Kumuamini Askofu Gwajima ni kutopevuka kisiasa na kuuzwa kirahisi katika propaganda

HIVI KAZI YA MBUNGE SIO KUONGEA KWAAJILI YA WANANCHI HATA KAMA ANAONGEA NA RAISI??

UKIPIGA KURA UKACHAGUA KIONGOZI NA UKALIPA KODI ILIALIPWE MSHAHARA NANI NI BOSS WA NANI HAPO??

TANZANIA NI NCHI YA WATU WANAOLIPA KODI BILA KUFAHAMU HIZO KODI ZINAFANYA KAZI GANI

VIONGOZI WAKO KWAAJILI YA WANANCHI SIO KWAAJILI YA NCHI TUNGEKUWA HATUPO HAPA NCHINI WANGEPEWA HIYO MIKOPO WANAYOOMBA?
 
UNATAKA KUAMINI KIPI? KUNA SERA AMBAYO AMEONGEA?
AU NI HOJA ZAKE NDIO ZINAZOWAPA CCM NJAA YA KUTEKA NA KUUA TENA?
KWAMBA HAWATEKI KIASI KWAMBA UNATAFUTA NINI CHA KUAMINI?!

😅Dhamira ya Ccm sio kubaki madarakani hadi mwaka 3000?
Kuishinda CCM na kubadili mfumo wa kisiasa wa Tanzania inabidi kubadili "rules of engagement" za mapambano ya kisiasa. Nitatumia maneno hayo machache kwa sasa. Lissu ndiye pekee amelijua hilo ila wanaomzunguka na Watanzania wengi hawapo tayari kumuunga mkono 100% maana inajumuisha kubadili "entire mindset" ya mtanzania wa kawaida. Sihesabu uungwaji mkono wa mitandaoni.

Conventional methods hazitafanikiwa kamwe maana CCM wamejizatiti kukabiliana na hizo njia na ndiyo maana wanaweza kufanya mambo mengi ya hovyo ambayo katika hali ya kawaida usingeweza kudhani yanaweza kufanyika karne hii.

CCM wana too many tools in the toolbox kukabiliana na conventional methods za kila aina. Inabidi kukabiliana nao katika angle ambayo hawajaizoea au kuitegemea.
 
Hujaeleweka, ongea taratibu bila kufoka kwa herufi ndogo ndio utaratibu wa mitandao.

Unasupport au kupinga nini?
 
Hujaeleweka, ongea taratibu bila kufoka kwa herufi ndogo ndio utaratibu wa mitandao.

Unasupport au kupinga nini, be brief, succinct, point yako hasa ni nini?
 
Gwajima anatumika tu. Wanajua Watanzania wanamsubiri na kumtafuta "hero" atakayewatetea. Ukiona mtu nchi hii anaongea maneno makali halafu haguswi jua hamna kitu hapo, labda mpaka reforms ikamilike, niamini nakwambia.
Line anachokisema ni mojawapo ya madai yetu. Utekaji upo,tusimame na anayeupinga. Pia anadai mengine ya msingi tuendelee kuyadai.
 

..una hoja nzuri sana.

..mimi sioni tatizo Gwajima akimlaumu Raisi na kuwakwepesha wakuu wa vyombo na watendaji wengine.

..pia sina tatizo na wale wanaomkwepesha Raisi na kuwalaumu wakuu wa vyombo na watendaji wa chini yao.

..Naamini suala hili linatakuwa kuwa approached from multiple angles.
 



Inawezekana kukubali hoja ya Gwajima ya kupinga utekaji.

Na wakati huo huo kutokubaliana na Gwajima kwenye mambo mengine kama vile hoja ya kwamba Polisi hawahusiki katika utekaji.

Jikite kwenye hoja, si mahaba au chuki na mtu.

You need distruptors. You need to get CCM out of its comfort zone. Do it and do it persistently and CCM will fall down.

Maelezo ya Gwajima yanaendelea kuiweka CCM katika comfort zone maana amewasafisha watu ambao umma ungeweza kushinikiza wawajibishwe. Ni excuse nzuri ambayo inaendelea kuwalinda wasiojulikana na wakati huo huo mkamuona amefanya kitu.
 
Gwajima kaishapata chaka baada ya mishale mingi ya kumtaka asigombee ubunge kutokana na kutofanya lolote katika jimbo 🤣🤣🤣
Hao wabunge wengine wamefanya kitu gani?
 

..mwingine anaweza kusema anayewawajibisha wakuu wa vyombo ni Raisi.


..hivyo bila kumlaumu na kumshinikiza Raisi hakuna atakayewajibishwa.

..mimi nadhani approach nzuri ni kuyatia moyo makundi yote yanayopinga utekaji na mauaji.
 
Gwajima pamoja na Luhaga Mpina wamekuwa the most disrupting people within CCM.

Tatizo lenu mnataka mtu awe disrupting 100% for 100% of the time, all or nothing at all.

Akiji contradict kidogo tu mnam dismiss kabisa.

The world does not work like that.

We work within a nuanced, contradictory, probabilistic world.

Wakati Nyerere anafanya jitihada za kupata uhuru, alikutana na Nehru wa India. Nehru akampa ushauri Nyerere, akamwambia take what you can and work with it.

We go to war using the army we have, not the army we want.

Surely Gwajima is not perfect. He is a charlatan many times over. He is self contradicting and a CCM apologist even right now.

But if he has an overarching message that advances the fight agains abductions, shall we not embrace it because Gwajima is not a saint? No.

Kuna mwanasiasa, Willie Stark, alikuwa anataka ku dig some dirt on his political opponent. Akaambiwa jamaa msafi sana hana baya.

Akasema hivii.

"Man is conceived in sin and born in corruption and he passeth from the stink of the didie to the stench of the shroud. There is always something" - Robert Penn Warren (All The King's Men)

Why do you want Gwajima to be perfect 100% for 100% of the time for any of his message to have meaning?
 
..mwingine anaweza kusema anayewawajibisha wakuu wa vyombo ni Raisi.


..hivyo bila kumlaumu na kumshinikiza Raisi hakuna atakayewajibishwa.

..mimi nadhani approach nzuri ni kuyatia moyo makundi yote yanayopinga utekaji na mauaji.
Ni kwa sababu tu ya mazoea yetu na giza tulilotandaziwa ila katika utawala wa sheria na utawala bora, mtanzania wa kawaida (ama binafsi au kama kundi) anaweza kushinikiza mtendaji wa serikali awajibike au awajibishwe kwa kumpa shinikizo yeye moja kwa moja bila kupitia kwa bosi wake.
 
Unakosea. Yeye ameenda juu, chimbuko la matatizo yote.

Ukimfukuza Jumanne Muliro wa kanda maalum. Ni kama unamuonea, ukimfuka IGP, Mkuu wa TISS ni kama huwatendei haki. Waki katika kubalance maslahi ya Taifa na maslahi ya Rais aliyechanganyikiwa. Wakikomaa wanawekwa pembeni, hata kuuliwa. Conundrum.

Wanatoa professional opinions kwa mamlaka hawasikilizwi. Muhimu kuweka lawama sehemu sahihi. Gwajima yupo sahihi 100%.
 
..mwingine anaweza kusema anayewawajibisha wakuu wa vyombo ni Raisi.


..hivyo bila kumlaumu na kumshinikiza Raisi hakuna atakayewajibishwa.

..mimi nadhani approach nzuri ni kuyatia moyo makundi yote yanayopinga utekaji na mauaji.

Sijui kwa nini mnadhani nampinga Gwajima kwa sababu ya makandokando yake. Mimi hata sipo huko. Hata angekuja Charles Kimei akasema alichosema Gwajima, ningekuja kupinga hivi hivi na kwa sababu hizi hizi.

Ngoja niwaambie distruption inayotakiwa. Si Gwajima amesema watendaji wa serikali na wateule wanajua kila kitu ila wanaogopa kutumbuliwa (ingawa serikalini hawatumbuani ila wanahamishana vituo vya kazi)?

Fanyeni hivi.....watengeni hao watendaji na wateule ambao wanahusika moja kwa moja na matukio au kushindwa kuyazuia kama wajibu wao wa kazi unavyotaka. Waondoeni heshima yote. Msihusike nao katika masuala ya kijamii. Zitengeni familia zao. Unfollow them kwenye mitandao ya kijamii. Hizo ni fujo zisizoumiza ila ni effective. Kuna meengi sana yanaweza kufanyika. Watendaji na hao wateule wakiona heshima yao imeondoka, familia zao zimetengwa hawatakubali kuendelea kuwa rubbing stamp ya udhalimu na hii pressure itamfikia bosi wao.

Mnadhani mnahitaji kufanya mambo makuuuubwa ili kuwaondoa comfortability ila mbinu nyingi zipo mikononi mwenu.
 
Uwe unasoma na historia ya watawala na majeshi yenye nguvu yalivyoshindwa na majeshi dhaifu kibinadamu...

Mfano:
➡Unajua Mussa alimshinda Farao mfalme wa Misri kwa silaha gani na watu wa aina gani?

===JIBU: Kwa maneno na maelekezo tu ya Mungu ya fanya hivi, usifanye hivi

➡Unajua Daudi alimshinda Goliath na jeshi lote la Wafilsti kwa silaha gani? Unajua Waisrael chini ya utawala wa Mfalme Sauli walishateswa na kunyanyaswa kwa kiasi gani na wafilisti?

===JiBU: Kwa kombeo na jiwe dogo la kuulia au kupigia ndege na panzi.. !

➡Hivi unajua wale wakoma walilishinda na kulikimbiza kwa vipi jeshi la la utawala wa Washami waliowatesa Waisrael kwa miaka mingi...?

===JIBU: Bila silaha yoyote zaidi ya vishindi tu vya miguu yao walipoelekea upande wa jeshi la adui zao. Haijulikani Mungu alitia nini kwenye vishindo vya miguu ya wakoma. Lakini lililo muhimu ni kuwa, jeshi la maadui liliposikia vishindo waligeukana wao kwa wao na kuanza kupigana risasi na kuchomana visu...!!

➡Unajua Gidioni masikini ambaye hakuwaga na lolote wala pesa zozote aliweza vipi kulishinda jeshi la utawala wa Wamidiani uliokuwa unaonea, kuwanyanyasa na kuwatesa Waisrael...?

===JIBU: It was really simple. Alitumia wanaume majasiri 300 tu kwa kutumia silaha rahisi sana ya maelekezo ya maneno tu ya fanyeni hivi, msifanye hivi, baasi. Lakini aliweza kuuangusha utawala na jeshi la mamilioni ya maaskari wa kimidiani lililokuwa na sophisticated war tools, pesa na teknolojia ya kisasa ya kijeshi..!

##Nini maana ya kukupa mifano hii yote toka kwenye kumbukumbu ya historia iliyoandikwa kwenye Biblia..?

Ni ili ujue na kuelewa kuwa wakati wa Mungu Yehova ukifika, hakuna linaloshindikana wala kuzuilika...!!

Pamoja na mbinu na mikakati yote ya CCM waliyozoea kuitumia ili kuendeleza utawala wao wa kiovu, ukifika wakati wao wa kufa, watakufa tu...!

MUNGU AKIWA UPANDE WETU, NI NANI ALIYE JUU YETU..?

Labda useme wewe mwenyewe kwa kinywa chako HUAMINI KAMA MUNGU YEHOVA YUPO NA ANAWEZA KUTENDA MAKUU. Hilo sasa litakuwa ni tatizo lako binafsi...
 
tangu atuahidi kwenda biminghamu sijawahi mwamini tena
 

..hicho ulichopendekeza ni ZIADA katika yale ambayo wenzako wanayafanya. Ni jambo zuri.

..sasa usiwavunje moyo wenzako, kwani ukifanya hivyo na wenyewe watapata uzito kuunga mkono wazo lako.

..mimi nimekuelewa. Wazo lako ni zuri. Mawazo ya Gwajima ni mazuri. Mawazo ya Chadema na wengine nayo ni mazuri.
 
Huoni hiki ndio inachokitaka. Imagine Gwajima ni mtu wao na wakimfungia inakua kama mfano kwa wengine lakini ki uhalisia yeyr hajaguswa. Ni bosheni tu.
 
Gwajima kashafanya disruption yake, anavyojua yeye, kwa njia yake.

Kama unaona haitoshi au haifai, fanya yako wewe nawe unavyotaka tuone.

Hawa CCM wasio na haya ndiyo unafikiri utawabadikisha kwa kuwatenga kijamii? Wakati wao ndio wana power?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…