Kumsingizia Rais Magufuli ufisadi haiwezi kumzuia kupambana na mafisadi

nimesma mara tatu sijaelewa kabisa. Ina maana na ofisi ya AG nayo inatumika kisiasa siku hizi au AG katoa taarifa ya uongo au hakuna na maana kama tulivyoielewa wengi wetu?
 
Eti hapa kazi kumbe boonge la jizi linatakiwa lifungwe kama Lula da Silva wa brazil
 
fisadi gani kanyooshwa?
 
Umemsikiliza PolePole?Je ukimuuliza Assad anaeeza kusema 1.5 trilioni zilichukuliwa na mtu au taasisi flani?usiwe mdaku!

Duu kweli tumsikilize Polepole wakati inaeleweka anatetea mkono unaomlisha? Kwenye hizo 1.5 si ndipo zinapotoka hela za kununua wapinzani na yeye ndio kakabidhiwa fuko la fedha? Hakuna ufisadi wowote awamu hii ya tano inaopambana nao vinginevyo mahakama ya mafisadi ingekuwa na kesi. Zile mbwembwe za kupambana na ufisadi tulisema ni maigizo na sasa imedhihirika. Wananchi wamestuka wanawachora tu.
 
Fisadi mkuu yupo Chadema ...na ufisadi wake ulithibitishwa na Bunge
Hebu tupe Report iliyothibitisha Ufisadi wake, maana Report iliyopo ilimwajibisha yeye kwa nafasi Yake, sii kwa Kosa lililofanyika! Tuchukulie ndiye fisadi Kuu, huoni REKODI YAKE IMEVUNJWA almost 7 times?
 
Sema zitapita na ufisadi mtaendelea kufanya
 
We need our 1.5 trillion,wewe endelea kutetea upupu
Mku si tumeasisi mahakama ya mafisadi kama tuhuma tuliyotuhumiwa nayo ni nani tunampeka ktk hii mahakama kwa liko ndani ya chama.
Kumbuka hii ni tuhuma ambayo sio ya kupepesa macho kwani halisia kwa hiyo ni tofauti na tuhuma zisizo halisia kama hii
Mleta Mada hajui lolote yuko kishabiki 'He or She thinks we are all Fools'
 
Ninachokiona hapa ni watu kutupiana maneno kwa kebehi...

Sioni tatizo kwa Polepole kumjibu Zitto kwasababu Zitto alitoa msimamo wa chama kuhusu Taarifa ya CAG na siyo msimamo wa mbunge...

Polepole nae kama kiongozi wa chama anayo haki yakutoa msimamo wa chama chake kuhusu ripoti hiyo...

Hoja ya msingi hapa ni je Ni nani Kati ya Zitto na Polepole anahoja za msingi???

Nimemsoma Zitto na nimezisoma hoja za Polepole....

Zitto ametoa hoja 8 kutoka katika ripoti ambazo hata CAG alihojiwa Azam akakiri kuna fedha haionekani ilipo....!

Polepole amechambua kimahesabu namna hela iyo ilivyo paswa kuwa...!

Polepole pengine anaweza kuwa na hoja sina hakika sana...ninachojiuliza mimi hao waandishi waliokuwepo walishindwa kumuuliza Polepole maswali haya?

1)Yeye kama kiongozi wa Chama je hakubaliani na ripoti ya CAG kuhusu huo upotevu?

2) Kama kweli hakubaliani nao je CAG ameupotosha Umma na Bunge?

3) Je uchambuzi alioutoa leo ndivyo CAG alipaswa kuweka ripoti yake? Na kama ndivyo je4 CAG na wataalamu wake walikosea namna ya kukagua na kuweka sawa hesabu za serikali?

4) CAG ameweka dosari za matumizi ya fedha kwenye baadhi ya vyama vya siasa ikiwamo CCM na Chadema, kwa maelezo yake ametoa ufafanuzi juu ya dosari kwa upande wa CCM lakini akawalamu Chadema kwa ubadhirifu, Je anakubaliana na ripoti ya CAG kuhusu matumizi mabaya ya fedha kwenye vyama vya siasa?

5) Kama anakubaliana na CAG kwa upande wa vyama vya siasa kwann anapingana nae kwa upande wa Serikali ilihali kuna mawaziri wameanza kutoelea ufafanuzi mapungufu yaliyo tajwa na CAG kwenye wizara zao na wengine wamewafukuza kazi baadhi ya wakurugenzi na kuvunja bodi?

Kuna maswali mengi waandishi walipaswa kumuuliza Polepole...

Anyways bila shaka ripoti hii itajadiliwa bungeni...wabunge wanapaswa kuangalia maslahi ya nchi na kutoa majibu sahihi juu ya hii ripoti ili Watanzania awaendelee kuwa na imani na serikali na chama chetu...

Ni vyema pia kukawa na mijadala ya Kitaifa kujadili kwa uwazi na mapana ripoti hii....

1.5 Trilioni ni hela nyingi sana ni vyema kitendawili hiki kikateguliwa mapema...!
 
Ndo mana nilikua nashangaa kuona wana ccm wanaongea kuhusu kupambana na ufisadi. Nikawa najiuliza hivi shetani katubu na kua malaika saizi. Hizi 1.5 zimefanya nikumbke kua shetani wakati mwingne ili atimize matakwa yake anajigeuza kua kwa mfano wa malaika.
 
Mwevi wa 1.5. Trilion
 
Weka mkuu si unajua wanajua kuandaa ep zingne kabla hata moja haijaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…