Kumuamini Askofu Gwajima ni kutopevuka kisiasa na kuuzwa kirahisi katika propaganda

Gwajima hajawai kua mpinzani wamesahau babu wa Loliondo Gwajima anatumika watu wametoka kwenye REFORMS
Gwajima anatumika vipi? Angeweza kula bata akikaa kimya, akiunga juhudi zote. Anapata faida gani akijaribu kuisadia nchi isimame kwa watu wote?
 
Umemsoma vibaya sana Machiavelli. Rudi kumsoma upya hasa ukiwa new Prince.
nasema hivi sitokuja kushangaa siku nikijua haya yote aliyoyafanya Gwajima ni mipango kama mipango mengine ya CCM. There is a power in controlling narratives and to keep staying in power CCM lazima watengeneze drama,adui feki ili wao ndio wawe on controll. Hawaogopi hasara wanajali power.

We hushangai wale raia wa nje waliokuja na kufanyiwa vile bila kujali? Unadhani ili kubalance mjadala lazima mtu kama Gwajiboy atokee abalance narratives. Ile siku ya pili pale bungeni walivoanza kumjibu na kumshambulia Gwajima hapo hapo nikawaambia masela wangu kua mchezo kwisha,watu washaingia mzigoni. Gwajima asingejibiwa ndio ningeamini yupo serious.
 
Mdude,No reforms,Maria Sarungi speech yake ulaya. Yote haya yashasahulika mnamjadili gwajima. 😂😂
Tanzania leo inajadili haki zao za kidini, kisiasa, kiuchumi. Vyote hivyo vimechoea uelewa wa Watanzania. Gwajima ni mchango muhimu japo unacheka kama zuzu kwa point muhimu kutetea haki zako za msingi kama haki ya kuishi, kuabudu, kutetea haki yako.
 
CCM means business. Bahati mbaya wengi sana wanashindwa kuona the big picture.

Gwajima kau frame mjadala kwa nia ya kuuspin, wao hawaoni madhara yake, wamebaki kumsifu kisa amepata ujasiri wa kuongea na wakiona kanisa limefungwa wanaona, yes huyu ndiye mkombozi wetu. Hawajui alichofanya ndiyo kinapoteza mjadala kabisa kuliko hata angekaa kimya.

Tuna safari ndefu sana.
 


Hii ndiyo inaitwa ''akili nyingi huondoa maarifa'' Yaani unafikiria jambo dogo kwa kutumia akili nyingi mpaka unapata jawabu tofauti kabisa kabisa. Sikilia: take it simple!
Tatizo hamjaona damage ya framing na spinning aliyoifanya Gwajima yenye nia ya kubadili mjadana na kuwapotezea dira ya kujua nani muanze kumwajibisha. Hii damage ni kubwa kuliko mnavyodhani.

Watawala wanacheza na weakness ya mtanzania ambayo ni kuwa na huruma. Wakiambiwa watendaji na wateule wanajua kinachoendelea ila wanaogopa kupoteza kazi, wanajua watanzania wengi wakijiweka kwenye viatu vya hao watendaji na wateule watasema "daah halafu kweli, hata mimi ningekaa kimya maana hata nikisema lolote nitatumbuliwa, familia yangu itaathirika na hakuna kitakachofanyika". Huu ndiyo utakaso ninaosema Gwajima amefanya.

Kaeni chini mfikirie kwa umakini madhara ya hii "spinning" kabla hamjasema amefanya kwa nafasi yake. Kuna sababu niliita hii ni "high level propaganda", nilijua wachache sana watanielewa.
 
Hutakiwi kumuamini mwanasiasa yoyote. Judge tu anachozungumza wakati huo kama kina maslahi kwako na kwa nchi.
 
Hahaha wakenya waliruka na sisi na kimataifa tulishakua maarufu kwa msala ule. Na ukimya wa watanzania huku nafsini mwao wana dukuduku iliwaumiza kichwa sana na the safest way ni kuwatafutia a safe space au mtu wa kuyatoa madukuduku ya moyoni ya watanzania.

Ogopa sana raia wakianza kukususia na kukaa kimya huku wanajua kila kitu. Mkombozi wetu from no where akaja na akafunguka yoote tuliyoyataka kuyaskia tena kwa ustaarabu sana. Nafsi zikapumua na kupongeza huku wapinzania wakiwa hawapo nyuma kumpa sapoti huyu nabii yetu aliyejitoa mhanga. Nakumbuka kuna Stori lissu anasema Dalali wa Lowassa Chadema alikua Gwajima 😂😂.
 
Mkuu tunaangalia kinachosemwa siyo mtu anayesema, hoja ya Mchungaji Gwajima nikuulize tu ni uongo au la?..
Tujikite kwenye hoja na siyo " Fallacy ad hominem"
 
Wewe umenielewa vizuri na umesoma vizuri siasa za Tanzania zilivyo. Ni wachache wamepata bahati hii.

Baada ya muda utasikia Gwajima amehamia ACT na ile "divide and conquer" itaendelea.

Watatokea maaskofu watatu wa kanisa lake, watasema wana taarifa za ndani za siri kuwa kanisa lao linafadhiliwa na watu wa kutoka nje wenye nia za siri za kuichafua nchi. Watakuwa vague ila effective. Win win kwa pande zote huku Gwajima akienda kukichafua huko ACT na mjadala wa utekaji utakuwa umevurugwa rasmi. Hakuna tena mtu mwingine atakayekuwa na ujasiri au uwezo wa kuanza kuwaelimisha upya na kuwarudisha watanzania waliangalie suala hilo katika muktadha sahihi na kufanya maamuzi sahihi kukabiliana nalo. Hii hatari ndugu zangu hapo juu hawaioni.
 
Tunywe bia na kuangalia kideo mkuu. Kunywa bia ndio kilichobaki.
 
Tunywe bia na kuangalia kideo mkuu. Kunywa bia ndio kilichobaki.
Kinachonisikitisha ni njia hii ambayo CCM wameamua kupeleka siasa za Tanzania.

Kwa miaka mingi tulitumia rasilimali nyingi za nchi kuyapinga haya mambo nchi zingine, badala yake kibao kimetugeukia wenyewe au kama Simba wanavyoweza kusema ubaya ubwela umewageukia, tumekuja kuyakumbatia mambo hayo hayo yatuumize wenyewe.

Tumekumbatia the worst kind of politics. Kutoka hapo ni ngumu mno.

CCM hawataki kusikia na wanaogopa external intervention na interference ya aina yoyote, ndiyo maana unaona nguvu kubwa kupita kiasi iliyotumika kwa yule mganda na mkenya, maana wanajua ni hiyo njia na sisi tuliyoitumia na ndiyo iliyomaliza huo uovu katika nchi nyingine. Wanaogopa kivuli chao wenyewe.
 
haihitaji hata kuwa na elimu ya msingi kujua yanayoendelea nchini, na kujua kwa nini gwajima anashughulikiwa. amekemea kutekwa, watu mapovu juu. kweli kuna mtanzania anaamini nchi hii haina kutaka na kuua watu? kuna mtanzania anaamini nchi hii haina unyanyasaji? jana tu pale kisutu uliona yule polisi alivyokuwa anampiga virungu yule mwanachadema? wanaamini bado tupo enzi zile ila wakati wa Mungu ni bora zaidi, watakuja kuyajutia yote hayo siku moja.
 
Kwani lazima kukubaliana na kila neno la Gwajima?

Mkuu, yani ushatudharau sana na kuona Gwajima katushikia akili?
 
Gwajima kaishapata chaka baada ya mishale mingi ya kumtaka asigombee ubunge kutokana na kutofanya lolote katika jimbo 🤣🤣🤣
Mi niliwaza ana hofu kubwa ya kupoteza ubunge, au labda ushapotezwa kwa inteligensia yake, ameona upepo ni mkali upande wake hivyo anatafuta kiki kubwa ili kuwashinda wapinzani wake kupitia kuonekana a hero kwenye madhila makubwa ya utekaji , au labda ni inside job kuzuga watu, ila pia niliwaza labda ana agenda kubwa zaidi kama kugombea urais agenda ambayo itampa bajeti kubwa toka nje kupambana kwenye ulingo mkubwa ambao anajua kabisa atashindwa ila mpunga utakuwa umeingia , he is a pure business mind! Hivi ile video ipo?
 
Fantacy
 
Agenda setting
 
Kuiamini sisiemu je?
 
Jamaa umeongea pumba sanaa mtu ameongea vitu vizito sanaa af wewe unaita propaganda
 
Kusema kuna kakikundi kanakojitegemea kanakofanya utekaji halafu unasema hakihusiani na vyombo husika ni njia ya kuwatakasa wahusika na kuwaondoa katika lawama ya kile kinachoendelea
Hukusikiliza vziuri video ile ya press conference, laiti ungesikiliza yote na ukaielewa usingequote hapo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…