GE2025 Kumekucha! CCM yaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa njia ya mtandao

GE2025 Kumekucha! CCM yaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa njia ya mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Chenga umepigwa wewe. Mnahangaika na kuifuta CHADEMA, halafu ghafla ndani mwenu Kuna shida mpaka mnaitisha vikao kila siku. Endeleeni kujipiga chenga wenyewe.
Umezaliwa 2009 au 2005?!!!
Hivi Kuna chadema Bado kwa unavyoona (maana naona hapa mwenyewe inahitaji vikao vya ccm mpaka unakasirika ukionA vinachelewa)?!!🤣🤣🤣🤣
Mipango ya ndani huijui mbwiga wewe..........unapoambiwa siasa ni sayansi uelewe.
 
Andikeni ni tetesi sasa maana hakuna mamlaka iliyothibitisha.
 
Majirani zetu wapendwa wa hspo Kenya hii kitu ya mitandao wanaipenda sana!
 
CCM ITAWATESA SANA NDO MJUE KUWA KILA MTU TANZANIA NI CCM
 
Ccm kwa mara ya mwisho walikutana January??
Wewe msahaulifu au ni mvivu wa kukumbuka. Ccm kamati kuu walikutana March,
Baada ya hapo wakakutana tena mkutano mkuu May 30, ambapo walizindua Ilani, wakabeba wasanii wote kwenda nao. Ndio hiuo siku walisema Wana wanachama million 13
Anyway, kuna kikao kiomja ndio walitangaza kuanza kufanya vikao kwa njia ya mtandao, wengi hamkumbuki hilo na ilikuwa ni kwenye Mkutano Mkuu mmojawapo.

Hlalafu acha kujadili hoja kwa chuki utadhani wewe hujawahi sahau katika maisha yako.
 
CCM ni chama. Na kama chama LAZIMA kiwe na uongozi. Na uongozi wa chama kazi yake ni kukiongoza chama kwa wakati wake na kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za chama kwa wakati husika.

Wasiolijua hilo kuhusu CCM wanabaki kupambana na mtu. Walipambana na Mkapa. Wanapambana na Kikwete. Wanapambana na Magufuli na sasa hivi wanapambana na Mama Samia huku wakiiacha CCM ikiendelea kuimarika!

Ahahahahaha!!
Bandiko hilo lilikuhusu wewe, "'sPecifically', halimhusu mtu mwingine. Nililiweka, nikikulenga wewe, kwa sababu nakujuwa. Sasa usijifanye hukuelewa ulicho elezwa.

Kuimarika kwa CCM chini ya Samia Suluhu Hasaan na GENGE lake, huo utakuwa ni muujiza wa kipekee sana.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utakaofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi, Julai 26, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya CCM, tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, kwa Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM linaeleza kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maandalizi ya mkutano huo, Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM wameelekezwa kuwaelekeza wajumbe wote wa Mkutano Mkuu waliopo katika maeneo yao kuhakikisha wanakusanyika katika ofisi za CCM za Wilaya au Mikoa, kutegemeana na nafasi, ili kushiriki kwa pamoja.

Taarifa hiyo pia imeweka msisitizo juu ya maandalizi ya mazingira ya kufanikisha mkutano huo, ikiwemo kuweka vifaa vya kuoneshea kama televisheni au skrini, viti vya kutosha, na kuhakikisha mazingira ni tulivu pamoja na kuwa na miundombinu imara ya mtandao.

Jambo TV imezungumza na makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa mbalimbali ambao wamethibitisha kupokea tangazo hilo huku wakieleza kuanza maandalizi ya mkutano huo.

Hata hivyo ajenda zenyewe za mkutano hazijawekwa wazi huku kukiwa na tetesi juu ya uwepo wa maamuzi kadhaa mazito yatakayopitishwa na mkutano huo wakati ambao chama hicho kiko katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

View attachment 3417211
Link please so we can participate effectively
 
Back
Top Bottom