GE2025 Kumekucha! CCM yaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa njia ya mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utakaofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi, Julai 26, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya CCM, tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, kwa Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM linaeleza kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maandalizi ya mkutano huo, Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM wameelekezwa kuwaelekeza wajumbe wote wa Mkutano Mkuu waliopo katika maeneo yao kuhakikisha wanakusanyika katika ofisi za CCM za Wilaya au Mikoa, kutegemeana na nafasi, ili kushiriki kwa pamoja.

Taarifa hiyo pia imeweka msisitizo juu ya maandalizi ya mazingira ya kufanikisha mkutano huo, ikiwemo kuweka vifaa vya kuoneshea kama televisheni au skrini, viti vya kutosha, na kuhakikisha mazingira ni tulivu pamoja na kuwa na miundombinu imara ya mtandao.

Jambo TV imezungumza na makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa mbalimbali ambao wamethibitisha kupokea tangazo hilo huku wakieleza kuanza maandalizi ya mkutano huo.

Hata hivyo ajenda zenyewe za mkutano hazijawekwa wazi huku kukiwa na tetesi juu ya uwepo wa maamuzi kadhaa mazito yatakayopitishwa na mkutano huo wakati ambao chama hicho kiko katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

View attachment 3417211
Ameshaogopa hata kuwa-face wanachama ana kwa ana? Kwisa habari yake!
 
Jk hamumuwezi, huu mwanasiasa aliebobea
 
Kama ni kweli basi inawezekana kukawa na mabadiliko wa wagombea wa ngazi za juu. Hususani, Majaliwa kuwa mgombea mwenza na Nchimbi akisubiri uwaziri mkuu. Kwani kile kikao cha January 2025 hakikutarajia Majaliwa hatagombea ubunge, walitarajia ataendelea na uwaziri mkuu. Ndiyo matatizo ya kuteua mapema mno. Busara huwa ni kusubiri hadi dakika za mwisho ukipima upepo unakoelekea.
Unazijua sifa za mtu kuwa waziri Mkuu wa JMT?

Ni lazima awe MBUNGE WA KUCHAGULIWA!!

Nchimbi amechukua fomu ya ubunge jimbo gani?
 
Bandiko hilo lilikuhusu wewe, "'sPecifically', halimhusu mtu mwingine. Nililiweka, nikikulenga wewe, kwa sababu nakujuwa. Sasa usijifanye hukuelewa ulicho elezwa.

Kuimarika kwa CCM chini ya Samia Suluhu Hasaan na GENGE lake, huo utakuwa ni muujiza wa kipekee sana.
Kama unanijua basi usingeliweka maana unanijua. Kwasababu unanijua I'm above you, your family, your father and everybody near you!!
 
Kama ni kweli basi inawezekana kukawa na mabadiliko wa wagombea wa ngazi za juu. Hususani, Majaliwa kuwa mgombea mwenza na Nchimbi akisubiri uwaziri mkuu. Kwani kile kikao cha January 2025 hakikutarajia Majaliwa hatagombea ubunge, walitarajia ataendelea na uwaziri mkuu. Ndiyo matatizo ya kuteua mapema mno. Busara huwa ni kusubiri hadi dakika za mwisho ukipima upepo unakoelekea.
Cabinet yote ya kuanzia 2015 to 2025 ya ccm inatakiwa kupigwa chini,

Ccm ije na mzee mkuchika, Makongoro Nyerere, au Mtaka.

Chadema ije na Tundu lissu kama reforms zitafanyika na wananchi ndo tuhamue kwa kura zetu
 
Mkutano Mkuu una hadhi yake, ndicho chombo kikubwa zaidi kwenye chama au taasisi kinachotoa maamuzi ya mwisho.

Mkutano Mkuu wa CCM una wajumbe takriban 2,000 kutoka mikoa yote Tanzania, unahusisha vitu vingi, kupata taarifa kutoka kila mkoa, wilaya, jimbo, jumuia za chama nk, unahusisha wajumbe kujadiliana, kupongezana, kukosoana, maswali na majibu baadae mkutano kutoka na maazimio ya pamoja. Interaction ya wajumbe uso kwa uso matters a lot.

Haya yote hayawezi kufanyika mtandaoni kwa muda wa nusu saa au saa moja, kingekuwa kikao cha NEC au Kamati kuu inayohusisha wajumbe wachache sawa. Kwanza teknolojia yetu huko vijijini bado duni.

Labda watuambie Mwenyekiti anakuja kutoa taarifa au anahutubia wajumbe lakini sio kutuambia ni Mkutano Mkuu.
 
Back
Top Bottom