Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

H
Mkuu, Imani yangu ni level za juu, siongei kwa hisia Nina nguvu za Rohoni...

Naweza kuona kuwa huyu ni Nabii feki au sio...

Hata wewe tukikutana na wewe nakujua mpaka ukoo wako...

Huna mamlaka ya kumuita mtu Wakala wa Ibilisi wakati hujapima Roho kwa njia ya Roho Mtakatifu
Hayo yatakuwa ni mapepo ya utambuzi ukadhani ni nguvu ya Roho Mtakatifu 🤔
 
Kabla ya kumpinga Nabii acha hisia na maneno ya watu acha mazoea na kukariri..
Manabii wa kweli wapo na wa uongo wapo.

Jukumu ni lako kuomba mwalimu Roho Mtakatifu akujulishe na atakujulisha kuwa Nabii ni wa kweli ama sio wa kweli...
 
Ukifika pale Temboni unataka kumuona Kuhani Mussa Richard, kuna dau kama ilivyo kwa manabii wengine ila jamaa kaongeza kitu kinaitwa FAST TRACK. Hiyo ukitoa haina foleni, ile unamaliza kuhesabu pesa tu huyu hapa anakufanyia maombi.

Ila msisahau kubeba pesa za kununulia vifaa vya kiroho ambayo pia vina grade zake. Kuna vya matokeo ya papo hapo, na vile vya gradually Yaani mdogo mdogo.
Imeandikwa,
Njooni kwangu ninyi nyote mliolomewa na Mizigo, nami nitawapumzisha......

Pole sana wanadamu mnaoteseka na kuhangaika kutafuta suluhu za matatizo, mahangaiko ahueni za kiroho na kimwili kwa ghazarama zinazowadidimiza zaidi kijamii na kiuchumi...
Poleni sana.....

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Wapendwa, miongoni mwa tatizo linaloitesa jamii hii ya kikrusto, sio maarifa. Ni uelewa na ufahamu duni juu ya masuala ya kiroho...

Ukielewa Roho na kweli, hutalipishwa gharama kununua huduma za kiroho.

Nawaombea kwa Mungu awajaalie ufahamu na uelewa wa kutosha juu ya Roho Mtakatifu na wawe tayari kuskia sauti ya wito wa Mungu katikati nafsi zao, kabla ya kwenda kuitika wito wa mwanadamu.
 
Ukifika pale Temboni unataka kumuona Kuhani Mussa Richard, kuna dau kama ilivyo kwa manabii wengine ila jamaa kaongeza kitu kinaitwa FAST TRACK. Hiyo ukitoa haina foleni, ile unamaliza kuhesabu pesa tu huyu hapa anakufanyia maombi.

Ila msisahau kubeba pesa za kununulia vifaa vya kiroho ambayo pia vina grade zake. Kuna vya matokeo ya papo hapo, na vile vya gradually Yaani mdogo mdogo.
Wajinga ndio waliwao .
 
Back
Top Bottom