Kumkamata Aliyepiga picha watoto wakiwa chini ni kumuonea, zipo shule nyingi watoto wanakaa chini

Watanzania wengi hawazalishi na hawalipi Kodi za Moja kwa Moja (direct taxes),wengi wanachojua ni kuzaa tu!
Hata ije Serikali gani hizi facilities haziwezi kutosha mpaka hii equation ya uzazi na uzalishaji iwe solved na balanced!
 
Picha iko wapi?
FB_IMG_1675843595771.jpg

Aliyekamatwa huyu hapa

FB_IMG_1675843441314.jpg
 
Shule ya Msingi Muyombo Kata ya Lwamgasa Busanda Geita wanafunzi wakiwa wamekalia madawati ya kisasa kabisa

View attachment 2510173
Hivi Watanzania wanategemea hiki kizazi ambacho hawakishulikii kiwe na uwezo wa kushindana na dunia ya leo. Nchi haiwezi kuendelea kama hanufaishi kizazi kijacho na hapa hii inathibitisha these kids are being short changed
 
Kwa kosa ngani??
Utakuta mkandarasi wa hiyo shule amelipwa pesa nyingi anaweza kusema alipa ripu na madirisha aliweka na madawati yalishalipiwa lakini ni hewa ndio sababu wamkamata msema kweli
 
Kufuatia sakata la picha liyopigwa ikionesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinde wakiwa wamekaa wakisoma chini bila madawati na Serikali ikionekana kung'aka kwa kumuweka ndani anayesemekana kupiga picha hiyo ni sawa na mbuni kujifunika kichwa huku mwili ukiwa nje na akidhani kajificha. Soma Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

foyxyjpxsaa5dru-jpg.2510070

Kwa Tanzania hii siyo Sinde pekee ambayo watoto wanasoma wakiwa chini bila madawati hivyo hata serikali ikijaribu kumtoa kafara huyo mpiga picha na raia mwema ili iweze kuficha aibu yake ni sawa na bure kwa kuwa ukweli ni kuwa hali hiyo ipo kwa shule nyingi nchini japo makujwaani mnajinadi kuwa mmeboresha mazingira ya elimu ila ukweli ni kuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu sana.

Turudi Sinde, imeonekana baada ya Viongozi kufika hapo shuleni madawati yalikuwepo darasani hivyo kuonekana huyo mpiga picha anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo alizusha ili kuleta taharuki.

Najiuiliza nani anadanganya kati ya Mwalimu na Serikali?
  • Je, Mwalimu alitoa madawati na kuwaamuru wanafunzi wakae chini ili apige picha asambaze uongo?
  • Je, baada ya Serikali kuona taarifa imefika kwa wananchi wakaweka madawati ili waweze kukanusha taarifa ya awali ionekane alizusha na aadhibiwe ili kuwatia hofu wengine wasifichue maovu?
Baada ya sinema hii nini kitajiri, iwapo Serikali itafanikiwa katika hili basi ni wazi watu wataingia ganzi kufichua madhaifu au uovu wowote hata unaoonekana kwa macho na kufanya jamii ibaki katika giza na maumivu ya kuishi na uduni kwa kuwa ukisema inabadilishwa na unakuwa mhalifu na kushikwa na polisi.

Iwapo Mpiga picha au picha ikaweza kuthibitisha kuwa ni kweli walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati basi ni wazi Serikali itapata aibu na itakuwa imejishushia zaidi heshima na kufanya hata ikiwa wanakanusha kitu hata kama ni kweli kilizushwa jamii ione wanadanganya kama ambavyo imekuwa hapo zamani.

Leo tukisema kila shule ilete takwimu za watoto wanaokaa chini au picha nchini hapa Serikali itaweka ndani nchi nzima kwa kuwa ni nyingi na si Sinde pekee, au kwakuwa anatoka Spika wa bunge ndio maana Serikali imeona haifai taarifa hii itoke kwa umma? Shule nyingi hazina madawati japo tumejaza misitu na tunajimwambafai kuupiga mwingi katika elimu.

Badala ya Serikali kuhangaika na watoa taarifa kuwakamata iboreshe shule zote kwa kuhakikisha zina miundombinu inayotakiwa kuanzia madawati, vyoo, madarasa na vifaa vya kufundishia kwa kuwa naamini uwezo huo upo ila havifanyiki kwa kuwa hakuna anayeona maumivu ya mtoto wa kitanzania kukaa chini kwa kuwa watoto wa wenye mamlaka hawasomi shule za Serikali.

Pia soma:
ukweli unauma...hamaki ya serikali yote ya wilaya inatia mashaka sana
 
1675847554076.png
 
Umevaa chup ilotoboka ila umeificha na gauni jipya.
Siku ukiifua itaonekana. Siku ukienda kwa baby wako ataiona
Dawa ni kununua nyingine ka huwezi ishone kupunguza aibu yako
 
Shule ya Msingi Muyombo Kata ya Lwamgasa Busanda Geita wanafunzi wakiwa wamekalia madawati ya kisasa kabisa

View attachment 2510173
Yaani tupigeni picha pote wanapokalia chini na tofali za tope na pia ishu ya vifaa vya zahanati huko kukoje.

Kuna watu wananunua gari la kutembelea utadhani Kama hawatakufa la 600M huku watu wankosa huduma muhimu Kama dawa ama watoto wetu wanakosa walimu wa masomo ya sayansi. Yaani watanzania Ni waoga Ila ngoja tozo na sindano zikiwa Kali nadhani kitaeleweka tu.

Saivi mwanza hapa machinga wameanza vurugu wanarusha mawe kwenye maduka ya watu.
Yaani wao wanadhani kuwa watu watakuwa kwenye maumivu wao wakiwa wanakula keki ya Taifa na urefu wa kamba yao.

Cheki huyu anadhani ndiye anayestahili kuila nchi
 
Back
Top Bottom