Kumtetea Mbowe ni vigumu. Igizo lake alilofanya leo lina makosa mengi sana ya kiufundi

Kumtetea Mbowe ni vigumu. Igizo lake alilofanya leo lina makosa mengi sana ya kiufundi

Kila kinachofanyika n planned,..hata lisu kubadilisha nafas anayogombea sio kuwa alikurupuka,..inaonyesha kabisa n maagizo..kuwachangany tu
 
Serikali unayoisemea juzi imewapa TLS gari la dhamani ya +300 million.
Lissu alizalisha migogoro tu
Uwongo mtupu. Lisu ndiye iyeitoa TLS kutoka kwenye pingu za Serikali, na ndiye aliyeipandisha hadhi kiasi cha hata wasio wanasheria kuitambua vizuri, na kuijua nguvu yake.

Lakini watu wehu wanasema eti Lisu hakuifanyia kitu TLS, hivi walitaka TLS ifanye nini chini ya uongozi wake ili wajue mabadiliko aliyoyaleta, ijenge vyoo na madarasa!! Hopeless kabisa!!
 
Aisee kumtetea huyu mmiliki wa CHADEMA ni kazi ngumu sana. Haina tofauti na kuwatetea single maza na polisi.

Igizo lake alilofanya leo lina makosa mengi sana ya kiufundi kiasi kwamba wapinzani wake wamepata nafasi ya kumdhihaki.

Nawatupia lawama timu yake yote kwa kushindwa kuweka jambo la leo lionekane lenye uhalisia. Hii clip inayosambaa ndo imekuwa chumvi kwenye kidonda.
Mzee hakusoma vizuri script, ama kasahau.
Nimecheka sana.
 
Aisee kumtetea huyu mmiliki wa CHADEMA ni kazi ngumu sana. Haina tofauti na kuwatetea single maza na polisi.

Igizo lake alilofanya leo lina makosa mengi sana ya kiufundi kiasi kwamba wapinzani wake wamepata nafasi ya kumdhihaki.

Nawatupia lawama timu yake yote kwa kushindwa kuweka jambo la leo lionekane lenye uhalisia. Hii clip inayosambaa ndo imekuwa chumvi kwenye kidonda.
Huyo ni mwanajangwani au Lucas Mwasha
 
Kila kinachofanyika n planned,..hata lisu kubadilisha nafas anayogombea sio kuwa alikurupuka,..inaonyesha kabisa n maagizo..kuwachangany tu
Sio maagizo

Unakumbuka alichokisema jana? Kwamba nafasi ya umakamu inagombewa na mtu aliyemleta Abdul nyumbani kwake?
 
Serikali haiwezi tumia TLS kama chombo chao kama Lissu akiwa kiongozi, Lissu ni mtu na nusu, hakika hapa Chadema imepata mwenyekiti
Unajibishana na mtu anayeandika "gari yenye dhamani" badala ya thamani, hujagundua unajibishana na nani?
 
Subir apewe TL uone mtakavyo buruzwa barabarani kudai haki na katiba mpya...

Sikumbuki kumuona Lussu kwenye maandamano yeyote ya Chadema zaidi ya Yale yaliyokuwa yamruhusiwa na Samia.
 
Wacha iendelee kunyesha ili tuone panapo vuja

80% ya Wanamtandaoni hawamuungi mkono MBOWE

90% ya wajumbe wa mkutano mkuu chama taifa hawamuungi mkono MBOWE

98% ya wanachama wa CHADEMA na wananchi nanaopenda mabadiliko ya kweli hawamuungi mkono MBOWE

Mwachaneni achukue hiyo fomu baada ya kufikilia hayo masaa 48 yake lakini atambue anakwenda kupigwa kipigo cha mbwa koko.
 
Sikumbuki kumuona Lussu kwenye maandamano yeyote ya Chadema zaidi ya Yale yaliyokuwa yamruhusiwa na Samia.
Kila Nilipokuwa Nikitaka Kung'atuka Walikuwa Wakiniambia: 'Mwalimu Endelea Tu, Hii Nchi Ni Changa Na Umeitoa Mbali. Nchi Hii Haitaendelea Bila Wewe'. Nami Niliiendelea Hadi Pale Nilipokuja Kugundua Kumbe Nchi Changa Waliyoiongelea Ni Familia Zao.” :-Mwl. Julius Kambarage Nyerere
 
Walioko Jf, 80% sio wapiga kura siku ya uchaguzi wa Chadema!

So walioko nje ya Jf, ndio wapiga kura.
Mbowe atamshinda Lissu mapema asubuhi!
Hao wapiga kura watakuwa ni wajinga sn, hawana akili wote!!.
Mbowe baada ya miaka 20 madarakani ana nn tena kipya??
Upuuzi!.
 
Yule ni mtu mwenye tamaa! Umakamu mwenyekiti,miaka yake yote ,hajafanya chochote.
Robert Amsterdam,ana msaidia KESI ya tigo!
Huku anatafuta kushindwa uchaguzi akimbilie Belgium
Kama Lissu hakufanya chochote kwa miaka yote akiwa Makamu Mwenyekiti ilikuwaje akapendekezwa na Chadema kugombea kuwa Rais?
 
Profesa Lipumba ameandika historia kwa kuongoza Chama cha Wananchi (CUF) kwa kipindi cha miaka 25, baada ya kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti. Uchaguzi huu unakuja katika kipindi ambacho CUF inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kisiasa na kiutawala.

Katika uchaguzi huu, Profesa Lipumba amejitambulisha kama kiongozi mwenye uzoefu na uwezo wa kuimarisha chama, huku akisisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano miongoni mwa wanachama.

Ni hatua muhimu katika siasa za Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa viongozi kama Freeman Mbowe pia wanapata nafasi ya kuongoza vyama vyao tena.

Hii inaweza kuwa fursa kwa CUF kujiimarisha zaidi na kuchangia katika mabadiliko ya kisiasa nchini.

Kwa hivyo, ni jambo la kusubiri kwa hamu kuona jinsi Profesa Lipumba atakavyoweza kuongoza chama katika kipindi hiki kipya.
 
Back
Top Bottom