askari wanyamapori waliomkamata ndio unatakiwa kuwalaumu. sio wanasheria. mtu kakamatwa na nyama ya swala, na yeye anakiri ni ya swala, na anajua kuwa nyama ya swala kukamatwa nayo ni kosa, analetwa mahakamani, anakiri, sheria inasema 22 yrs,unafikiri mwanasheria au hakimu angefanya nini zaidi ya kumlima miaka na adhabu hiyo sio optional, mtu akitiwa hatiani lazima miaka hiyo mtu atumikie. cha kuwashauri, aidha alipiwe faini atoke, au asubiri rufaa, ama la kama wanaona kuna makosa, High court waitishe jalada wafanye revision, wamwachie kama kuna mwanya. au la, presidential pardon ifanyike, though sidhani kama samia atatoa msamaha kwa mtu aliyekutwa na nyamapori kwasababu ndani wamejaa watu wengi wa aina hiyo watakaolalamika kwamba why only huyu wakati kuna watu wana hali mbaya kuliko huyu huko gerezani hawana hata tumaini na wameshatumikia kifungo cha kutosha. mimi mwenyewe nina ndugu zangu kibao gerezani na ni wanavijiji. hizi mavitu mara nyingi wanafungwa wanakijiji watu masikini kabisa kwasababu hawajui kujieleza, hawawezi kuajiri wakili, hawana pesa za kuhonga tangu upelelezi hadi mahakamani. kwa tulioshinda mahakamani ndio tunajua ukweli huu.