Kumfunga Maria jela miaka 22 kisa nyama ya swala ni matokeo ya kuwa na wanasheria waliokosa hekima na busara

Kumfunga Maria jela miaka 22 kisa nyama ya swala ni matokeo ya kuwa na wanasheria waliokosa hekima na busara

Hivi wale wageni wanaowinda nyama pori,si wanazila sana hizi nyama.

Watu wanapiga ma b ya kutosha ya walipa kodi,yani hii hali inamfanya kila mtu kutamani kuwa kibaka

Tanzania ,tanzania.
 
Hakimu gani anakua kama shetani aliyevaa ngozi ya mtu.., angekuwa mwanae angemfunga 22 yrs wakati sheria imetoa nafuu na mwanya kwa hakimu kutumia busara? Mdada huyo anaonesha sio jangili, labda alipewa tu.., pia ni masikini sana anaonekana, ni shida tu...View attachment 2807065
Kiukweli hakuna uhalisia wa kosa na adhabu..
Swala hao wapo kibao tu mbugani huko
 
Hawa ni aina ya mahakimu ambao Sheria haipo kichwan, ni wapuuzi wanaotembea na tukanuni twaao kichwan,, Sina shaka ukifatilia hukumu za huyu mpuuzi, utagundua zote zinafanana.

Hivi Kwa hali ya kawaida, mwanamke alochoka kama huyu, hata km kakukutwa na nyama ya Swala, ni wakumfunga miaka 22?

Kwa mwanamke, kitendo tu cha kusota mahabusu kipindi chote cha kesi, kimetosha kumfundisha
Nimesoma mahala Peter Kibatala kasema apewe details za huyo mama ili amsaidie kwenye rufaa..
 
Hatafungwa kifungo hicho. Ila lazima umma utangaziwe maamuzi ya mahakama. Huyu atakwenda kukaa mahabusu kama wiki tu kisha atatoka ili next time awe makini na wanyama pori

Sheria ni lazima ziwe kali ili kuwalinda wanyana pori sababu tukicheka na hawa raia wadogo wanaozunguka mbunga miaka 10 ijayo wakiwekeza maisha yao kwa hao wanyama hamtaamini namna namna watawatokomeza pia usisahau swala la magonjwa ya mlipuko kutokana na kula nyama ambazo hazijathibishwa ubora wake.

Kwa kifupi tusiwe wepesi sana wa kuleta hisia katika maswala ya kisheria. Huu mchezo wa kuleta hisia ndio chanzo cha rushwa na utendaji mbovu wa mamlaka za serikali sababu wanainchi ndio mstari wa mbele kuwatetea wakosaji sababu wanatia huruma wakitiwa mbaroni.
Sijui unaongea kitu gani wewe, yaani hakimu atoe ruling, tena mbele ya umma halafu mtu awekwe mahabusu? Mama tayari yuko gerezani acha kudanganya watu. Pili hoja iliyopo ni kwamba mafisadi papa wanapigwa hivyo vifungo au ni masikini tuu? Waliosafirisha twiga walifungwa? Yule mama tajiri aliyekamatwa na meno ya tembo alifungwa?? Mama kashikwa na vipande sijui 10 vya swala je huko porini wanaliwa swala wangapi na chui, simba na fisi? Bora ungeniambia majangili 10 walikamatwa na swala 50 wamekamatwa huko kwenye hifadhi badala ya kumkamata mama wa watu.
 
Kuna kitu tunakosea sana kuhusu wanyama pori. Raia hawana elimu ya kuishi nao pale wanapoingia mazingira yao au wanyama wanapokuja mazingira yao.

Nadhani tunahitaji wataalamu wanaowafahamu hawa wanyama vema ili raia waweze kuelekezwa namna ya kuishi nao na kuweza ku:co exist.


Mnyama kama tembo akija eneo la makazi ya watu basi amepata harufu ya chakula kama mahindi, viazi, mihogo na kadhalika. So raia wanatakiwa kujua yule ni mnyama kitendo xha kumletea shari au kutaka kumfukuza itamlazimu kujitetea na ndipo hapo madhara hutokea.

Nimeshaona video ya tembo wanaokwenda kwenye hoteli ya kitalii na wapishi huwa wanaandaa mazaga wanawawekea hapo pembeni maana walifumua paa la jiko na ndipo hapo chakula wanaweka so wakija wanakula wakiwa wamesimama kwa nje na kupenyeza mikonge yao kwa ndani ya chumba cha jiko.

Imeshakuwa mazoea na hao tembo huwa wanakuja hapo mara kwa mara. Aiseee ukiwa muoga huwezi kukaa hilo eneo maana unakuta bonge la tembo linachungulia juu ya paa linaingiza mkonga wake kupapasa msosi. Halafu wanakuja kimya kimya.

Tembo anaweza pita nyuma ya jengo na usijue kama wapo nyuma ya nyumba hapo sasa tokea huko nyuma bila mahesabu utashangaa umempiga kikumbo. Me wakisema sehemu fulani tembo huwa wanapita au kuja sana huwa sishauri mtu aende hayo maeneo kama ana umakini mdogo maana ukizingua wanapita na wewe na kukudedisha ni dakika chache tu.
Umetoka zako sijui mweka au Pasiansi wildlife college lakini bado hujui real situation on the group... Nenda katembelee wanavijiji huko Serengeti ukae huko miezi 6 halafu uje hapa na story zako za ku co-exist...
 
Kilo 22 si ni nyama ya kuchoma na kutengeneza rosti kidogo kula na mumewe na watoto wake??

Ni uduanzi sana majitu ya ripoti ya CAG yanatingisha makalio kwa raha zao hawajaenda sero wala jela.
Siyo kilo 22 ni kama kilo 6 au 7 maana ni vipande kama 10 hivi... Hiyo 22 ni miaka aliyohukumiwa...
 
nenda jela wewe kwa niaba yake km umemwonea huruma, mnafki mkubwa sheria ni msumemo haiangalii hali ya mtu. Sheria haijatungwa kwa maskini wala tajiri. Km we unajijua ni maskini tii sheria. Ufanye uhalifu halafu ndio uachwe kisa maskini? We kweli ni kenge tena mnafki tu unatafuta umaarufu wa kilofa.
Hiyo sheria unayoiringia alitunga mkoloni..
 
inabidi wanasheria wamsaidie huyo mama ni uonevu sana, hawa mahakimu wa sisiem kazi kuwaonea mafukara tu,
Hakuna cha wanasheria wala nini, Rais amsamehe tu, majangili ya kiarabu yamejaa tele huko Loliondo, wakayakamate hayo
 
Tuache mambo ya kuwa na mihemko,ametenda kosa acha sheria ifanye yake
 
Hatafungwa kifungo hicho. Ila lazima umma utangaziwe maamuzi ya mahakama. Huyu atakwenda kukaa mahabusu kama wiki tu kisha atatoka ili next time awe makini na wanyama pori

Sheria ni lazima ziwe kali ili kuwalinda wanyana pori sababu tukicheka na hawa raia wadogo wanaozunguka mbunga miaka 10 ijayo wakiwekeza maisha yao kwa hao wanyama hamtaamini namna namna watawatokomeza pia usisahau swala la magonjwa ya mlipuko kutokana na kula nyama ambazo hazijathibishwa ubora wake.

Kwa kifupi tusiwe wepesi sana wa kuleta hisia katika maswala ya kisheria. Huu mchezo wa kuleta hisia ndio chanzo cha rushwa na utendaji mbovu wa mamlaka za serikali sababu wanainchi ndio mstari wa mbele kuwatetea wakosaji sababu wanatia huruma wakitiwa mbaroni.
askari wanyamapori waliomkamata ndio unatakiwa kuwalaumu. sio wanasheria. mtu kakamatwa na nyama ya swala, na yeye anakiri ni ya swala, na anajua kuwa nyama ya swala kukamatwa nayo ni kosa, analetwa mahakamani, anakiri, sheria inasema 22 yrs, unafikiri mwanasheria au hakimu angefanya nini zaidi ya kumlima miaka na adhabu hiyo sio optional, mtu akitiwa hatiani lazima miaka hiyo mtu atumikie. cha kuwashauri, aidha alipiwe faini atoke, au asubiri rufaa, ama la kama wanaona kuna makosa, High court waitishe jalada wafanye revision, wamwachie kama kuna mwanya.

Au la, presidential pardon ifanyike, though sidhani kama samia atatoa msamaha kwa mtu aliyekutwa na nyamapori kwasababu ndani wamejaa watu wengi wa aina hiyo watakaolalamika kwamba why only huyu wakati kuna watu wana hali mbaya kuliko huyu huko gerezani hawana hata tumaini na wameshatumikia kifungo cha kutosha.

Mimi mwenyewe nina ndugu zangu kibao gerezani na ni wanavijiji. hizi mavitu mara nyingi wanafungwa wanakijiji watu masikini kabisa kwasababu hawajui kujieleza, hawawezi kuajiri wakili, hawana pesa za kuhonga tangu upelelezi hadi mahakamani. kwa tulioshinda mahakamani ndio tunajua ukweli huu.
 
Jamani tupazeni sauti huyu mama asaidiwe huyo hakimu aliemfunga mama yake kamsomesha kwa hela za kudanga lakini bado haoni uchungu.
 
askari wanyamapori waliomkamata ndio unatakiwa kuwalaumu. sio wanasheria. mtu kakamatwa na nyama ya swala, na yeye anakiri ni ya swala, na anajua kuwa nyama ya swala kukamatwa nayo ni kosa, analetwa mahakamani, anakiri, sheria inasema 22 yrs,unafikiri mwanasheria au hakimu angefanya nini zaidi ya kumlima miaka na adhabu hiyo sio optional, mtu akitiwa hatiani lazima miaka hiyo mtu atumikie. cha kuwashauri, aidha alipiwe faini atoke, au asubiri rufaa, ama la kama wanaona kuna makosa, High court waitishe jalada wafanye revision, wamwachie kama kuna mwanya. au la, presidential pardon ifanyike, though sidhani kama samia atatoa msamaha kwa mtu aliyekutwa na nyamapori kwasababu ndani wamejaa watu wengi wa aina hiyo watakaolalamika kwamba why only huyu wakati kuna watu wana hali mbaya kuliko huyu huko gerezani hawana hata tumaini na wameshatumikia kifungo cha kutosha. mimi mwenyewe nina ndugu zangu kibao gerezani na ni wanavijiji. hizi mavitu mara nyingi wanafungwa wanakijiji watu masikini kabisa kwasababu hawajui kujieleza, hawawezi kuajiri wakili, hawana pesa za kuhonga tangu upelelezi hadi mahakamani. kwa tulioshinda mahakamani ndio tunajua ukweli huu.
Wewe ulishindwaje kuwasaidia hao Ndugu zako kisheria?? Ulipaswa kusoma na kuielewa mada. Mafisadi wanadunda mitaani, waliokamatwa na silaha za ujangili wako mitaani. Waliowasafirisha nje twiga wakiwa hai wanadunda mitaani bila hofu.
 
Wewe ulishindwaje kuwasaidia hao Ndugu zako kisheria?? Ulipaswa kusoma na kuielewa mada. Mafisadi wanadunda mitaani, waliokamatwa na silaha za ujangili wako mitaani. Waliowasafirisha nje twiga wakiwa hai wanadunda mitaani bila hofu.
Mara nyingi tu unakuja kusikia ndugu yako tayari yupo gerezani, na wakati mwingine ushahidi unakuwa mkali dhidi yake anafungwa. hoja hapa sio kufungwa au kutokufungwa, hakuna ubishi kwamba huyo mama amekamatwa na nyama, shida ni adhabu, watu wanaona yaani kaswala tu ndio mtu aende gerezani? bila kujua kuwa sheria hiyo wao wenyewe kupitia wabunge wao wameitunga na wao wenyewe kupitia wabunge wao wanaweza kushinikiza ifutwe au irekebishwe. pia, watu wanachanganya hisia na sheria. havichangamani.
 
Back
Top Bottom