GE2025 Kumekucha! CCM yaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa njia ya mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Taratibu za kuitisha Mkutano Mkuu wa CCM ziko kwenye Katiba ya CCM, toleo la 1977 (kama lilivyorekebishwa). Kwa muhtasari:

1. Wito wa Mkutano Mkuu
  • Huitishwa na Mwenyekiti wa Taifa kupitia Katibu Mkuu wa CCM.
  • Wajumbe hupewa taarifa kwa maandishi angalau siku 30 kabla ya tarehe ya mkutano (isipokuwa kama ni wa dharura).

2. Aina za Mikutano
  • Mkutano Mkuu wa kawaida: Hufanyika kila baada ya miaka mitano.
  • Mkutano Mkuu Maalum: Unaweza kuitishwa wakati wowote kwa sababu maalum kama chama kinahitaji kufanya maamuzi ya haraka (mfano: mabadiliko ya katiba au uteuzi maalum).

3. Wajumbe wa Mkutano Mkuu
Ni pamoja na:
  • Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Taifa
  • Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
  • Wenyeviti wa CCM mikoa
  • Wawakilishi kutoka mikoa, wilaya, jumuiya za chama n.k.

4. Ajenda
Ajenda kuu huandaliwa na Sekretarieti ya CCM, hupitishwa na Halmashauri Kuu kabla ya kuwasilishwa kwa wajumbe.

5. Uamuzi
Maamuzi hufanywa kwa kura za wazi au siri, kulingana na suala.

Unataka taratibu hizi kwa muktadha wa uchaguzi, dharura, au mabadiliko ya katiba? Naweza kuzifafanua zaidi.
Maboresho ya katiba ya ccm ya 29 may 2025 uliyazingatia?
 
Karma inajirudia walichofanya kwa lissu naona wanakifanya kwao
 
Mabadiliko ya katiba ya ccm yaliyofanywa 29 may 2025 uliyazingatia?

Endapo mkutano kwa njia ya mtandao utafanyika basi mfahamu ya kuwa:-

Mama 3 - 0 Polepole.
 
Umezaliwa 2009 au 2005?!!!
Hivi Kuna chadema Bado kwa unavyoona (maana naona hapa mwenyewe inahitaji vikao vya ccm mpaka unakasirika ukionA vinachelewa)?!!🤣🤣🤣🤣
Mipango ya ndani huijui mbwiga wewe..........unapoambiwa siasa ni sayansi uelewe.
Kwani CAHADEMA ni nini?
 
Wakuu

Hivi ni nini kinaendelea huko CCM? Mbona ni kama mfumo umepaniki wakuu?

Baada ya kuhairishwa kwa vikao leo wameitisha mkutano wa dharura. Nini kinaendelea?

=======

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utakaofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi, Julai 26, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya CCM, tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, kwa Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM linaeleza kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maandalizi ya mkutano huo, Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM wameelekezwa kuwaelekeza wajumbe wote wa Mkutano Mkuu waliopo katika maeneo yao kuhakikisha wanakusanyika katika ofisi za CCM za Wilaya au Mikoa, kutegemeana na nafasi, ili kushiriki kwa pamoja.

Taarifa hiyo pia imeweka msisitizo juu ya maandalizi ya mazingira ya kufanikisha mkutano huo, ikiwemo kuweka vifaa vya kuoneshea kama televisheni au skrini, viti vya kutosha, na kuhakikisha mazingira ni tulivu pamoja na kuwa na miundombinu imara ya mtandao.

Jambo TV imezungumza na makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa mbalimbali ambao wamethibitisha kupokea tangazo hilo huku wakieleza kuanza maandalizi ya mkutano huo.

Hata hivyo ajenda zenyewe za mkutano hazijawekwa wazi huku kukiwa na tetesi juu ya uwepo wa maamuzi kadhaa mazito yatakayopitishwa na mkutano huo wakati ambao chama hicho kiko katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

View attachment 3417205
Kunyukana kwa CCM ndio pona ya Tanzania. Sasa hivi hawaaminiani wakora wakubwa. Umoja wa wakora haujawahi kuwa wa milele.
 
Posho zimekata?Na lazima tuwadukue ili tumzomee jini Kabula live
Watu wa chudai tafadhali tunawaomba mkae mbali/ mtuvumilie kidogo hadi kikao kiishe. Msije kutupandishia mapicha picha ya ngono kwenye screen wakati mwenyekiti yupo live anahutubia.

Hamchelewi nyie.
 
Huyu mama anatia huruma Sana unawezaje kulazimisha kuongoza watu ambao hawakupendi?
Mkuu,

Kwani wakoloni wa kizungu walipokaa Africa miaka zaidi ya mia mbili mlipenda?

Sisiem ni kama UKIMWI tuishi nayo hivyo hivyo Huku tukitumia ARV kupunguza makali. Si tumeshindwa kuitoa?
 
Mkutano Mkuu una hadhi yake, ndicho chombo kikubwa zaidi kwenye chama au taasisi kinachotoa maamuzi ya mwisho.

Mkutano Mkuu wa CCM una wajumbe takriban 2,000 kutoka mikoa yote Tanzania, unahusisha vitu vingi, kupata taarifa kutoka kila mkoa, wilaya, jimbo, jumuia za chama nk, unahusisha wajumbe kujadiliana, kupongezana, kukosoana, maswali na majibu baadae mkutano kutoka na maazimio ya pamoja. Interaction ya wajumbe uso kwa uso matters a lot.

Haya yote hayawezi kufanyika mtandaoni kwa muda wa nusu saa au saa moja, kingekuwa kikao cha NEC au Kamati kuu inayohusisha wajumbe wachache sawa. Kwanza teknolojia yetu huko vijijini bado duni.

Labda watuambie Mwenyekiti anakuja kutoa taarifa ya jambo fulani lakini sio kutuambia ni Mkutano Mkuu.
Yote hiyo ni kutaka kutafuta. Namna ya kulazimisha mambo
 
Ataendesha Kikao kutokea Ikulu ya Kiximkazi.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utakaofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi, Julai 26, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya CCM, tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, kwa Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM linaeleza kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maandalizi ya mkutano huo, Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM wameelekezwa kuwaelekeza wajumbe wote wa Mkutano Mkuu waliopo katika maeneo yao kuhakikisha wanakusanyika katika ofisi za CCM za Wilaya au Mikoa, kutegemeana na nafasi, ili kushiriki kwa pamoja.

Taarifa hiyo pia imeweka msisitizo juu ya maandalizi ya mazingira ya kufanikisha mkutano huo, ikiwemo kuweka vifaa vya kuoneshea kama televisheni au skrini, viti vya kutosha, na kuhakikisha mazingira ni tulivu pamoja na kuwa na miundombinu imara ya mtandao.

Jambo TV imezungumza na makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa mbalimbali ambao wamethibitisha kupokea tangazo hilo huku wakieleza kuanza maandalizi ya mkutano huo.

Hata hivyo ajenda zenyewe za mkutano hazijawekwa wazi huku kukiwa na tetesi juu ya uwepo wa maamuzi kadhaa mazito yatakayopitishwa na mkutano huo wakati ambao chama hicho kiko katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

View attachment 3417211
Utekaji na
Kufungia kanisa lilikuwa kosa kubwa sana na Mungu kashatuma upepo wa kisulisuli
Wananuka sio kawaida wanatafuta utulivu unakosekana mwisho kuna mtu ataanza kuongea pekeyake
 
Back
Top Bottom