Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Bora Baraka Shelukindo kapotelea Kenya maana hii issue ingetokea chini yake, na yeye ingemletea shida kwenye reputation yake. Halafu Lamata toka nisikie Juakali imeanza hadi leo haijaisha tu au anapata mgao mzuri 😁
 
Binafsi ofisini kwetu nimebaki mtazamaji tu. Watu wanapiga vibaya, nimechagua kuishi maisha yangu ninayoyaweza na kuyamudu.

Ubaya wa kuongeza kipato kwa wizi ni kuishi maisha ya stress, maana pale unapopiga pakizibwa kidogo unaanza kuhaha kwa kuzoea maisha makubwa yasiyoendana na kipato chako.
 
Pole sana Ila ndio maisha ya ofisini hayo. Nilishafurahishwa hamu sina Ila kwa wazungu kuna unafuu mkubwa sana tofauti na kwa races nyingine za business as usual
 
Ajabu wala rushwa wanapewa sifa kedekede.

Angalia katika huu uzi, wamepata watetezi!
Shem ukipata chimbo chukua chako mapema hata wakikutimua uwe umeshatoka kimaisha.

Dunia haina usawa wala haki.

Ukisubiri upewe utachelewa

Anayekuasa usiibe yeye anakwapua.

To win in life one has to break the rules πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Unafaa sana lakini dah pole
 
Hivi ndivyo mijadala inatakiwa kuwa, unabisha ukiwa na hoja za maana.

Nimekubali Mkuu, uko sahihi kwa upande wako.
 
Nimeelewa sasa.

Hamna namna, hata mambele creators/producers wananyonywa na hawa wasimamizi....

Budget ya kutengeneza filamu ni kubwa, producers hawana namna zaidi ya kunyonywa. Ila ni mbaya.
Kumbe ulikuwa hujaelewa mwanzo?

Isike amewaokoa wenzie pakubwa sana, nahisi hata Lamata alishachoka ndio hakuwa tu jinsi.
 
Ila Nchi za Afrika na Rushwa ni kama Pete na Kidole

Kama hadi Yuda Eskariote alikula rushwa ya vipande 30 ili kumsaliti Masihi ndiyo iwe kwa huyo Bibie?

Ila nimependa ulivyomaliza habari yako
"Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini"........

Utasema warumi 🫑
 
Bora Baraka Shelukindo kapotelea Kenya maana hii issue ingetokea chini yake, na yeye ingemletea shida kwenye reputation yake. Halafu Lamata toka nisikie Juakali imeanza hadi leo haijaisha tu au anapata mgao mzuri 😁
Lamata hana hiyana, kaamua kutoa ushirikiano ndio maana Juakali haipishani na Isidingo, haiishi!

Sasa si bora Jua Kali, Huba je?
 
Lamata hana hiyana, kaamua kutoa ushirikiano ndio maana Juakali haipishani na Isidingo, haiishi!

Sasa si bora Jua Kali, Huba je?
Bora juakali ilianza kwa setting nzuri na mastar wengi sana kiasi ilikuwa huwezi kuimiss.
Ila hii huba niliikuta watu wanaangalia na sikuelewa wanaangalia nini maana story line sikuielewa na hata uigizaji wenyewe

Labda Nicole joeberry anawahamasisha maana ana fans wa kutosha
 
Shem ukipata chimbo chukua chako mapema hata wakikutimua uwe umeshatoka kimaisha.

Dunia haina usawa wala haki.

Ukisubiri upewe utachelewa

Anayekuasa usiibe yeye anakwapua.

To win in life one has to break the rules πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Shem, kitu wizi ndio nimeshindwa maishani!

Nimelelewa vyema, udokozi ulinipitia kando utotoni hadi hivi sasa.

Uaminifu kazini ni kila kitu, napenda amani hivyo siwezi kuipoteza kwa tamaa.

Halafu hao wanaoiba sijui hela wanapelekaga wapi masikini! Sijigambi ila nina maisha bora kuwazidi!
Nafikiri ni vile Mungu anabariki kidogo changu cha halali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…