Yaani unasema kweli, huyo mwana dada kakaa jela miaka 22?Miaka 22 kwa nyama yenye thaman ya laki tisa?
Na, kosa lake ni hiyo nyama ya swala?
Na katika miaka yote hiyo, 22, hapakuwepo hata na KUDURUVU (Review); wala ile tume ya msamaha aliyokuwa akiiongoza Marehemu Mrema, haikuweza hata kumfikiria?
Mkuu 'Carlos', nimejikuta nashindwa kabisa hata kukupa 'like' tu ya taarifa ya namna hii, kwa sababu hakuna kitu cha 'ku-'like' kwenye dhuruma ya namna hii.
Nchi hii imechelewa sana kupata mapinduzi za kuondoa utawala wa namna hii!