Kumlipa Clinical Officer laki 6 sio haki hata kidogo

Kweli maslahi ya Nesi yanahitajika kuangaliwa upya, Waboreshewe.
 
Kama upo government stahamili utapanda madaraja. At least awamu hii imeleta matumaini.

Wengine tulistahili kubadilishiwa hayo madaraja 2016, tumeteseka hadi Jiwe alipokatiwa pumzi... ila Mama ametukumbuka
 
Nchi hii wajinga ni wengi. Yani ka mtu kana diploma kanakuja hapa kanajiona kana stahili zaidi kulko kada zingine.

Kwa nini ulifeli mdogo wangu? Kama kazi kubwa ndo kigezo basi tuanze kutoa mishahara mikubwa kwa wafanya usafi na walinzi.

Ntambafu ungesoma ukawa angalau hata na ka degree
 
Pesa nyingi unajitafutia!
Hakuna mwajiri (Serikali ama Mtu binafsi) Anaefanya biashara yake atakupa pesa ikutoshe!

Ukitaka kikubwa anzisha biashara uibembeleze ikue.

Serikali Siyo mzazi/ndugu yako, ni wafanya biashara so lazima wakunyonye!

Unajua kwa nini ‘shuguri’ zote za Serikali zinaendeshwa kijeshi?
 
Mshahara siku zote huwa hautoshi...
Hahahahahah we utakuwa unazungumzia wages mzee! Kuna wages na mshahara na hii tofauti yake ni kwenye ajira, kazi na kibarua!

Ukiona unalipwa not less than 50K per day jua upo kwenye ajira mzee. Hapa kuna ambao wanalipwa kati ya laki 1 mpaka laki 3 per day kwenye taasisi hizi hizi za serikali ama NGO za kimataifa. Huwezi sema ati mshahara hautoshi wakati account yako inaingiziwa 7.5M kila mwezi!

Less than 30K jua upo kwenye kazi. Hawa ni vibarua waliochangamshwa kidogo na overtimes.

Less than 20K jua unaenda kibaruani. Hawa ndio wanakula wages sema zimekuwa extended kwa mwezi tu.
 
Analipwa hivyo sababu hayupo kwenye level ya maamuzi ya Kodi yake, wanasiasa wanajipendelea malipo makubwa sababu wapo kwenye mfumo wa maamuzi
 

Namaanisha mshahara kaka....hata hiyo 7.5M siku ukifikia kulipwa hiyo utaona haitoshi...

Sisi wanadamu tuna kawaida ya kuhama madaraja kulingana na tunavyoingiza...

Mahitaji yetu kadiri yanavyobadilika ndio hubadilisha matamanio ya kuongeza kipato zaidi na zaidi...

Ukiwa hauna hela au unalipwa let say 1.5M kwa mwezi, huo mpunga wa 7.5M unauona mkubwa kishenzi, lakini ukipambana hadi ukafika huko, utaona hata life style yako inabadilika kuendana na watu wanaopokea huo mpunga...matumizi kibwena, ulikuw unavaa kiatu cha 15k, utataka uvae cha 450k 😁 n.k
 
Kwa Msoto niliopitia ndani ya mwaka tu wa huo mshahara naweza nikawa nishakamilisha dreams zangu by far.
 
Kodi muhimu duniani kodi ukifanya kazi utakatwa tu kodi

Wewe sema wapewe motisha kama vile allowances mbili tatu kwa kila kada

Kaa vile

Overtime
House
Food

Kada zingine hivi vitu wanapewa hasa huko majeshini

Muhimbili wanakula sana allowances

Na hii iende kwa kada zote at least manung'uniko yatapungua.

Tatizo wanasiasa wanajijali wao tu
 
Kwani kuna fofauti ndugu? MD ni 1,000,000/=. Hawezi hata kupanga Sinza.
MD 1480000. Nimecheka sana yaani Co hawa wanaoiba mitihani. Nao wanalalamika. Kama anaona anafanya kazi kubwa aache kazi. Au aongeze shule 5 years. [emoji23] [emoji23]
 
Kwa Msoto niliopitia ndani ya mwaka tu wa huo mshahara naweza nikawa nishakamilisha dreams zangu by far.

Hahaha!!!

Mungu akusaidie ufike huko kaka, halafu utakumbuka maneno yangu...

Mfano sasa hivi, unaweza jiambia nikipata huo mpunga labda ndani ya mwaka nikisave 4M kwa mwezi hivi nitanunua kiwanja Goba au K'mboni...

Lakini ukishaanza pata mpunga, unaanza jiona hivi nikisave 5.5M hivi si naweza nikapata uwanja kwa wadosi wa Mbweni au maUnunio huko...
 
Hakuna kitu kigumu kama CO kwenda MD. Ukipata ni bahati ya Mungu kakuangazia tu.

Na sasa hivi CO wamejaa mtaani kama nzige.Na wengine manalipwa mpaka Laki 2 kwa mwezi kwenye vijiwe.
Hahahahahah aisee ni ngumu sana
 
Nile mkataba kama huo si naingia bank tu navuta 500M chap namaliza michakato yangu yote ndani ya 2022 tu yani nahakikisha mjengo, ndinga na miradi kadhaa tayari imesimama.

Hata wakikata 4M kila mwezi nikaishi na 3.5M sio swala. Alimradi tayari nina mzigo wa kutosha kwenye account. Mjengo upo na miradi inaendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…