Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

Sijajua kwanini hili swala la kufanyiwa interview linaibua mijadala ya namna hii kwasababu mtu huyo aliyesoma PCB na aliyesoma PCM wote walichakaa, yeye alisoma miaka mitano na mwenzie alisoma miaka minne kwahiyo kuchakaa wote walichakaa ila hii sio point ya msingi ya hii comment yangu ila nnachotaka kusema ni kwamba...

Kufanya interview haimaanishi kwamba wewe hauna ubora kwenye field uliyosomea ila kuna nyakati hizi interview zinafanywa kutokana na uwingi wa watu walioomba hizo nafasi na ufinyu wa hizo nafasi zenyewe zilizopo kwahiyo ili game iwe ya haki basi yeyote ambae anajihisi yuko na sifa za kufanya kazi atatuma maombi hata mkituma watu million kwenye nafasi alufu kumi zilizotoka wote mtafanyiwa mchujo hadi hao wahitajika watakapo patikana.

Sasa hapa shida ni kwamba....

Walimu na madaktari wengi wa nchi hii mlizoea kitonga ila lazima muelewe kwamba wasomi katika hii nchi wanaongezeka na hii inapelekea ufinyu wa maeneo ya kuwaweka moja kwa moja wahitimu wote wa hizo kada kama ambavyo mwanzo ilikua.

Kwahiyo ifike mahali tukubaliane na hali halisi na tufuate mabadiliko yanavyotaka.

And you know what?...

Atleast now hata hao vijana unaosema wanavunjwa moyo huko chuoni watasoma course ambazo wanazihitaji sio kusoma kwa kufuata trend ya ajira.

And the thing is...

Mtazoea tu ndugu zangu and karibuni kwenye ulimwengu wa interviews, sisi wenzenu tumeshazoea and tunajionea kawaida tu kwakweli.

NB:
Kama yuko mwalimu au daktari ambae anataka arushe mawe kwenye hii comment naomba atafakari kwanza, kwa maana sina hatia baba wa watu 😆😆😆.
 
Sasa serikali mna somesha madaktari kwa pesa nyingi, kumbuka hii kada Ina wapungufu wa waataalumu wa afya kila idara.

Doctor amethibitishwa na MCT. Lakini Tena kufanyiwa interview kwenye hospital ya wilaya TU, jamani.

Mimi na shauri interview wafanyiwe kwenye hospital kubwa ( mzena). kwa ajili ya kuwaandaa ma doctors bingwa TU.

Hivi tunavyo jadili tayari kimeshaumana huko kwenye interview.
Ma doctors tz ni wachache , wanatakiwa wote waajiriwe ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wetu.
 
Interview ni muhimu sana asee sema sasa kwa Tanzania hii interview zina mambo mengi sana tena ya kipuuzi tu. Imagine mtu anaweza akakuchukia tu just kwa muonekano wako na ukakosa kazi hata kama vgezo vya umahiri wa kazi unavyo. Wenzetu wazungu ndio wanajua nn hasa maana ya interview ila sisi waafrica ni upumbavu mtupu.
 
Acheni kulialia.. ndiyo Dunia ya sasa ipo hivyo... Kama umuhimu kila fani inaumuhimu
 
Huna unachojua ,Madokta ni wengi sana sikuhizi
 
Moja ya dhumuni la interviews ni kuangalia utimamu wa akili pia.
 
Nimekuelewa. Sasa kama kuna nafasi 20 na walioomba ni 200 na wote wanepitia huo mchakato. Unawachaguaje hao 20 kutoka 200?
Chief, sipingi usaili ila naomba nikuswalike swali

Hivi lengo la usaili ni kuchuja idadi au ubora?

Kama ni idadi vipi mtihani wakifaulu wote watatumia kigezo gani kingine kupata hao 20 out of 200
 
Chief, sipingi usaili ila naomba nikuswalike swali

Hivi lengo la usaili ni kuchuja idadi au ubora?

Kama ni idadi vipi mtihani wakifaulu wote watatumia kigezo gani kingine kupata hao 20 out of 200
Ubora. Njia yoyote ile as long ni transparent na inaleta fairness.
 
Ubora. Njia yoyote ile as long ni transparent na inaleta fairness.
Kwahiyo kigezo cha idadi hakina mantiki hapo, kwamba eti kwakuwa wanaohitaji ajira ni wengi halafu nafasi ni chache hili halihusiani na interview
 
Chief, sipingi usaili ila naomba nikuswalike swali

Hivi lengo la usaili ni kuchuja idadi au ubora?

Kama ni idadi vipi mtihani wakifaulu wote watatumia kigezo gani kingine kupata hao 20 out of 200
Swali gani la kijinga hivi.
Kwani wote wanapata 100% Utumishi wanapanga rank kulingana na ufaulu wa interview, wanaanza kuchukua toka juu ( highest mark) mpaka kufikia idadi inayotakiwa kulingana na nafasi wanaobaki wamefaulu lakini hawajapata nafasi kwa sababu ya competition wanaingia database, nafasi zikipatikana wanachukuliwa.
Nami nilipata nafasi kwa njia hii.
Mfumo wa Utumishi wa recruitment uko perfect, labda kama usipofuatwa inavyotakiwa.
 
Ukweliii mtupuuu.
 
Nikweli ni swali la kijinga lakini ungejibu kwa welevu

Kwahiyo lengo la usaili ni kuchuja ubora au idadi?
 
Shida si usaili kwa maana usahili ni lengo kupunguza watu mfano MD katika usaili wapo 4000 wanataka 700 changamoto nayoona usahili umejaaa wakuda nilishawahi kwenda ktk usahili wa MDH sina hamu tena na ajira yaan kumbe ilikuwa kanyaboya watu walikuwa washaandaliwa kumbe na majina yalikuwa tayari kumbe sie tulikuwa tunazugwa tulienda mm na rafiki angu ambaye baba ake anamjua sijui DMO yeye akapita baada ya kupita ndio aliniambia Baba yake alimfanyia mpango
Hapo katika usaili ndugu wenye connection wanaasilimia kubwa sana kupita mwenzangu na mm kajamba nani utaangukia pua
 
Kwahiyo unataka watumie kigezo gani kutowaita wengine ambao wameomba na wanavigezo vya kupata hiyo kazi ?
 
Kuchuja idadi ili wapate idadi kulingana na nafasi zilizopo.
Kwahiyo sio ubora tena ni idadi?

Sasa vipi wote wakiscore high marks watakaowekwa kwenye data base watatumia kigezo gani kuwaita kazini endapo nafasi ikitokea let's say nafasi moja?

Na kama lengo ni idadi tunakubaliana na mtoa mada kuwa ubora washauchuja baraza na taasisi za elimu kama shule, hiki kinachofanyika ni sarakasi tu za kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…