Kumuamini Askofu Gwajima ni kutopevuka kisiasa na kuuzwa kirahisi katika propaganda

Mtu wa Dini huwezi kutengeneza senario ya kumdhihaki Mungu na kama ikitokea basi we utakuwa ni binadamu wa hivyo kupata kutokea hapa Duniani.

Gwaji kasema ukweli kuhusu watejkaji
Nimemuongelea Gwajima kama mwanasiasa. Hata hiyo title ya Askofu kwenye kichwa cha habari wameiweka mods, mimi sikuitumia.

Siku hizi madhabahuni wanasimama watu wa kila namna ikiwemo hao hao wanasiasa ambao leo mnawaona wanahusika na utekaji na uchafu wa kila namna.
 
Sasa we ulitakaje, CCM ni jabali la siasa, wanaijua siasa in and out na kila chama kingetaka kuwa hivyo.
 
Gwajima anatumika tu. Wanajua Watanzania wanamsubiri na kumtafuta "hero" atakayewatetea. Ukiona mtu nchi hii anaongea maneno makali halafu haguswi jua hamna kitu hapo, labda mpaka reforms ikamilike, niamini nakwambia.
We ni mwehu? Mtu ameshafungiwa taasisi yake unasema haguswi? Ulitaka akamatwe? Dogo dola inajua pa kuanzia hayo mengine yatafuatia
 
We ni yale yale mazuzu yasiyojitambua
 
Warioba, Kitima, Lissu hao wamepita kwenye "litmus test" na sina mashaka na dhamira zao.

Mpina, Gwajima baaado. Kuongea au kuipinga serikali siyo issue. Tumeshuhudia wangapi miaka yote hii, halafu kirahisi rahisi wanaunga mkono juhudi na kuwaacha solemba na matatizo yenu?
 
Kudhani mfumo thought this through and made a plan ni kuwapa sifa za bure ambazo hawana.

What else unachoamini, utekaji na mauaji yanayoendelea nayo propaganda sio?
 
We ni mwehu? Mtu ameshafungiwa taasisi yake unasema haguswi? Ulitaka akamatwe? Dogo dola inajua pa kuanzia hayo mengine yatafuatia
Kufungiwa kanisa siyo "kuguswa" kama umeelewa ukubwa wa jambo ninaloliongelea na mbinu za kisiasa ninazoziongelea. Mbowe alifungiwa biashara zake na sijawahi kumuamini katika mambo ya siasa.
 
Gwajima anatumika tu. Wanajua Watanzania wanamsubiri na kumtafuta "hero" atakayewatetea. Ukiona mtu nchi hii anaongea maneno makali halafu haguswi jua hamna kitu hapo, labda mpaka reforms ikamilike, niamini nakwambia.
Kuguswa ni nini? Kufungia taasisi ya kanisa yenye watu zaidi ya milioni moja kwa kosa binafsi, huoni kwamba ni unprecedented action. Haijawahi kutokea Tanzania.

Hii italeta precedent ambapo makanisa, misikiti yoyote yanaweza kufungiwa wakiomba haki itendeke.
 
Gwajima anatumika tu. Wanajua Watanzania wanamsubiri na kumtafuta "hero" atakayewatetea. Ukiona mtu nchi hii anaongea maneno makali halafu haguswi jua hamna kitu hapo, labda mpaka reforms ikamilike, niamini nakwambia.

..sasa mbona Gwajima kaguswa?

..Ni kweli Gwajima ana makandokando mengi.

..Lakini tatizo lililoko mbele yetu ni kubwa na kama sauti na kauli za Gwajima zitasaidia kuongeza nguvu hata kiduchu dhidi ya utekaji hatuna budi kuzipokea.
 
Time will tell....
And indeed...

It will tell you exactly what I am telling you now...!
Huwa napenda kufukua nyuzi kama hizi nyakati zikifika tukiwa na mwanga wa kile kilichojiri. Juzi nimefukua uzi wa Mbowe, wale waliokuwa wananipinga sijawaona tena.
No problem at all...

Wewe fanya kuu - archive vizuri ili uje uufanye reference yako baadaye..

Kuhusu Freeman Mbowe, kama ulikuwa upande wake ktk kumuonya kuwa hawezi kushinda, basi kwa hilo tulikuwa pamoja...

Hili la Gwajima na mgogoro dhidi ya Rais na Mwenyekiti wake wa CCM tunatofautiana 100%...

Hawa wote wawili Gwajima vs Samia au serikali upande mmoja na CCM upande mwingine ni two opposite colliding forces zilizojikuta ziko chungu kimoja kwa kusudi maalumu la Mungu..

Kwenye collision hii, lazima kimoja kipasukepasuke...

You can easily see, who is a loser here...

Wewe utaangalia magari, polisi, mbwa na majeshi aliyonayo Samia na hivyo ku - conclude kuwa Mungu Yehova anayewakilishwa na Mch. Gwajima hapa ni loser. You're absolutely wrong...!

The opposite is true...
 
Litmus test gani ambayo unataka Mpina, Gwajima wapitie, kupondwa na vyuma kama Kitima,risasi kama Lissu, au kutengwa kama Warioba. Fafanua.
 
NASHINDWA KUELEWA MAPOLISI WALIFWATA NINI KANISANI KWAKE KAMA ANAWALINDA WAHUSIKA KAMA USEMAVYO
 
Kufungiwa kanisa siyo "kuguswa" kama umeelewa ukubwa wa jambo ninaloliongelea na mbinu za kisiasa ninazoziongelea. Mbowe alifungiwa biashara zake na sijawahi kumuamini katika mambo ya siasa.

..Ccm pia inatengeneza mazingira ya kutoaminiana miongoni mwa wapinzani kama njia ya kuwadhoofisha.

..Kwa hiyo hata Gwajima yatatengenezwa mazingira ya kutomuamini kama njia ya kupinga hoja zake.

..Tunachofanya sasa hivi ni kuunga mkono HOJA za Gwajima dhidi ya utekaji bila kutilia mkazo makandokando yake yaliyopita.

..Kauli na hoja zake kwa wakati huu zinawachoma watekaji kuliko zinavyowaathiri wanaharakati.
 
UNATAKA KUAMINI KIPI? KUNA SERA AMBAYO AMEONGEA?
AU NI HOJA ZAKE NDIO ZINAZOWAPA CCM NJAA YA KUTEKA NA KUUA TENA?
KWAMBA HAWATEKI KIASI KWAMBA UNATAFUTA NINI CHA KUAMINI?!
 
Litmus test gani ambayo unataka Mpina, Gwajima wapitie, kupondwa na vyuma kama Kitima,risasi kama Lissu, au kutengwa kama Warioba. Fafanua.
Ukielewa extent ya tatizo hauwezi kuuzwa kirahisi kwa mtu kufungiwa biashara au taasisi yake.

Tatizo wengi mmedogosha sana dhamira ya CCM kubaki madarakani, hamjui au mnadharau mizizi yake imeenda chini kiasi gani na hili linawagharimu sana.
Kusema watendaji wa serikali wanashindwa kufanya maamuzi kwa kuogopa kutenguliwa ni ushindi mkubwa kwa wahusika maana inawaondolea lawama wale ambao mlitakiwa muanze nao kuwawajibisha.

Gwajima na waliomtuma wanajua kwa nchi hii, Rais ni mtu wa mwisho kuwajibishwa kwa hiyo kuweka shutuma kwake ni jambo salama zaidi kwa wahusika. Hawa watendaji ni rahisi kuwasafisha maana tayari yeye ameshafanya hivyo! Watu hamuelewi spinning zinavyofanyika.

Think hard and long, mtanielewa.
 
Ukielewa extent ya tatizo hauwezi kuuzwa kirahisi kwa mtu kufungiwa biashara au taasisi yake. Tatizo wengi mmedogosha sana dhamira ya CCM kubaki madarakani
😅Dhamira ya Ccm sio kubaki madarakani hadi mwaka 3000?
 
Ila Gwajima siyo mpinzani!
 
It takes more balls kuweka shutuma kwa rais, kuliko vyombo vilivyoko chini vyake. Sababu kwa Tanzania Rais yupo juu ya mifumo yote.

Consequences za kujaribu kumshauri Rais kutenda haki ni tofauti na kujaribu kumshauri mkuu wa TISS, IGP, Magereza au CDF.

Jaribu wewe binafsi uone matokeo yake. Unaweza kutuma twitter, Facebook kutumia jina lako halisi.
 
Inawezekana kukubali hoja ya Gwajima ya kupinga utekaji.

Na wakati huo huo kutokubaliana na Gwajima kwenye mambo mengine kama vile hoja ya kwamba Polisi hawahusiki katika utekaji.

Jikite kwenye hoja, si mahaba au chuki na mtu.
 
Samia Hakusema NENO "KIFO NI KIFO TU" baada ya kifo cha Kibao kuleta mzozo?
RAIS WAKO AMETOA STATEMENT IPI JUU YA UTEKAJI NA MAUAJI HAPA NCHINI?
ULIMSIKILIZA GWAJIMA VIZURI "SIO KWAMBA VIONGOZI WA VYOMBO VYA DOLA HAWAJUI KUHUSU HAYA YANAYOTOKEA"
ALFU WWE UMESOMA WAPI?? RAISI ANAWAJIBIKA NA HII NCHI WAKAT SAA YOYOTE ANAPASWAA KUWAJIBISHA VIONGOZI KWA MATENDO MAOVU AMEFANYA HIVYO?
Kufungiwa kanisa siyo "kuguswa" kama umeelewa ukubwa wa jambo ninaloliongelea na mbinu za kisiasa ninazoziongelea. Mbowe alifungiwa biashara zake na sijawahi kumuamini katika mambo ya siasa.
KWAHIO KIONGOZI MBUNGE ALIOCHAGULIWA NA WANANCHI AKIMKUMBUSHA RAISI JINSI YA KUWAJIBIKA NA KUWAWAJIBISHA WALIOTENDA MAKOSA HILO NDIO KOSAA UMESAHAU GWAJIMA NI MBUNGE UNAE AKILI KWELI THINK IT'S NOT ILLEGAL YET
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…