Kumkamata Aliyepiga picha watoto wakiwa chini ni kumuonea, zipo shule nyingi watoto wanakaa chini

Jamaa aachiwe Mara moja

Kufuatia sakata la picha liyopigwa ikionesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinde wakiwa wamekaa wakisoma chini bila madawati na Serikali ikionekana kung'aka kwa kumuweka ndani anayesemekana kupiga picha hiyo ni sawa na mbuni kujifunika kichwa huku mwili ukiwa nje na akidhani kajificha. Soma Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

foyxyjpxsaa5dru-jpg.2510070

Kwa Tanzania hii siyo Sinde pekee ambayo watoto wanasoma wakiwa chini bila madawati hivyo hata serikali ikijaribu kumtoa kafara huyo mpiga picha na raia mwema ili iweze kuficha aibu yake ni sawa na bure kwa kuwa ukweli ni kuwa hali hiyo ipo kwa shule nyingi nchini japo makujwaani mnajinadi kuwa mmeboresha mazingira ya elimu ila ukweli ni kuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu sana.

Turudi Sinde, imeonekana baada ya Viongozi kufika hapo shuleni madawati yalikuwepo darasani hivyo kuonekana huyo mpiga picha anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo alizusha ili kuleta taharuki.

Najiuiliza nani anadanganya kati ya Mwalimu na Serikali?
  • Je, Mwalimu alitoa madawati na kuwaamuru wanafunzi wakae chini ili apige picha asambaze uongo?
  • Je, baada ya Serikali kuona taarifa imefika kwa wananchi wakaweka madawati ili waweze kukanusha taarifa ya awali ionekane alizusha na aadhibiwe ili kuwatia hofu wengine wasifichue maovu?
Baada ya sinema hii nini kitajiri, iwapo Serikali itafanikiwa katika hili basi ni wazi watu wataingia ganzi kufichua madhaifu au uovu wowote hata unaoonekana kwa macho na kufanya jamii ibaki katika giza na maumivu ya kuishi na uduni kwa kuwa ukisema inabadilishwa na unakuwa mhalifu na kushikwa na polisi.

Iwapo Mpiga picha au picha ikaweza kuthibitisha kuwa ni kweli walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati basi ni wazi Serikali itapata aibu na itakuwa imejishushia zaidi heshima na kufanya hata ikiwa wanakanusha kitu hata kama ni kweli kilizushwa jamii ione wanadanganya kama ambavyo imekuwa hapo zamani.

Leo tukisema kila shule ilete takwimu za watoto wanaokaa chini au picha nchini hapa Serikali itaweka ndani nchi nzima kwa kuwa ni nyingi na si Sinde pekee, au kwakuwa anatoka Spika wa bunge ndio maana Serikali imeona haifai taarifa hii itoke kwa umma? Shule nyingi hazina madawati japo tumejaza misitu na tunajimwambafai kuupiga mwingi katika elimu.

Badala ya Serikali kuhangaika na watoa taarifa kuwakamata iboreshe shule zote kwa kuhakikisha zina miundombinu inayotakiwa kuanzia madawati, vyoo, madarasa na vifaa vya kufundishia kwa kuwa naamini uwezo huo upo ila havifanyiki kwa kuwa hakuna anayeona maumivu ya mtoto wa kitanzania kukaa chini kwa kuwa watoto wa wenye mamlaka hawasomi shule za Serikali.

Pia soma:
 
Me mwenyewe hapa muda huu nimekaa chini.
 
1977 nilitumia darasa kama hilo!
Mwongo mkubwa wewe! 1977 darasa moja lilikuwa na wanafunzi wasiozidi 45 na serkali ilihakikisha madawati, meza na vitu vya kukalia walimu vipo muda wote! Hiyo shule uliyosoma wewe hapo Kinondoni haikuwahi kuwa na upungufu wa madawati kwa mwaka huo. Tafuta uongo mwingine!
 
Shule ya msingi mianzini ,mburahati kata ya makurumla wilaya ubungo kuna baadhi ya madarasa hayana madawati ya kutosha na wanafunzi waliopo darasani ni wengi kuzidi namba ya madqwati wengine wanakaa chini kwa hiyo shule ambazo hazina madawati ni nyingi hata mufindi ambako zinatoka mbao kuna baadhi ya shule zina upungufu wa madawati
 
CHADEMA mlisema amekufa Magufuli haya hayakuwepo tena nchi imetulia

USSR
Tukisema Sukuma Gang nyie mataahira mnasema mnatukanwa, lakini kwa post hii na thread husika ni dhahiri nyie wote mna mtindio wa ubongo. Hamna uwezo wa kujibu hoja yoyote au sijui ni uvivu wa kusoma na kuelewa hoja iliyopo mezani mnakurupuka kuihusisha Chadema na mada ambayo haiwahusu.
 
Ingekua serikali ya awamu ya 5 ndio imemkamata huyo mpiga picha mayowe yangekua mengi Dunia ingejua.
Lakini awamu hii ya maridhiano ndio inafanya haya.
 
Trillion 4 pesa za madawati tumekopa, na bado watoto wanakaa chini, daah!!!!
 
Kufuatia sakata la picha liyopigwa ikionesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinde wakiwa wamekaa wakisoma chini bila madawati na Serikali ikionekana kung'aka kwa kumuweka ndani anayesemekana kupiga picha hiyo ni sawa na mbuni kujifunika kichwa huku mwili ukiwa nje na akidhani kajificha. Soma Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

foyxyjpxsaa5dru-jpg.2510070

Kwa Tanzania hii siyo Sinde pekee ambayo watoto wanasoma wakiwa chini bila madawati hivyo hata serikali ikijaribu kumtoa kafara huyo mpiga picha na raia mwema ili iweze kuficha aibu yake ni sawa na bure kwa kuwa ukweli ni kuwa hali hiyo ipo kwa shule nyingi nchini japo makujwaani mnajinadi kuwa mmeboresha mazingira ya elimu ila ukweli ni kuwa watoto wanasoma katika mazingira magumu sana.

Turudi Sinde, imeonekana baada ya Viongozi kufika hapo shuleni madawati yalikuwepo darasani hivyo kuonekana huyo mpiga picha anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo alizusha ili kuleta taharuki.

Najiuiliza nani anadanganya kati ya Mwalimu na Serikali?
  • Je, Mwalimu alitoa madawati na kuwaamuru wanafunzi wakae chini ili apige picha asambaze uongo?
  • Je, baada ya Serikali kuona taarifa imefika kwa wananchi wakaweka madawati ili waweze kukanusha taarifa ya awali ionekane alizusha na aadhibiwe ili kuwatia hofu wengine wasifichue maovu?
Baada ya sinema hii nini kitajiri, iwapo Serikali itafanikiwa katika hili basi ni wazi watu wataingia ganzi kufichua madhaifu au uovu wowote hata unaoonekana kwa macho na kufanya jamii ibaki katika giza na maumivu ya kuishi na uduni kwa kuwa ukisema inabadilishwa na unakuwa mhalifu na kushikwa na polisi.

Iwapo Mpiga picha au picha ikaweza kuthibitisha kuwa ni kweli walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati basi ni wazi Serikali itapata aibu na itakuwa imejishushia zaidi heshima na kufanya hata ikiwa wanakanusha kitu hata kama ni kweli kilizushwa jamii ione wanadanganya kama ambavyo imekuwa hapo zamani.

Leo tukisema kila shule ilete takwimu za watoto wanaokaa chini au picha nchini hapa Serikali itaweka ndani nchi nzima kwa kuwa ni nyingi na si Sinde pekee, au kwakuwa anatoka Spika wa bunge ndio maana Serikali imeona haifai taarifa hii itoke kwa umma? Shule nyingi hazina madawati japo tumejaza misitu na tunajimwambafai kuupiga mwingi katika elimu.

Badala ya Serikali kuhangaika na watoa taarifa kuwakamata iboreshe shule zote kwa kuhakikisha zina miundombinu inayotakiwa kuanzia madawati, vyoo, madarasa na vifaa vya kufundishia kwa kuwa naamini uwezo huo upo ila havifanyiki kwa kuwa hakuna anayeona maumivu ya mtoto wa kitanzania kukaa chini kwa kuwa watoto wa wenye mamlaka hawasomi shule za Serikali.

Pia soma:
Kwa maoni yangu watu wote au walimu wote ambao wanafundisha shule zote ambazo baadhi ya wanafunzi wanakaa chini ni busara sana na wao wakapiga picha na kutuwekea hapa ili jamii ione, na nafikiri ndio njia mojawapo sahihi pia ya kumsaidia mwalimu aliyejitoa mwanga.
 
Back
Top Bottom