Kumfunga Maria jela miaka 22 kisa nyama ya swala ni matokeo ya kuwa na wanasheria waliokosa hekima na busara

Mbunge
Mbunge wa Kishapu alifungwa miaka mingapi vile nikumbushe?
 
Hivi umekijua nilichoandika au umevurugwa na mvua?

Mtu analima shambani kwake unfortunately tembo anatokea anamuua, je , hapo inahitajika elimu ya kuishi na tembo?

Tembo wamekuwa wengi sasa wamewafuata wanadamu wanakula mazao ya watu huku waathirika wakilipwa fidia kiduchu tena kwa kuchelewa na wakati mwingine hulipwi.

Mjomba wangu kauwawa na tembo mchana kipindi yuko shamba analima. Tembo wavunwe au wauzwe ili kutuamini uhai wa watu.

Watu wanakufa serikali inatoa million 1 huku wewe ukiua tembo miaka 50 jela na faini sh. 50 ml.
 
Hii sio haki nilipoisoma hii habari Kwa Millard Ayo machozi yalinilenga walahi. Umasikini ni kitu kibaya Sana jamani hivi kweli wale waliokua wanaiba wanayamapori kwenda nje ya nchi wamefanywa nini?
Huyu hakimu aliyetoa hii hukumu ana vina Sana na shetani siamini kama ana Moto wa kibidamu
 
Naamini huyo mama angekua ndugu yako usingeandika hizi pumba. Kama ni Sheria iwabane na wale wanaosafirisha wanyama kwenda ughaibuni sio mama masikini asiye na nguvu hata ya kuua sungura
 
umlinde binadamu mwenye akili zake, funga hata miaka 100, pumbavu kabisa. Na ujue wanyama ktk himaya yao ni bora kuliko we kenge mtu
Kaeni karibu na majority ya watanzania muone Wana upeo dini kiasi gani,elimu mmewanyima,elimu ya sheria hamuwapi,mmeshindwa kuwaondolea umasikini,mmeshindwa hata kuwapa huduma za wanasheria Bure,mnawafunga tu!!..watanzania wengi wajinga,hawajui kitu
 
Mahakama
Polisi
Vyombo hivi vimewekwa kuwanyoosha masikini havihusiki na watu wa daraja la 2 na 1
 
mnafki tu wewe
Wewe mbona unabwabwaja sana kwani wew ndiye hakimu uliemuhukumu mubibi wa watu!? Hoja siyo msumeno au mukisu wa sheria, hoja ni kwa nin vyombo vya dola vinashughulika wa watu wenye makosa madogo kama hayo ya mubibi wa watu na kilo tisa(9) za nyama ya swala ambayo hata haifiki thamani ya milioni moja huku majambazi makubwa yanayoiibia nchi matrion na matirion na fedha kama yalivyotajwa na CAG yakiendelea kuvimba mtaani huku yakitembelea V8 na ulinzi wa hali ya juu ukisindikizwa na ving'ora.
 
Waarabu wanawaswaga hao swala bila kuchukuliwa hatua yoyote!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mambo madogo madogo kama haya nadhani huwa yanatakiwa kumalizwa hukohuko eneo la tukio kabla hayajafika huko mahakamani au kwenye vyombo ya juu vya sheria.

Sitaki kuamini kwamba huyu mama angeonywa kwa faini aua ka adhabu nyingine inayoendana na kipato chake pamoja afya yake kwamba angegomea hiyo adhabu.


Some times sheria huwa zina kifungu cha kuangalia ubinadamu kwanza ndipo hukumu katili dhidi kosa kam hilo kutolewa. Anyway,Mungu akuongoze vyema huko gerezani mama mpambanaji🙏🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…