Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Niliwahi kushuhudia boss wangu akitembelewa ofisini na meneja wa tawi la CRDB pamoja na wafanyakazi sita wakimwomba akope angalau 5 billions. Ana shule ya msingi na sekondari pamoja na kampuni ya ujenzi. Kwa haraka haraka ana nyumba zaidi ya 70 hapa Dsm bado Arusha, Dodoma na Moshi mjini. Nyie endeleeni kuweka hela UTT; na bondi mkidhania serikali ya tanzania ni kama ya serikali za Umoja wa ulaya.
 
Badala ya kuwakashifu wanaoweka pesa utt na bond ni vyema ukaeleza kwa hoja zilizo na mashiko kwamba kwanini john atoe pesa zake utt/bond ajenge majumba na asubiriwe na crdb kukopeshwa
 
Nna kisoma story kama hz, hu
Nikisoma story kama hz, huwa naziona za kufikirika tu, kwanza hazina ualisia, maana wasimuliaji hawajiweki wazi,
Pili kuna matajiri wakubwa, walionufaika na , nyumba na ardhi,Donald Trump, William Ruto, unawezaje kusema ardhi sio investment, wakati akili kubwa zimewekeza huko?
Kuna familia za mkubwa mmoja, kule dar, zina miriki majumba, apartment za kifahari kibao, na hayo majumba, yamepangishwa kwa taasisi kubwa kubwa tu, balozi, UN,
Niki Jenga nyumba Leo kwa 100M, nikaipangisha kwa millions 6 kwa mwaka,itachukua miaka kama 20 kurudisha pesa, kwa, mie dingi wa miaka 37! May be nitakufa kabla pesa hazijarudi! Lakini kwa binti yangu wa miaka 12,huu mjengo kwake ni faidi kwa 100%
 
Nikiwa mdogo nilikuwa na mawazonkama Yako mtoa mada. Niliamini kwenye biashara na niliona kuwekeza pesa kwenye nyumba ni kupoteza muda.

Ila ilifika mahali, nimepata biashara kubwa na Sina fedha, nilienda bank kuomba support. Ukiachilianmbali mzunguko ilikuwa vizuri, bado Wakataka dhamana. Sikuwa nayo.

Mwaka jana nimeingia kwenye ujenzi, ikatokea biashara kubwa. Jengo likawekwa dhamana. Bank hawakujifikiria mara mbili kunisupport.

Ila changamoto ni kwamba hawakupi mzigo zaidi ya thamani ya dhamana Yako. Nikaanza kuelewa kwamba, build as much houses as you can, utazitumia kama dhamana kupata pesa in a lump sum ukiwa na kazi kubwa ukiachana na kukusanya mia mbili mia mbili za Kodi.

Sasa unakuta nyumba ya kwanza Ina thamani ya Mil 100, unakazi ya Mil 200. Utaanza kuona umuhimu wa kuwa na nyumba mbili ili qualify kupata kiwango unachohitaji. Ila ipo siku utapata kazi ya Billion, utagundua uwezo wa kufanya unayo, ila bank hawawezi kukusupport kwa vile dhamana hairuhusu. Happy ndipo utaona umuhimu wa kuwa na nyumba hata 100 hapa mjini uziweke dhamana.

So ndugu yangu,....kama wewe ni mfanyabiashara, usiwekeze sana kwenye stock, Jenga. Siku ikihitajika pesa ya kuagiza stock ..nenda bank na hati wakupe pesa.
 
Badala ya kuwakashifu wanaoweka pesa utt na bond ni vyema ukaeleza kwa hoja zilizo na mashiko kwamba kwanini john atoe pesa zake utt/bond ajenge majumba na asubiriwe na crdb kukopeshwa
Mkitaka ushauri zaidi niulizeni wajinga ndio waliwao
 
Wala sio story ndugu yangu kuwekeza majengo uwe na roho ya kusubiri
Hela yake inachelewa sana kurudi, wanaokimbilia majengo ni woga wa biashara akili zao zinawaza kupoteza ili kujilinda wanawekeza majengo kwasababu hayapotei
Usipokuwa mwoga hela utaipata haraka huna haja ya kusubiri miaka 20
 
Uchwara sidhani kama ni rafiki kwangu siwezi kuwapa assets za 200m wanipe 100m wangenipa 180m nakuendelea sawa
Hii ni kwasababu maombi makubwa ya taasisi za fedha ni mkopaji ushindwe kulipa
Bora ukashindwa kulipa lakini hela yako umepata kuliko kushindwa kulipa alafu uliwe na kula msumari wa moto, wao wakienda kuuza waondoke na utajiri wewe ukafe
Afadhali ukopeshane na watu mnaofahamiana

Lugumi alichukua mkopo kwa Manji kama ni uchwara wasingempa ile hela
 
Bado una kashifu hujapevuka bado kiakili, mtu mzima mwenye akili timamu akiulizwa kitu anajibu kwa staha na hoja...hata mtu mweny akili timamu hawez kuja kukuuliza mana hata maelezo utakayoyatoa yatakua ya kukashifu.
 
Kwa matajiri sawa, ila kwa makapuku sio kitu cha kufanya ...
Kapuku una nyumba moja huna biashara ama una biashara za uchuuzi kwamba uende benki ukakope kwa hati ..hakuna kitu kama hiko..hii inawafaa matajiri akitoa statement ya benki turnover yake ni kama kuanzia 100 hadi 500m ana biashara kadhaa ..
 
Kwa sehemu kubwa inategemea na location nyumba ilipo

Kujenga nyumba ya kuishi ni mhimu sababu biashara hazieleweki, isije ikayumba hiyo biashara hata pakulala sina itakua shida
 
Bado una kashifu hujapevuka bado kiakili, mtu mzima mwenye akili timamu akiulizwa kitu anajibu kwa staha na hoja...hata mtu mweny akili timamu hawez kuja kukuuliza mana hata maelezo utakayoyatoa yatakua ya kukashifu.
Ndiyo wewe uje ulete bond zaa nchi zaa kiafrika zilizomature na kutajirisha watu. Jenga nyumba nunua mashamba chukua mkopo anzisha biashara. Biashara ikifeli as long as una collateral kuna Banki nyingi zinanunua mikopo. Kuna bank ziko tayari kuilipa bank inayokudai na kuhamisha deni lako kuja Banki yao. Nyie endeleeni kujidanganya. Ushaona kuna matangazo ya Banki kuhusu kutoa mikopo ? Lakini kila kukicha kuna matangazo ya kijani bond, mara samia bond. Sasa nyie chagueni maana Kuna msemo kizuri chajiuza .........malizia
 
Mkopo wa bank ni msumari wa moto ndugu yangu
 
Wewe ndio umeongea cha maana kuna watu wana idea nzuri ya maana ila hawawezi kupata mtaji. Ila kuna watu wana assets anaweza kupewa mkobo hadi wa billioni mbili within two days. Kuhusu mikopo nimeshuhudia mambo mengi sana. Kuna wakati nilikuwa naona client anajenga hoteli amekopa banki na banki hio hio imeikopesha kampuni inayomjengea client. Kuna watu walianzisha biashara mpya kariakoo wakongwe wenye majumba wakachukua mkopo na kwende kuchukua mzigi mara kumi ya wao wakateka soko. Unadhani wangewekeza bondi wangeweza, Kaeni karibu na watu wa wizara ya atdhi iuna miradi kibao ya kuboresha unaweza ukajua wapi kutakuwa hot cale ndani ya miaka mitano ijayo. Kuna watu walinunua survey, sinza na maeneo ya karibu mwaka 1996 maana mipango ya kujenga mlimani city iliikuwa ndiyo inaanza. Vijana wanaogopa vitu vigumu lakini jua amua uteseke leo au uteseke uzeeni. Ukijibana na kununua sehemu ya potential ni rahisi kutoboa. Kule Mbeya kuna sehemu inaitwa Iwambi kuna jamaa zangu kibao walipawahi mapema sana. Ni kuishi na watu vizuri tu. Ipo mifano mingi sana kuanzia Goba, Mbweni hadi Kinyerezi. Sasa ni mwwendo wa kuamka na kutambua sehemu nyingine zinazochipukia. Namalizia kwa kusema Hakuna bishara unaweza kufanya bila ya kumiliki au kuitumia ardhi. Kama hiyo biashara ipo naomba je uilete hapa na unieleweshe.
 
Aisee kuna jamaa alikuwa anaitwa Tolu pale Survey hivi sasa ni marehemu. Huyu jamaa alikuwa na Bucha ya nyama kuna kipindi alikuwa anataka tufanye joint venture. Nilipitia mauzo yake huyu jamaa alikuwa anafikisha milioni 15 kwa mwezi. Ila huyu jamaa nyama yake ilikuwa Quality sana wanaomjua wanajua. Sijui biashara yake inaendeleaje. Biashara ya nyama ina faida sana inategemea na location uliyopo.
 
Kijiji cha mkoa gani uko aliko zaliwa
Wauza nyama Mwanza + Arusha + Kilimanjaro + Mbeya + Kagera wana nyumba za kisasa na Hilux kali wachovu ni wale walevi
Kwa muwekezaji utatembelea zaidi ya Hilux
 
Mkopo wa bank ni msumari wa moto ndugu yangu
Ndugu yangu mikopo ni misumari kama haujui jinsi ya kukopa. Mtu unapata tenda ya miliono 100 unataka ukope milioni mia ndio uifanyie kazi. Unatakiwa ukope maximum asilimia 40 ya mtaji wako wa biashara. Kama umepata tenda ya ujenzi unatakiwa ukope hela ya kukuwezesha kukamilisha scope ya ujenzi kwa required stage. Kama unategemea kulipwa baada ya kumaliza msingi au mobilization. Kopa kwa ajili ya mobilization ukishalipwa unalipa deni na kutumia hela iliyobakia kwa hatua inayofuata. Kama haitoshi unachukua tena mkopo this time utakuwa na higher Credit maana mkopo wa kwanza ulisharudisha. Hautakiwi kuogopa mikopo kama kweli business plan ayako imesimama kuna banki kibao zinanunua mikopo. Nimeshashuhudia zaidi ya mara kumi wafanyabiashara wakihamisha mikopo. Siwezi kutaja banki maana maafisa mikopo walikuwa wanatuambia tukaushe.
 
Mambo si ndo hayo, ingekuwa ni kodi za jengo angepata wapi hiyo 15m watu wengi ni woga unawamaliza wanakimbilia assets
 
💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…