo?
Ipo hivi.....
Kwa kutumia mfano mdogo sana kama wewe ni mpenzi wa ku-view WhatsApp statuses basi kuna kitu inabidi ubaini na ujifunze, nitakupa 'code' ukimuona mwanamke au binti ka-post statuses za picha au video fupi ya mjongeo akiwa anatabasamu saaana tena saaaaana au kaweka dp picha akiwa anatabasamu saaaana, ndugu yangu huyo unaemuona elewa kwamba ni ana msongo mkubwa wa mawazo hapo alipo ni ana-pretend tu kutoa tabasama la uongo ila ndani kwa ndani anaungua vibaya sana analia machozi yasiyoisha na yasiyokauka.
Asikuhadae na hio fake smile ni amepatwa na msongo mkubwa kiasi kwamba sasa anaji-post hivyo ili walau tu apate watu wa kumpunguzia msongo wa mawazo na ikitokea mwingine akaisema vibaya picha yake basi msongo wa mawazo unapaa mara 2 au 3 ya vile ulivyokua mwanzo.
Mbili, wanawake wengi sana wana msongo wa mawazo na wengi hujipooza na social medias picha na video kuziweka mtandaoni ili wapate likes wapate comments walau waone tu kuna watu wanawaona, mfano ukiangalia fb stories nyingi nyingi nyingi km una marafiki wa jinsia zote basi utaona wanaopost wengi wengi ni wanawake wakiwa na fake smile yaan tabasamu la uongo, nyuma yake akiwa na msongo mkubwa wa mawazo ila anaigiza tu km vile kila kitu kipo sawa. Ndugu yangu hilo ni tabasamu la uongo.
Wanawake wanapitia changamoto kubwa sana ya msongo wa mawazo mpaka inafika hatua sehemu pekee wanayoona wanaweza kutuliza msongo wao wa mawazo ni nyumba za ibada au mikutano ya injili, wakihisi labda wana mapepo wabaya wamewaingia kumbe ni msongo mkali wa mawazo au labda kutokana na hali zao basi wakijazana kwenye makongamanoya kiinjili au hio mikutano msongo wa mawazo utaacha kumbe ni kinyume chake.
Na huko kwenye nyumba za ibada wakihisi wanaenda kupunguza msongo wa mawazo kumbe akifika huko ibada sio ya bure anatakiwa atoe hela ya kuhudhuria ibada unaingia msongo mwingine mkali wa mawazo unaoanza kuwaandama.
Ukitembea hizo sehemu za mikutano ya injili na kwenye makongamano utaona ya kwamba idadi kubwa ya wahudhuliaji ni wanawake, hujawqhi kujiuliza ni kwanini? Kwa sababu wanawake wanaongozwa na msongo mkali wa mawazo unaotokana na hisia zao za ndani. Kuna wakati hua wanafika hatua wanatembelewa na kichaa cha muda (temporary insanity) sababu ya msongo mkali wa mawazo, wewe ukiwa sio mwelewa mzuri wa jinsi wanawake walivyo itakupa tabu kuwaelewa.
Mwanamke hubadirika msongo wa mawazo kwa vipindi tofauti tofauti, msongo wa mawazo wa mwanamke akiwa kwenye hedhi hubadirika pale anaopotoka kwenye hedhi akatoka akikaribia hedhi anakua na msongo wa mawazo mwingine akiingia hedhi msongo wa mawazo unakua mwingine, mwanamke akishika mimba anakua na msongo wa mawazo mwingine, kwa hio mabadiriko ya msongo wa mawazo huenda kuendana na mabadiriko ya vipindi vya mzunguko wa hedhi wa mwanamke.
Mwanamke akishatoka kwenye hedhi siku 3/4/5 za mbele msongo wake wa mawazo ni tofauti kabisa na vile akiwa kwenye hedhi na kabla ya kuingia kwenye hedhi.
Msongo wa mawazo wa mwanamke akiwa na mimba changa ni tofauti na msongo wa mawazo wa mwanamke akiwa na mimba ya miezi 9 na msongo wa mawazo wa mwanamke aliejifungua kipindi anachojiuguza mgongo na kujikanda ili tumbo lirudi ndani na kuurudisha mwili wake km mwanzo ni tofauti na msongo wa mawazo wa mwanamke anaenyonyesha.
Msongo wa mawazo wa mwanamke hautulii, haupoi na haupumziki mwanamke kila siku mpya anakua na msongo mpya wa mawazo yaan alivyo amka jana sio km atakavyoamka leo kila siku ya mwanamke ina msongo mpya wa mawazo.
Sasa hivi kumekuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo kwa wanawake kwa sababu ya matatizo mbalimbali ambayo yameongezea kwenye ule msongo wao wa kawaida.
Mfano wa mambo ambayo yanaongezea msongo mkali wa mawazo kwa mwanamke ni km ifuatavyo, kuachwa na mwanaume wakati ambao anamuhitaji sana, mwingine alikua na kawaida ya kutoatoa mimba sasa kila mimba ikiingia inatoka, kutokupata mtoto/watoto, kutokusikilizwa pale anapohitaji kusikilizwa, kutelekezwa na mwanaume aliemtia mimba na kuishia kua single mother, kupitia unyanyasaji wa kingono/kubakwa, kuteswa kihisia aidha na mwanamke au mwanaume km kuambiwa maneno yasiyofaa na kadhalika, kutokua na kazi maalum ya kufanya ili kujiingizia kipato, kua na mahusiano ya mbali, kutokuolewa kwa wakati na umri unakimbia huku kila siku wenzio wanaolewa, kuanza kukopa vicoba na kuishi na madeni yasiyo na kikomo, kutokua na uchumi mzuri mwisho anaishia kudanga, kutokua na ajira rasmi, kuishia kua jobless na amesoma akafaulu, kuvujishwa kwa clip au picha yake chafu mtandaoni ambayo alifanya iwe ya faragha/siri, nk hivyo ni baadhi ya vile vinavyoongeza msongo mkali wa mawazo kwa mwanamke.
Kwa sasa hivi idadi ya wanawake wenye msongo wa mawazo imekua kubwa sana. Mamlaka zinazohusika wajitahidi kuliangalia kati hili. Hususani miaka ya kuanzia 25 mpaka 30+, tena hawa wanaofika 30 na mambo yao yamekaa vibaya hajaolewa, hana kazi, hana ajira, uchumi wake upo upo vibaya, madeni hayakauki kila sehemu anadaiwa vicoba kwenye vikundi na hajui analipalipaje, hana mahusiano yanayoeleweka leo yupo na Juma kesho yupo na Hussein keshokutwa yupo na Selemani, yupo yupo tu, fake smiles zisizoisha kwenye statuses na story zao, kila siku afadhari ya jana, ni hatari kwa afya zao za akili.
Naona kwa leo inatosha kuelezea niishie hapa.