JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Sababu ulizotoa hazina msingi sana,Clinical officers wanafanya kazi kubwa sana kunusuru Maisha ya watu, kumlipa CO laki 6 ambayo ni sawa na Tsh elfu 20 kwa siku tena hapo bado makato sio haki hata kidogo.
Tukianza na sekondari ,huyu Co alilipa ada kubwa tofauti na wanafunzi wengine wanaosoma michepuo ya biashara na sanaa.
Pia asilimia kubwa ya CO's wa sasa walipita ngazi ya advance na walilipa ada kubwa mno tofauti na michepuo mingine mf PCM,hkl,hge eca nk.
CO hata Kwenda field tu analipia wakati fani zingine field hulipii Bali wewe ndiye unalipwa.
Serikali wajitahidi kumuongezea Hela CO angalau laki 8 kwa mwezi.
Kwamba wanasaidia watu,wamesoma kwa gharama kubwa.
Ili maisha yaende unahitaji taaluma na wataalamu wengi,wahasibu,wahandisi nk,na wote hao wamesoma kwa gharama kubwa!!
Swala la mshahara mkubwa inategemea umeajiliwa wapi?
Upo serikalini,muhimbili,bugando nk,au upo nje ya nchi