Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Nikweli mkuu, ukitaka kuona hela mingi fanya maseto/kachumbari business yaani unafanya biashara nyingi tofautitofauti lakini moja haitatosha kukupa pesa mingi
Watu wengi wanapoteza ramani kwa kuwaza biashara yenye faida kubwa kitu ambacho sio sahihi
 
Sasa wewe wa Tandale unaleta mambo ya ulaya bongo?.Hatufanani nao hata nusu
 
Kuna kitu kikubwa mnoo mleta mada unakosea, umechanganya vitu viwili tofauti kwenye kapu moja.

Kujenga nyumba ya kuishi sio mbadala wa kufanya biashara, na kufanya biashara sio mbadala wa kumiliki nyumba. Watu wanafanya biashara ili kupata pesa za kuweza kumiliki nyumba za wao kuweza kuishi kwa raha, uhuru na uhakika leo, kesho na keshokutwa. Kuna muda unaweza kufikia wewe na jamii yako ukashindwa kufanya biashara (kwa sababu ya umri, afya nk) lakini bado ukahitaji kuishi kwa raha, furaha, uhuru na uhakika, na hilo litafanikiwa ukiwa na nyumba yako.

Jiulize hili swali, ukiweza kulijibu utakuwa umeelewa kitu. Unasaka pesa (kuwekeza au kufanya biashara) ili ukija kuzipata uzifanyie nini?
 
Kununua 2014, kuuza 2024
Siyo lazima iwe hivyo. Kuna kiwanja nilinunua mil 8 kwa jamaa alikuwa na uhitaji wa pesa ya haraka. Baada ya wiki 2 narudia wiki 2, akapatikana mteja wa 15mil.

Kuna Real estate broker alinunua eneo maeneo ya pugu kwa raisi kwa mil 100 watu wakamuona kichaa, jamaa alikata vipande ndani ya miezi mi3 akaviuza kwa zaidi ya mil 150.

Hilo biashara hakikisha una mziko wa kutosha, kisha kazi yako ni kudeal na watu wenye uhitaji wa pesa ya haraka. Wanauzaga kwa bei za kutupa. Kisha wewe uza ukiwa umerelax, utapata super profit mpaka wengine uwaone wamekuja mjini kudhurula
 
Utatunza milion mia kwenye laini
 
Ni kweli kabisa Mkuu. Mfano ni Dodoma, sasa hivi viwanja vya mjini kati havikamatiki. Hata fremu za biashara ni bei mbaya sana. Uchaguzi wa sehemu ya kuwekeza kwenye masuala ya ardhi ni muhimu sana.
Ardhi ukiwa na subra utaona hela yake kwa vichaa wa hela za motomoto ambazo hazijapoa tunateseka sana kusubiri ndio tatizo letu lilipo
Binadamu anasaka hela apate za kuboresha maisha na kufanya maendeleo
 
Hao wazungu Kama hawajengi wanaishi wapi? Kwenye nyumba zinazomilikiwa na real estate kwahiyo hiyo ndiyo biashara ya kijanja pata picha unamiliki gorofa pale posta au chanika stendi au mjiwowote sehemu iliyochqngamka swala la msingi ni location ya nyumba yako.
Donard Trump na Robart Kiyosaki ndio biashara zao hizo tafuta location yenye soko Jenga nyumba kula Kodi,
 
💯
 
Ardhi huwa pia inaweza ukashuka thamani, mfano serikali ikidesignate sehem iliyo karibu na ww kuwa mayb Dampo la jiji, au sehem ambayo inapatwa na majanga mara kwa mara kama kujaa maji , tetemeko la ardhi nk…huwa ardhi inaweza kushuka thamani ingawa ni mara chache
 
Yuko sawa nimjibie hili...hivyo anavyoviita asset ukweli sio asset...NI luxury liability...asset NI mpaka pale vinapoanza kuongoza hela...ardhi inatunza dhamani ya hela uliyonunulia sio inapanda dhamani kwa utafiti lakini...inapanda dhamani pale demand inapopanda na Kuna some rare case inapoteza dhamani.. mf.. sehemu kulikuwa na mradi Fulani Kama nzega palipokuwa na mine viwanja vilipaa Bei Ila Sasa mgodi umefungwa viwanja vipo chini sana pamoja na nyumba zipo chini sana...misigiri ilipokuwa onatumika barabara moja kabla ya manyoni tabora kufunguliwa palikuwa na demand kubwa ya nyumba na viwanja kuliko ilivyo leo..
Nyumba inashuka thaman sana kuliko eneo...Kuna watu wananunua nyumba Ila wanatagert eneo...hao matajiri unaosemea wanahifadhi hela ya ziada kwenye maeneo sio unachukua hela ya mtaji kununua ardhi NI kujipiga Pini....au hela ya mtaji kujengea nyumba ya kuishi...Bora ingekuwa ya biashara frem au lodge..
 
Labda utupe mfano uliowahi kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…