Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Sote wapemba tulimpigia chapuo Shamsi kuna manyang’au wakampitisha Mwinyi ambae hatumjui , kwasasa sisiem siwaamini kabisa badala ya Ndugulile utaambiwa kapita Makonda yule mwizi wa vyeti vya shemeji yake!! kuna wasaa huwa nasikia aibu kuwa mtanzania hasa wajinga wanapohodhi madaraka!!

Tufanye kaiba Vyeti, mbona wenye vyeti halisi hawana wakifanyacho wanashindwa na Bashite?
 
Makonda kukatwa ni ndoto za alinacha tena za mchana kweupe mapeema kwa wengine waweze wana nini na yeye ashindwe ana nini hamtaamini atakavyo kuja kuwa mbunge kamili tena kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi na wananchi mwisho wa siku mtazimia kama sio kustaajabu atakapo kuja kuwa waziri muda utaongea


Siasa huwa hazieleweki Mkuu
 
He! Tayari mmeanza kumchukia kiasi hicho? Hakika ccm ni kama mbwa mwitu, wanakula nyama pamoja lakini mlo ukiisha umebaki na damu mdomoni nawe unaliwa!
Nani kakwambia mi nipo CCM? Hebu cheki avatar uone mambo ninayoshughulika nayo.Na nafahamu hutayaelewa pia.
 
Makonda hawezi kunituma mimi.
So umejituma kumsafisha mtekaji ,mtu mwenye kauli chafu,mjivuni,mkandamjzaji wa wafanyabiashara anaetumia mgongo wa jina la mungu, mtu asie kuwa hata na ID ya ukwel,mtu alie mpiga makofi mzee warioba??try to be serious sio kila jambo linahitaji ushabiki...usilete siasa kwenye maisha ya watu.
 
kamati ya roho mbaya imeshapewa rungu na imeshaamriwa "hakuna yeyote aliyetumwa na rais"

konda anakatwa
Mtukufu aliwahadaa watanzania lakini anao watu wake aliowatuma mojawapo ni profesa Kabudi kule kilosa, mpango kule kigoma na wengineo wengi wakiwemo wazaliwa wa mwaka 1982 wa Arusha na Kigamboni, kudhihirisha hilo ni pale watakapokuwa wabunge ambapo lazima atawapa uwaziri bila chenga
 
1. Nafahamu
2. Moja ya kiongozi bora mwenye kuleta maendeleo ni kuleta hofu. Fuatilia historia utaelewa hilo. Hata hizo nchi za ulaya zilijengwa kwa hofu zilizoundwa na viongozi shupavu
3. Hata akipewa U-PM Haina shida, lakini uwaziri upo kitaifa zaidi tofauti na mkuu wa Mkoa ambapo yupo level ya mkoa yaani mipaka yake ni mkoa mmoja
4. Upo sahihi, lakini maneno ya shombo inategemea anayasema wakati gani na anamwambia nani? Hata Yesu alikuwa ana maneno ya shombo
Okay..kama unatambua, na hayo ndio mawazo yako naomba niyaheshimu..TZ ni nchi yetu sote..Kila raia ana haki ya kutoa na kuheshimu mawazo ya mwingine bila kuvunja Sheria za nchi..
 
Kuhusu kupitisha Fenicha nilishawahi kumkosoa,
unafikiri ni mara yangu ya kwanza kuandika habari zake huyu mtu?
Mbona makala nyingi nilizoandika habari zake nimemkosoa zaidi kuliko kumsifia. Lakini bado sioni kijana anayesogelea nafasi yake.

Makonda anamakosa mengi huenda kwa sababu anajaribu mambo mengi. Wengine hawana makosa kwa sababu hawajajaribu hata jambo moja
Hivi ukiwa unaandika andika hivi kuna kipato chochote unachopata labda ndugu?
 
KUMKATA MAKONDA SI MAAMUZI YENYE AKILI

Na, Robert Heriel

Ikiwa CCM itaamua kumkata Mhe. Paul Makonda itakuwa imefanya maamuzi yasiyo na busara. Yatakuwa ni maamuzi yasiyo na akili. Makonda ni moja vijana wachache muhimu kwa zama hizi katika taifa hili. Taifa la Tanzania linahitaji vijana mia moja mfano wa Makonda ambao watakuwa nchi nzima kwa ajili ya kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii.

Ni muhimu Makonda akipitishwa na CCM katika nafasi ya ubunge kisha baadaye apewe nafasi ya uwaziri katika wizara zinazowahusu vijana, burudani na michezo.

Kwa nini Makonda ni kete muhimu kwa siasa za sasa hapa nchini?
Hoja zifuatazi zitahusika;

1. UJASIRI
Makonda ni kijana jasiri asiye mwoga. Ni moja ya vijana wachache hapa nchini ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika uongozi, Makonda matukio aliyojiingiza yanambeba licha ya kuwa hajafanikiwa sana lakini angalau tuliona nia yake. Kuna mambo kuyafuatilia lazima uwe na roho ya kikulungwa, roho ya simba. Kufuatilia Wauza Madawa ya kulevya ni moja ya mambo ambayo ni magumu sio hapa nchini hata duniani kwa ujumla.

Makonda ni jasiri kwani haogopi kusimamia kile anachokiamini. Watu waoga huwa hawana Msimamo. Kilichomwangusha Makonda ni mipaka ya mamlaka katika kazi yake.

2. MWANAJAMII
Makonda ni moja ya viongozi wasiojifungia ndani. Huchangamana na jamii. Sio wale viongozi ambao wakipewa nafasi hujifungia ndani muda wote maofisini, kumuona tuu utahangaika mpaka ukate tamaa. Hii ni tofauti na Makonda, yeye anapatikana muda wowote, ukifika ofisini kwake hakuna milolongo ya ajabu ajabu. Makonda ni kawaida kumuona kwenye matukio ya kijamii mathalani matamasha ya vijana ya burudani na michezo, matukio ya misiba, n.k. Hii ni tofauti na viongozi wengine. Kiongozi lazima achangamane na jamii.

3. USTAHIMILIVU
Kama kuna vijana wavumilivu kwenye hili taifa ni pamoja na Makonda. Moja ya vijana walioonja joto la jiwe awamu hii mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni pamoja na Makonda. Licha ya kashfa kibao kama vile Kufoji vyeti, ambapo mahasimu wake walidai alicharaza mswaki kidato cha nne kwa majina yake halisi Daudi Albert Bashite. Hilo akalivumilia, kashfa za kuwa anatabia za kishoga, nalo akavumilia, kashfa za kuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto, yote alistahimili.

Pengine aliniudhi siku moja aliyolia kanisani, ile siku alijishushia credit. Mwanaume kulia lia mbele za watu sio jambo jema hasa wanaume shupavu. Hata hivyo halimuondolei sifa zingine lakini namuasa, siku nyingine asilie lie mbele za watu. Mwanaume kulia lia ni dalili ya udhaifu.

4. DHAMIRI YA DHATI YA KUISAIDIA JAMII
Makonda ni moja ya viongozi waliojipambanua katika kuisaidia jamii yake hasa kwenye Mkoa aliopewa auongoze. Makonda amesaidia vikundi vingi vya kina mama na vijana. Makonda ameonyesha nia za kuwasaidia watoto na kinamama waliotelekezwa na waume zao. Makonda ameonyesha nia ya kuwasaidia wale walioonewa kisheria kwa kuwawekea wanasheria, Makonda kajitahidi kupunguza uchafu wa jiji la Dar es Salaam, Makonda kajitahidi kurejesha usalama jijini Dsm kwa kupunguza vikundi vya Panya Road, sijui watoto wa Mbwa n.k.

Makonda anaweza asionekane ni kijana bora labda kutokana na tabia yake ya kujitukuza, na kutoa maneno ya shombo ambayo kwa sehemu kubwa nafahamu analenga kujifariji na kuwaumiza adui zake. Kwa kawaida kisaikolojia watu wanaotoa maneno ya shombo huyatamka kama njia ya kujifariji na kuondoa sonona, na kuwaumiza adui zao.

Wapo wakuu wa Mikoa wengi lakini waliofanya kama makonda hawafiki kumi. Hii ni dalili kuwa Makonda anafaa kupewa nafasi zaidi ya ukuu wa Mkoa.

5. MSAADA MKUBWA KWA MAGUFULI
Kama kuna watu waliomsaidia Mhe. Magufuli katika uongozi wake basi ni pamoja na Makonda. Imekuwa ngumu kumtenganisha Magufuli na Makonda katika siasa za awamu ya tano. Makonda amekuwa moja ya wabadilisha upepo katika masuala yanayotokea hapa nchini. Kwa namna hii amekuwa msaada mkubwa katika siasa za awamu hii. Makonda haoni shida kusemwa yeye kwa kupoteza mada fulani iliyokuwa inavuma ikiisakama serikali.

Pengine Makonda asiwe na ushauri wa maana kwa Magufuli lakini kiukweli anamchango mkubwa katika kubadili upepo wa mambo yanayovuma hapa nchini. Hili pekee linatosha kwa Magufuli kumkubali Makonda. Kumzima Makonda kwa wakati huu sio uamuzi wa akili. Nyota yake inang'aa lazima itumiwe kwa maslahi ya nchi.

6. KAFANIKIWA KULETA UTISHO
Makonda ni moja ya viongozi wachache waliofanikiwa kuleta utisho kwa watu wengi hapa nchini. Watu wa kawaida na viongozi wengi wanamuogopa Makonda. Kujenga hofu ni moja ya mambo ya muhimu katika utawala. Hofu hufanya utekelezaji uende kwa haraka. Makonda kwa cheo alichokuwa nacho cha ukuu wa Mkoa hakilingani na hofu aliyoijenga ndani ya jamii yake. Wengi humheshimu kupita cheo alichonacho.

7. BINGWA WA UHAMASISHAJI NA UCHANGISHAJI
Kiongozi sharti awe amebobea katika kuhamasisha watu. Makonda anajua kuhamasisha watu. Makonda anauwezo wa kuwachangisha matajiri, Akawaweka pamoja wafanyabiashara, wasanii na watu maarufu. Makonda anauwezo wa kuhamasisha vyombo vya habari vizungumzie jambo fulani. Tumeona mara kadhaa Makonda akikodisha kumbi za gharama kwa ajili ya tukio fulani mpaka wengine wanasema huyu Makonda anatoa pesa wapi. Makonda ni mhamasishaji na mchangishaji kwa wale atakaowaona wadau wa maendeleo.

Matajiri watachanga iwe kwa kumuogopa au kwa upendo. Hiyo haitamhusu Makonda ilimradi lengo limefikiwa.

Viongozi wengine katika hili walishindwa kabisa.

Magufuli anahitaji vijana kama hawa, watu kama Makonda, Tundu Lisu, Jokate, Anthony Mtaka, Prof jay, Ally Hapi, GJ Malisa, Ole Mushi, Ole Sebaya, Sugu, Profesa Mkandara, Ummy Mwalimu, Joyce Ndalichako, Suleiman Jafo, Bashe, Kassim Majaliwa, Bashiru, Ester Bulaya, miongoni mwa viongozi wengine wenye sifa.

Nafahamu kila mmoja ana mapungufu lakini kwenye mizani; ubora uzidi mapungufu.

Makonda apewe nafasi kwani ni mtu anayejirekebisha kila uchwao, sio mtu wa kutoa boko tena kama zamani alipokuwa mgeni wa kazi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300.
Inashangaza kwamba unampigia chapuo Makonda! Umeshapata uthibitisho wa uhalali wa elimu yake? Anajulikana kushindwa kumaliza masomo yake pale Ushirika Moshi kwa kuwa na suplementary nyingi ambazo inasemekana haku zi clear. Makonda ametaka kupitisha mizigo yake binafsi bila kulipa kodi bandarini, je huyu ndio shujaa wako? Eti Makonda (na kama hili ndilo jina lake halisi...) amefaulu kuwatisha watu! Kweli? Na hii nayo sifa ya kiongozi bora? Kuna mengi; namna alivyotaka kutatua changamoto za kifamilia kwa namna isiyokubalika kijamii, n.k. Hujui pia anahusika vipi kwenye underground affairs. Kwa kifupi ni mtu mnafiki na anauweza unafiki sana. Na mwisho wa yote, tayari Makonda ni international criminal, Marekani imeshamwekea red dot, hii ni sifa mbaya kabisa.
 
Muda utaongea
Kwa mujibu wa Le mutuz msiri wako mpaka Dakika hii huko Kigamboni mlipo tayari wewe Bashite upo top 3 kisha msubiri jina kurudi toka Dodoma ambapo ni mwenyekiti Ata kupitisha kwa nguvu zake binafsi lakini wajumbe wengine hawakutaki
 
Back
Top Bottom