Kumekucha bomoabomoa Ubungo-Kimara ndani ya 90m za hifadi ya barabara

Kumekucha bomoabomoa Ubungo-Kimara ndani ya 90m za hifadi ya barabara

Pamoja na kuwa Barabara ya Ubungo—Kimara (stop over) zimepigwa X jioni hii hadi usiku huu. Wananchi wamepewa siku 30 waondoke kupisha upanuzi wa barabara.

Pia kuanzia Kimara Bucha mpaka Kimara resort wamepewa Notisi ya kobomoa na kuvacate kwa walio ndani ya Mita 90 za hifadhi ya barabara kama barua inavyoonesha.
Hii yote ni kwa ajili ya kuendelezwa kwa barabara hiyo na wakala wa barabara TANROADS. Nakala ya notisi hiyo ni kama inavyoonekana hapo chini:

View attachment 1847872
This time i hope watafidiwa
 
Sukuma gang chato gang at work..ila they will perish soon
Kwa hiyo wewe unataka nchi isiwe na barabara, na wala mipango ya matumizi ya ardhi wala mipangilio ya ujenzi?
Wewe jamaa wewe ni mtu wa hovyo sana. I declare and decree, you have failed again and if you are enchanting against people with development mindsets, tubu dhambi hiyo na uache ujinga huo tena. La sivyo, wao kwa macho yao watashuhudiwa ukomo wako tena muda si mrefu.
 
Hata Ulaya wakati wanajenga train za ardhini (underground) walihamisha watu mijini. Hii ndiyo dhana kubwa ya Rais kumiliki ardhi.

Kabla ya kufanya hivyo inatakiwa watu wajengewe nyumba na kulipwa pesa ya usumbufu wa kuhama. Kama furniture ziliharibika wakati wanahama. Pia wanapohamia pawe na huduma zote muhimu za kijamii, maji, umeme, barabara, hospitali, shule, soko na kituo cha polisi.
 
Mama inampasa apate mtu kama Sabaya na ubaya wake wote ili amsaidie.kuna vitu vya kuhoji kizalendo.
Hizi wiki mbili za kumalizia mafungu kwa morogoro nimeshuhudia barabara ya old dsm road ikiwekwa changalawe za kutosha juu ya rami na baadhi ya maeneo yakitanuluwa kwa kumwagiwa lami nyepesi kama maji huku ikiachwa barabara ya mjimpya ambayo ina mashimo na ilijengwa ndani ya miaka 10 iliyopita.barabara ya mjimpya haikuwa na lami nzito na imebanduka banduka na kuacha mishimo halafu leo hii sehemu ambayo ina lami kama mkeka ina mwagiwa tena changalawe.
Kuna mawili inawezekana wanataka kumgombanisha mama na wananchi au wanaopanga hizi kazi hawapiti maeneo husika bali wana letewa na maofisa ambao wao wana waza 10 %kutokana na mishahara yao midogo.
Morogoro barabara ya kihonda manyuki nayo ni mbovu,yepsa ukiwa na gari ndogo unajuta,
 
Siyo kila Maamuzi tu ni ya Kuilaumu Serikali Mkuu. Na bahati nzuri wakati Wewe ukitaka 'Kuichongea' Serikali kwa Wakazi wa huko ila Wananchi wenyewe wanajua na walishajiandaa kwa hayo Maamuzi baada ya hata Wao wenyewe Kugundua kuwa Wamejenga Kiholela japo kuna ambao wamejenga Kihalali na hao ama Wameshalipwa au Watalipwa Fidia na Mamlaka ( Serikali ) husika.
Hii id imekua HACKED au...😳😳😳😳
Mbona unaandika kwa staha sana, sio kawaida yako!😀😀😀😀
 
Mama anaupiga mwingi kweri-kweri.
Ahahahahahaha kiufupi mama kawakomesha waliokuwa na kisebusebu kwake!

Kiufupi wamejikuta hawaoni tofauti na yule kipala mwenye speed ya ndege vita aina ya F22 raptor yenye iko inafanya maneuvability zisizo elezeka!

Saivi kaanza kuwatisha akina Mbowe..ahahahaha
 
Hahaaaaa yaan nikimwangalia SAMIA namuonea huruma tu maana hajui lolote maskini ye anajipigia tu misele hajui kuwa kuna wenzie wanamchonganisha na wanachi kwa makusudi kabisa

walianza umeme, wamekuja mafuta, haya makato ya line za simu, bado hapo makato ya luku haya sasa bomoa bomoa karibu kila mkoa yeye yupo yupo tu haelewi lolote maskini mzanzibari wawatu, hazijui fitna za wabara huku yeye anaamini wapo pamoja wanaimba wimbo mmoja kumbe wenzie wana hama tune taratibu kwa ustadi mkubwa.

Yaan wananchi huku hawamwelewi kabisaa na wamesha anza kumchukia kwa sasa maana tangu ashike nchi vitu vya msingi tena vinavyo gusa wananch moja kwa moja vimeanza kupanda bei
Kwahiyo mkuu unamaanisha tumepigwa au!

Ila sema Magu alikuwa na Mapungufu yake lakini moto wake haukuwa wa kawaida..nakumbuka anamfokea Thonthony yule Mcanada wa Baric duh!

Mzee alikuwa naye anajua masuala mbalimbali ya kitaalam! Sasa Mama yeye kakalia mipasho na kuinua mabega, yaani kufikia 2025 aisee atakuwa yuko hoi wallah tena!

Na watu wa bara ni hatari, si washamgundua kuwa amekalia kutoa mikeka ya wateuliwa, wao wanamtia kwenye tanuli la moto wa mkaa wa mawe...yaani akija kugeuka atakutana na maskendo balaa..

Wazanzibar kama wao wana maadili vile ukiwaangalia kwa ndani, sasa watu wa bara hawana habari na mtu wao kupiga tu; shauri yake..
 
Pamoja na kuwa Barabara ya Ubungo—Kimara (stop over) zimepigwa X jioni hii hadi usiku huu. Wananchi wamepewa siku 30 waondoke kupisha upanuzi wa barabara.

Pia kuanzia Kimara Bucha mpaka Kimara resort wamepewa Notisi ya kobomoa na kuvacate kwa walio ndani ya Mita 90 za hifadhi ya barabara kama barua inavyoonesha.

Hii yote ni kwa ajili ya kuendelezwa kwa barabara hiyo na wakala wa barabara TANROADS. Nakala ya notisi hiyo ni kama inavyoonekana hapo chini:

View attachment 1847872
wangebomoa mita 45 Tu bana! tisini wanabakiza pori kati watu wanabakwa na kunya vichakan
 
kuna watu wanapenda kuishi pembeni ya barabara.
Hayati JPM aliwahi kusema;
"Kuishi karibu na barabara ni kutafuta umasikini"
tujenge mazoea ya kujenga nyumba za kuishi mbali zaidi na barabara ili nyumba zetu zibaki zaidi ya miaka 100, tusije kuwa sumbua wajukuu na vitukuuu.

japo hiyo barua inaonekana sio ya kweli sio sahihi ni batili
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kila Maamuzi tu ni ya Kuilaumu Serikali Mkuu. Na bahati nzuri wakati Wewe ukitaka 'Kuichongea' Serikali kwa Wakazi wa huko ila Wananchi wenyewe wanajua na walishajiandaa kwa hayo Maamuzi baada ya hata Wao wenyewe Kugundua kuwa Wamejenga Kiholela japo kuna ambao wamejenga Kihalali na hao ama Wameshalipwa au Watalipwa Fidia na Mamlaka ( Serikali ) husika.
Pia awavunji maeneo mapya- Kimara ilipovunjwa miaka ya 90 kuna wengine walibakiziwa pande moja za nyumba ama vijinafasi hawa waliendelea kaa na kuendeleza hizo sehemu.Hizi ndizo zinazovyunjwa na sio maeneo mapya
 
Hahaaaaa yaan nikimwangalia SAMIA namuonea huruma tu maana hajui lolote maskini ye anajipigia tu misele hajui kuwa kuna wenzie wanamchonganisha na wanachi kwa makusudi kabisa

walianza umeme, wamekuja mafuta, haya makato ya line za simu, bado hapo makato ya luku haya sasa bomoa bomoa karibu kila mkoa yeye yupo yupo tu haelewi lolote maskini mzanzibari wawatu, hazijui fitna za wabara huku yeye anaamini wapo pamoja wanaimba wimbo mmoja kumbe wenzie wana hama tune taratibu kwa ustadi mkubwa.

Yaan wananchi huku hawamwelewi kabisaa na wamesha anza kumchukia kwa sasa maana tangu ashike nchi vitu vya msingi tena vinavyo gusa wananch moja kwa moja vimeanza kupanda bei
Yeye anawaomba wafanye haki 😅😅😅 hajui watumishi wakoje wa kibongo! Yani Magufuli alivyoendesha nchi ndio hasa Tanzania ilitakiwa iendeshwe vile.

Sio kuwabembeleza watumishi maana wataunda magenge ya wizi tu ndio kitu wanakiweza hicho na hela zikitolewa za kulipa watazipiga panga ziingie mifukoni😅
 
Back
Top Bottom